Kina Ras Makunja wakichukua picha ya kocha marcio maximo na wadau wakati wa mechi ya Taifa Stars na Brazil pale neshno.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2010

    Kwa hapa Ulaya hiyo ni kashfa kubwa sana..
    kwani wametumia muda wa kazi iwalipayo mishahara yao (kodi za wananchi) kufanya shughuli binafsi.

    Endapo ingetokea vurugu na watu wangeumia ingebidi wawajibike kwa kushindwa kuangalia usalama kwa wakati huo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2010

    Hawa mapolisi hawajui kabisa WAJIBU wao ni nini.
    Kwa tukio la shabiki kuingia uwanjani ni kashfa kubwa sana kwao.
    Endapo angekuwa na KISU na akamchoma mchezaji KAKA wa Brazil, nadhani hawa "WAPIGA PICHA" ndiyo wangetakiwa kufunguliwa mashtaka ya UZEMBE.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2010

    ya leo kali.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2010

    katika hali ya kawaida mimi sioni kama kuna tatizo, maana shughuli za maaskari hawa zilikuwa ni kusimamia usalama wakati wa mechi UWANJANI, ilipoisha na majukumu yao yaliisha, kama wangekuwa na sehemu ya kubadilisha magwanda nafikiri wangefanya hivyo. Suala la mtu kuingia kwenye 'pitch' ni bahati mbaya kwani mbona hata huko Ukerewe yamewahi kutokea.

    Pili, Mimi nachukia kufananisha polisi wa hapa Bongo na wale wa Ukerewe, kwanza ukiachilia sana undani wa mafunzo yao na maadili waliyonayo, polisi wa ukerewe wana maslahi mazuri kiasi kwamba 'they have something to lose'.

    Nkyabo Bongo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2010

    JAMANI WATANZANIA TUACHE KUWA TAIFA LA WALALAMISHI KAMA ALIVYOWAHI KUSEMA RAISI, HEBU TUANGALIE NAFASI YETU KIELIMU KAMA INAVYOONEKANA KWENYE SHINDANO LA ZAIN VYUO VIKUU, TANGU LIANZISHWE NAFASI YETU IKILINGANISHWA NA MAJIRANI ZETU IKO WAPI; WAKATI SISI TUKIFIKIRIA KUTUNGA MALALAMISHI WENZETU WANABUKUA KUTOKANA NA KUBUKUA HUKO WANAWEZA KUSHIKA NAFASI ZA KAZI NCHINI MWETU NA SISI KUBAKIA KULALAMIKA MCHANA NA USIKU, TUKUMBUKE DUA LA KUKU HALIMPATI MWEWE KWANI KUKU HUKAA CHINI AKILALAMIKA WAKATI MWEWE YUKO JUU ANGANI AKIRUKA NA KUENDELEA KUKAMATA VIFARANGA VYA KUKU AMBAVYO NI NAFASI ZETU ZA KAZI ZINAZOCHUKILIWA NA WENZETU. HAYA SASA TUENDELEE KULALAMIKA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2010

    Hata ungerushwa mkuki kuelekea uwanjani ungefika tu, kwa mtaji huu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2010

    WATOA MADA WA HAPO JUU MLIOTANGULIA KUANZIA WA KWANZA NA WA PILI

    MSIJIFANYE UJUAJI KWA SANA KAMA KWELI MPO UGHAIBUNI BASI MTAKUWA MMEFUNGUKA MACHO VYA KUTOSHA

    MIMI PIA NIPO UGHAIBUNI NA NAHUDHURIA SHEREHE MBALI MBALI ZA HUKU UGHAIBUNI NA NAKUTANA NA MATUKIO MENGI SANA YANAYOFANANA NA HAYO YALIYOTOKEA HAPO

    POLISI WA HUKU UNAWEZA KUMSIMAMISHA NA KUPIGANAE PICHA BILA WASI KUNA SHEREHE NYINGI ZA NCHI HUWA NIKIFIKA NAOMBA KUPIGA PICHA NA POLISI NA WANANIKUBALIA

    HUKU NI JAMBO LA KAWAIDA POLISI KUPIGANAE PICHA AU HATA YEYE MWENYEWE KUSIMAMA SEHEMU NA KUSHUHUDIA TUKIO LA KUCHEKESHA NA BAADAE AKAENDA ZAKE NA KUENDELEA NA KAZI ZAKE

    NA KUHUSU JAMAA KUINGIA UWANJANI ETI ANGEKUWA NA KISU MSITAKE KUWASHUTUMU WATU BILA KUFIKIRIA

    JAMBO LA MTU KUINGIA UWANJANI LIPO DUNIA NZIMA KAMA KWELI MNAFATILIA MPIRA BASI MTAJIONEA NI SEHEMU NYINGI DUNIANI MAMBO KAMA HAYO YANATOKEA TENA KWA MATAIFA MAKUBWA

    NINACHOWAOMBA NDUGU ZANGU TZ MSIWE MNA MIDOMO MIREFU KATIKA KUISHUSHA NCHI YENU WENYEWE

    KILA JAMBO LIKITOKEA HUKO TZ ETI NI MAKOSA HUKU UGHAIBUNI HALITOKEI NANI KASEMA HUKU HAYATOKEI MAMBO KAMA HAYO KAMA SIO UJINGA NA KUJIFANYA MNAJUWA KWA KUKAA UGHAIBUNI

    WACHENI USHAMBA MMEKUJA UGHAIBUNI ISIWE NDIO SABABU YA KUIPIGA VITA NCHI YENU KWA KILA JAMBO WANALOLIFANYA MNAONA NI BAYA AU NI MAKOSA

    HAO JAMAA WANA HAKI VILE VILE KAMA BINADAMU WENGINE

    mdau wa mahakama kuu ya dunia mtambo wa kutia adabu natoa cheche zangu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2010

    aibu tupu, kwanza kuchukua picha na hivo visimu ndo nini, at least wangekuwa hawajavaa uniform

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2010

    HAHAHAHAH NA NDIO MAANA KIJANA AKAENDA KUMPA HUG KAKA... HALAFU SASA WANATAKA WAKAMPIME AKILI?!!! SASA HAPA NANI WA KUPIMWA AKILI WAJAMENI ???

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2010

    Polsi nao watu jamani sio mbwa,
    stop looking everything in negative ways.
    By the way hapa ni Tanzania siyo Ulaya,mambo yakwetu yaacheni kama yalivyo msitufananishe na ulaya yenu,we cant b the same.
    Stupid!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2010

    inasikitisha sana je kina ras makunjas wanalinda usalama au wamegeuka kuwa paparazi tujaribu kujifunza askari wa usalama kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE wanavyokuwa siriasi

    ReplyDelete
  12. chakubangaJune 09, 2010

    Duh bongo!!
    Kwa mtaji huu ndio maana jamaa alifanikiwa kumkumbatia kaka uwanjani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...