Kundi la watoto washule wakigombea kofia za Karatasi zenye Nembo ya Bunge toka kwa Afisa wa Bunge bi Lily Mraba mara walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi yaliyoanza leo Mjini Mwanza. Maonyesho haya yanatarajia kumalizika tarehe 23 Juni, 2010, ambapo zaidi ya taasisi 100 za Umma zinashiriki. Mtoto ambaye hakufahamika mara moja jina lake, akisoma kwa umakini kipeperushi chenye maelezo kuhusu Historia ya Bunge huku wenzake wakimtizama mara walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi yaliyoanza leo Mjini Mwanza. Maonyesho haya yanatarajia kumalizika tarehe 23 Juni, 2010, ambapo zaidi ya taasisi 100 za Umma zinashiriki
Kundi la watoto washule wakigombea kofia za Karatasi zenye Nembo ya Bunge toka kwa Afisa wa Bunge bi Lily Mraba mara walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi
Katibu wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Bi Lina Kitosi, akimwonyesha mwananchi wa Mwanza Vedastus Rugemarila Kiapo cha Wabunge mara baada ya Kutembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi yaliyoanza leo Mwanza. Ofisi ya Bunge inashiriki katika maonyesho hayo ambayo yatafunguliwa rasmi tarehe 19 Juni, 2010 na kufungwa tarehe 23 Juni, 2010.Banda la Ofisi ya Bunge linavyoonekana katika Viwanja vya CCM Kirumba Mwanza leo mara baada ya Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma kuanza leo Mwanza.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2010

    KITENDO CHA MAHAKAMA KUTENGUA UAMUZI WA KURUHUSU MGOMBEA BINAFSI KINAONESHA NI JINSI GANI MAHAKAMA INAVYOWEZA KUTOA MAAMUZI KWA SHINIKIZO TOKA SERIKALINI NA KUWA TAYARI KUWANYIMA HAKI WATANZANIA. MAHAKAMA INAPOSEMA INALIPELEKA SWALA HILO BUNGENI KWA MAAMUZI NI KUSHINDWA KWA O KUTAFSIRI KATIBA AMBAYO TAYARI INAMPA HAKI RAIA KUPIGA KURA NA KUPIGIWA KURA BILA KUPITIA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA. HATA HIVYO MAAMUZI HAYO HAYASHANGAZI KWANI BAADHI YAO NI WAGOMBEA WATARAJIWA KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI HIVYO WANAOGOPA KUACHA KWENYE MCHAKATO WA UGOMBEAJI, HIZI NDIZO MAHAKAMA ZA NCHI ZA KIAFRIKA KWANI ZINA TABIA YA KUMLINDA BWANA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2010

    Hongereni bunge kwa kutoa elimu ya masuala ya bunge!nawaona vijana menawiri sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...