Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Tanzania Nyabuchwenza Methusela akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete risala ya Baraza la watoto katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar jana jioni.Katika hafla hiyo Rais Kikwete aliongea wawakilishi wa watoto na kujibu maswali mbalimbali aliyoulizwa na watoto hao kuhusu masuala ya haki za watoto. JK akijibu maswali mbalimbali aliyoulizwa na
wajumbe wa Baraza la Watoto Tanzania wakati alipokutana nao
JK katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Watoto Tanzania muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo nao na kujibu maswali mbalimbali yahusuyo haki za watoto
JK akiwa na wajumbe wa Baraza la Watoto muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo nao


JK akiagana na wajumbe wa Baraza la Watoto muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo nao





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2010

    Hiyo picha ya tatu nimeipenda sana.

    Kids are our future.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2010

    Mheshimiwa JK, nina suali kwa vile uliongea juu ya haki za watoto, je elimu ni moja wapo ya haki za watoto? jee unajua kama Sekondari Kibungo Juu ina wanafunzi 270 na mwalimu ni mmoja tu? jee hiyo ni haki gani? Jee unajua ni sababu gani zinazowafanya walimu kutokaa huko? ni nyumba na usafiri, jee kwa nini serikali inatumia mamilioni katika sherehe mbali mbali na pia kuwapa wabrazil, ilhali watoto wa taifa la kesho wanakosa elimu ya msingi?

    Michuzi usiitie kwenye kapu hii, ni lazima JK ajibu hii scandal ya Sekondari Kibungo Juu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2010

    Kweli Obama kawapa changamoto ma Rais wengine kuwaita watoto ikulu ni kwa mara ya kwanza kuona hiyo ni copy paste ya Obama mpakaa mavaaji

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2010

    hivi hili baraza la watoto likoje,linaundwa na watoto wapi na wanateuliwa vipi,wanakutana na raisi mara ngapi kwa mwaka,je kuna mtoto yeyote mwenye uwezo wa kumuuliza raisi swala la kumchalenge katika utawala wake?..kwa tanzania ni watoto wachache sana wanaoweza kufahamu kinachoendelea katika siasa ukiacha wanayofundishwa shuleni, wasiende kumtukuza tu kama kaka na dada zao wa dodoma,mi nahisi mamluki tu wale hata sio wanafunzi,angalia hata sura zao wengine sio kabisa.
    Mdau wa hyderabad.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 15, 2010

    hivi hili baraza la watoto likoje,linaundwa na watoto wapi na wanateuliwa vipi,wanakutana na raisi mara ngapi kwa mwaka,je kuna mtoto yeyote mwenye uwezo wa kumuuliza raisi swala la kumchalenge katika utawala wake?..kwa tanzania ni watoto wachache sana wanaoweza kufahamu kinachoendelea katika siasa ukiacha wanayofundishwa shuleni, wasiende kumtukuza tu kama kaka na dada zao wa dodoma,mi nahisi mamluki tu wale hata sio wanafunzi,angalia hata sura zao wengine sio kabisa.
    Mdau wa hyderabad.

    ReplyDelete
  6. Ndoto ya mchana,SwedenJune 15, 2010

    Hii nadhani ni kwa Rais kujinufaisha kisiasa na kuongeza umaarufu wa kupata kura.Tanzania haina sera nzuri za kuwajali watoto.Viwanja karibia vyote vya kucheza watoto zimeuzwa.Watoto hawana haki ya msingi wowote Tanzania wengi wanaishi kwenye maisha ya manyanyaso na kuteseka.

    Ndoto ya mchana,Sweden.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...