Mwalimu afundisha shule nzima peke yake!
Mkuu wa Sekondari Kibungo Juu, Tarafa ya Matombo, Bw. Chapembe Chapembe, ndiye mwalimu pekee anayefundisha wanafunzi 270 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na amelazimika kutoifunga shule hiyo kwa likizo iliyoanza Juni mwaka huu.
Uamuzi wa kuendelea kufundisha madenti hao wakati wa likizo ni kwa ajili ya kuwawezesha madenti wa kidato cha nne na pili ambao wanatarajia kufanya mitihani yao mwaka huu wamudu vyema kufaulu masomo yao.
Mwalimu Mkuu huyo alisema hayo juzi mjini Morogoro katika hafla ya kumkabidhi pikipiki kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh. Issa Machibya, baada ya kutambua ushupavu wake wa kujituma katika kufundisha kwenye mazingira magumu, uwajibikaji na kuipenda kazi yake.
Kwa mujibu wa Mwl. Chapembe, shule hiyo ilianza mwaka 2007, na kati ya wanafunzi hao 114, wasichana ni 81, mwaka huu ilipangiwa wanafunzi 79 wa kidato cha kwanza na inatarajia kutoa wanafunzi zaidi ya 53 wa kwanza wa kidato cha nne.
Alisema shule hiyo iliyopo katika uwanda wa milima na miinuko, inakabiliwa na changamoto za kukosa walimu na nyumba za kuishi, hali iliyomfanya kubaki peke yake na mwaka huu wanafunzi wake watafanya mitihani ya kumaliza sekondari.
“Walimu wote wanaopangiwa Kibungo Juu hufika na kuondoka kutokana na mazingira magumu … usafiri ni wa shida na nyumba hakuna,“ alisema Mkuu wa Shule.
Aliongeza: “Mimi mwenyewe ninaishi Kijiji cha Kiswira ni umbali wa zaidi ya kilometa 40 kutoka ilipo shule, na mara nyingi nalazimika kupiga kambi shuleni ili kuwafundisha vizuri wanafunzi wangu,” alisema.
Mkuu huyo alisema amelazimika kuwatumia wanafunzi wa kidato cha nne wa Sekondari ya Tawa kufundisha wenzao wanaotarajia kufanya mitihani mwaka huu kwa baadhi ya masomo.
Wanafunzi wa shule hiyo wengi wao wana uwezo mkubwa kiakili, lakini wanachokosa ni nyongeza ya maarifa na mbinu za kitaaluma kutoka kwa walimu wenye taaluma ya masomo ya sekondari.
“Bado ninawahurumia wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kama watamudu kufanya mtihani kikamilifu … ninaona ipo hatari ya wanafunzi kushindwa mitihani yao ya mwaka huu,” alisema Chapembe.

kaka Michuzi hebu tuweekee account number au paypal jamani tumtumie huyu mwalimu hata vijisent vyetu. Huyu nahitaji kuwa mwalimu wa mwana na anastahili zaidi ya pikipiki.
ReplyDeleteHivi hao wabunge wanaona haya kweli?
Wale waliokuwa hawatufahamu tuliokuwa tunapiga kelele juu ya kuilipa brazil mamilioni kuja kucheza mechi ya kirafiki sasa yaoneni haya! Unadhani ni nyumba ngapi za walimu zingeliweza kujengwa hapa?
ReplyDeleteTenga na wenzio haya basi wakija hao watalii wenu hakikisheni wanafika huku kuona maendeleo!
Inauma jamani ahhh
Mafanikio ya shule za kata!! Michuzi fanya twende tukaitembelee hii shule, usafiri juu yangu!!
ReplyDeleteChe.
JK ni lazima ajibu hili, ilikuwaje kuwaje akaruhusu mamilioni yatumike kuileta brazil tanzania wakati watoto wa mtanzania mnyonge wanateseka namna hii?
ReplyDeleteNa kama jawabu ni kuwa hakuwa anajuwa hili basi yeye na waziri wake wa elimu ni lazima wawajibike, hii ni scandal ya mwaka!!!
Yaani hapo ningekuwa PR wa JK ningemshawishi mama Salma ajitolee kufundisha na kutoa mfano ambao ungesaidia kuwashawishi kutozikimbia shule za vijijini. Watu wanatoka Korea, Japan na marekani kuja kujitolea na sisi tumefunga mikono yetu kama sio tatizo letu.
ReplyDeleteI got idea, get rid of all wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wabunge maalum,pamoja na kupunguza size ya bunge. The money saved could be used to invest on schools. Bila shule the future is bleak, because few educated sons and daughters wa viongozi wont be enough. We dont need wafadhili to help us on this. Its a shame beyond belief 46 years after independence the education system is still dreadfull.
ReplyDeleteLord help us!!
Nyie mnaoponda kuhusu ujio wa Brazil nafikiri ni vyema mngekuja na sera nyingine ya maana hii ishapita. Binafsi naona kwamba kwa kua tunalengo la kuitangaza nchi yetu basi tufanye kitu kimoja. TFF kushirikiana na Serikali watafute timu moja huko bondeni kama ni Ujerumani, Ureno, Uingereza au Argentina waiombe ije kucheza mechi hapa kiingilio cha chini kiwe ni Tsh20,000/= na cha juu angalau Tsh150,000/= hivi mapato yatakayopatikana basi 60% ziende kujenga nyumba za walimu kama wa shule hizi walau tukijenga tano kila mkoa kupitia wapenzi wa kandanda sio mbaya . Tutakua tumeitangaza nchi na pia tumewawezasha wananchi wenzetu kupata walimu au mnasemaje wadau?
ReplyDeleteHuyo mkuu wa mkoa badala ya kugawa pikipiki alitakiwa aachie ngazi, na yule aliyekuwepo awali anapaswa kutoa maelezo kuhusu utendaji wake mbovu. This whole thing falls, in overall, onto JK and his poor leadership cadres. Ovyo sana, mimi siwaheshimu hata chembe, nawaona ni wakoloni tu katika ngozi nyeusi. Ovyo sana!
ReplyDeletewewe mdau unaetaka JK amshawishi mkewe kwenda kusomesha huko, umesoma ripoti yote kwanza? kama umesoma sasa sema atakaa wapi ikiwa hakuna nyumba za walimu? au kuna ikulu ndugo huko?
ReplyDeletemdau wa Mon Jun 14, 09:59:00 PM, nakubaliana nawe kabisa, suali lililopo ni ni nani atakaemfunga paka kengele?
ReplyDeleteHii habari niliitoa hapa, nilishindwa tu kuweka link
ReplyDeletehttp://www.darhotwire.com/home/news/2010/06/14/mwalimu_afundisha_shule_nzima_peke_yake.html
Hii ni moja tu ya shule lukuki zenye tatizo kama hili nchini mwetu. Hii ndiyo adhali ya kujenga shule kisiasi zaidi kuliko kitaalamu. Haiwezekani ukajenga shule wakati haujaandaa walimu, hujaandaa mazingira ya kufundishia, it doesnt make sense..!!
ReplyDeleteso sad
ReplyDeleteHOW ON EARTH COULD SOMEBODY TEACH TEN SUBJECTS ALONE IN AN ENTIRE SCHOOL, THAT IS WHY STUDENTS FROM THOSE KIND OF SCHOOLS DO NOT PERFORM WELL. IT IS UNDREAMABLE DREAM TO GET SOMEONE FROM THAT KIND OF SCHOOL TO GO ALL THE WAY HIGH SCHOOL OR TO UNIVERSITY!!!
ReplyDeleteWewe mwalimu unayejitia kimbelembele na ukome kuzaliwa Tanzania. Wahi kununua tiketi uwaachie ufisadi wao, la sivyo utakufa maskini. Hakuna ushujaa wala nini, wenzio wanakuona bonge la lofa tu.
ReplyDeleteKwanza ningekuwa na nafasi ningekutimulia mbali kewa sababu pamoja na kuwa mwalimu mkuu, bado hujui kwa nini upo hapo. Unaruhusu vipi shughulii za shule ziendelee bila ya kuwa na nyenzo muhimu kama walimu n.k?
Haiingii akilini kuwa wewe unajua masomo yote, hivyo ni wazi kuwa unawafundisha MADUDU hao wanafunzi wako. Wewe unazalisha mambumbumbu wa kesho wa kupigia kura sisiemu.
Ni kosa la jinai kuwafanya wanafunzi wako mbumbumbu wawafundishe umbumbumbu wanafunzi wengine hali wewe unaona sifa eti umekuwa krietivu.
Tunaelekea kubaya. noo, tupo pabaya kwa kuti kavu
Nina imani kuwa zaidi ya kumpa pikipiki, wanafanya jitihada za kumpunguzia mzigo huo mkubwa!
ReplyDeletewewe anonymous wa Tue Jun 15, 12:56:00 AM, kwani waliotembea nchi nzima kutoa ujinga na kufundisha elimu ya watu wazima walikaa wapi? hao wakorea, wamarekani na wengineo huwa wanakaa wapi? mapinduzi ya kweli ya elimu hayatakuja kwa kujenga madarasa na nyumba za walimu tu bali kwa watu kujitolea. Mama Salma hatakosa nyumba ya wenyeji kufikia na hapo ndipo PR itakaponoga kuonyesha yuko pamoja na watanzania wa hali ya chini.
ReplyDeleteInasikitisha sana wakati mwingine huwa na waza tupo dunia ya ngapi????? Eeeh baba wa Taifa hayati Kambarage utukumbuke huko uliko hawa viongozi wotee uliwasomesha bure kabisa na walikuwa wakinywa maziwa pale mlimani na kulala bureeeee kabisa wakiapa watakuja kutuletea maendeleo nini hiki? Tanzania ya leo sio kama ya mwaka 47 nafikiri Tanganyika ilikuwa na maendeleo zaidi kuliko Tanzania! Mungu akulaze mahala pema peponi Baba yetu Kambarage daima tutakuenzi ni mm mpiganaji mwenzio tuliokuwa pamoja kwenye Azimio la Arusha Aaamin!
ReplyDeletewewe anon Mon Jun 14, 11:48:00 PM, hivi unaishi tanzania? unataka watu wachangie kujenga shule? namna gani wewe? huoni watu tunaendesha kampeni ya kuchangia CCM ili wazidi kunenepa vitambi wewe unataka kujenga shule?
ReplyDeleteby the way idea yako nzuri tukipata pesa nyingi tutaweza kununua ndege mpya ya rais na magari mepya ya mawaziri na wabunge. Watoto vijijini wanachotaka kujua ni misimu ipi ya kupand ana misimu ipi ya kuvuna, wakijua kuhesabu pesa imetosha!
Hii ndio Tanzania yetu!
wewe anon wa Tue Jun 15, 09:24:00 AM una bichwa maji? umesoma maelezo ya mwalimu mhusika? nini amesema sababu ya kutokuwepo walimu huko? Tatizo ni nyumba, well kwa nini basi JK hajengi nyumba na walimu wakaenda huko? hakuhitajiki PR hapo. infact kwa maelezo yako mwenyewe unaonyesha kuwa hiyo PR itakuwa ina walakini, kwa sababu mke wa rais kila mtu atataka kumpa mahali pa kukaa wakati walimu wa kweli hakuna atakaekubali kumueka mwaka mzima wa masomo!
ReplyDeleteNdugu yangu anonymous Tue Jun 15, 05:42:00 PM, pamoja na ubichwa maji wangu nafahamu kuwa Serikali imejenga asilimia 1 tu ya nyumba zinazotakiwa na walimu. Sasa kwa spidi hii bado unataka tuzisubiri hizo nyumba ndio tutume walimu au tuanze polepole na kuwahamasisha wanavijiji wawahifadhi hao walimu? Na ni nani atakaeweza kuwahamasisha hao wanavijiji? Suluhisho hili sio geni liliwahi kutumiwa katika miaka ya 60 na tulifanikiwa kupunguza ujinga.
ReplyDeleteNapenda kuwafahamisha kwamba hata mkuu wa elimu mkowa hawan nyumba, nyumba zao ziilikuwa za serikali na zimeuzwa, sasa kama bosi hana nyumba atafikiria namna gani ya mwalimu kuwa na nyumba, wakati nyumba zinauzwa watu wengi waliopo kwenye hii blog walikuwa wanpigania kununuwa, sasa matokeo yake ni kama hayo. Tatizo ni kwamba wakija wakenye kufundisha kwenye hizo shule mtasema kwamba kazi zinachukuliwa wakati watanzania hawatki kukaa vijijini. Hongera kwa huyo mwl mkuu, huyo ndiyo mtanzania halisi aliyebakia anaestahili sifa kwani anajuwa umuhimu wa kizazi kijacho. Inagawa wanfunzi wake watafeli lakini watamkumbuka kwa kazi nzuri aliyofanya. Wakati wanfunzi wa mjini Dar watafulu kwa kuiba mitihani. Ndugu Michuzi naomba jina lake na anuwani yake nimtumie chochote.
ReplyDeletejamani hawa ni watoto wetu, sasa basi kama wanatuhusu lets do something kama wadau, tuchange chochote ulichonacho ili tupate nyumba hata moja ya walimu, this is so sad, matokeo yake watoto hawasomi waishia kuolewa
ReplyDelete