JK akimkaribisha ikulu jijini Dar Meya wa jiji la Instanbul, Uturuki, Mstahiki Kadir Topbas jana jioni.Baadaye viongozi hao wawili walifanya mazungumzo
Mwenyekiti wa Shirika la ndege la uturuki Bwana Hamdi Topgu akimpa zawadi JK wakati alipomtembelea Ikulu jijini Dar. Mwenyekiti huyo wa Shirika hilo la Ndege alifuatana na Meya wa jiji la Instabul.Shirika la ndege la Uturuki linaanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi Uturuki.
Jk akiwaonesha mandhari ya ikulu wageni wake Meya wa jiji la Instanbul Bwana Kadir Topbas(kulia) na Mwenyekiti wa Shirika la Ndege la Uturuki Bwana Hamdi Topgu wakati walipomtembelea ikulu jijini Dar



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2010

    safi sana tanzania hadi Uturuki. ulaya hiyo !!
    wasitunyime viza tu !!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2010

    Mtu kama Kadir Topas ndio vidume tunaowataka waje ili wawape hamasa viongozi wetu ktk uboreshaji wa nchi.
    Je Kadir Topas ni nani?
    He was born on January 8, 1945 in Altıparmak village of Yusufeli district in Artvin Province, Turkey. Kadir Topbaş moved in 1946 with his family to Istanbul. He earned a PhD in architectural history from Istanbul University following his education of theology in 1972 and architecture in 1974. After working as preacher in Edirne, teacher and freelance architect in İstanbul, he served between 1994 and 1998 as advisor to mayor Recep Tayyip Erdoğan(ndio Prime Minister now wa Turkey nani kidume usipime kaka) for the restoration and decoration of palaces and other historical buildings in Istanbul.
    Mdau Edinburgh Uk

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2010

    Mh Rais, Naomba tusijishushe sana Tanzania, Rais wetu, Ikulu Yetu na watu wetu, Ugeni kama huu ungeacha meya amkaribishe meya mwenzake au ata Waziri maana ni Ugeni mdogo sana.

    Meya yoyote wa DSM au ata hiyo Uturuki akienda USA au nchi yoyote hakuna Rais wao atakae jitokeza na kuwakaribisha Ikulu, Ikulu ni mahali muhimu sana. Angalia wasije wakatununua hao jamaa.

    MtAnZaNiA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2010

    Nchi za wenzetu mpaka mayor anasafiri nje ya nchi, ingekuwa bongo angeenda rais mwenyewe utafikiri hakuna wasaidizi

    Mdau Indiana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...