LEO NI MIAKA 3 KAMILI TOKEA MH. AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIA (PICHANI) ATUTOKE. KIFO CHAKE, KILICHOTOKEA GHAFLA, KILITIKISA NCHI NZIMA NA WATANZANIA WOTE KWA JUMLA YAO WALIBAKI MIDOMO WAZI KWA KUONDOKEWA NA MBUNGE HUYU KIJANA ALIYEJIPATIA UMAARUFU KWA MENGI, KUBWA LIKIWA MSIMAMO WAKE WA KUPAMBANA NA JANGA LA MADAWA YA KULEVYA. NA LEO, IKIWA NI SIKU YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA, GLOBU YA JAMII INAJIUNGA NA WANAHARAKATI KAMA AMINA CHIFUPA KUADHIMISHA SIKU HII HUKU TUKIMKUMBUKA MWAHARAKATI HUYU. ASUBUHI HII KUTAKUWA NA HAFLA YA KUADHIMISHA SIKU YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA KITAIFA ITAYOANDALIWA NA TUME YA MADAWA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ITAYOFANYIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA AMBAPO MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, MH. PHILIP MARMO. HAPANA SHAKA JINA LA AMINA CHIFUPA LITAKUMBUKWA


OOH JAMANI AMINA AMEFARIKI? JAMANI NINI TENA, OOH ALIKUWA MTU WA WATU NINI JAMANI KIMEMKUTA MARA YA MWISHO ALIKUWA AWATAJE WAUZA UNGA SIKUMSIKIA TENA NA HILI BOX LETU HAPA UFINI LILIKUWA GUMU SANA SASA LEO NAFUNGUA MICHUZI NAKUTANA NA HII HABARI YA KUHUZUNISHA SANA POLENI JAMANI KINA MEDI NA FAMILIA YA MAREHEMU
ReplyDeleteDah ni kama jana alipoondoka huyu dada.Anyway,ndo dunia kuna kuzaliwa na kufa.Life goes on.Misupu na wewe chunga usitake wakuchifupe kwa kuungana na mambo haya.
ReplyDeleteAnkal, Samahani kama nimekosea. kwa kumbukumba zangu Amina alifariki dunia mwaka 2007, yaani miaka mitatu iliyopita. Kama nimekosea naomba nisahihishwe. Amina, we will never forget you. RIP. Nachukua fursa hii kuwalaani wauza mihadarati/madawa ya kulevya. They will not get away with it! Amandla!!!!!!!!!
ReplyDeleteAnkal sio miaka 4 bana ni 3.Hebu rekebisha hapo juu.Anyway Amina jamani uliondoka bado mbichi kabisa, jamani kifo hakina huruma. Kila aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi hapa duniani ni chache. Hivyo jamani tukumbuke kuna kufa kesho hivyo tufanye matendo mema hapa duniani.RIP Amina chifupa.
ReplyDeleteMdau karume wa ufini.Napenda kukupa taarifa na Mohamedi Mpakanjia nae ameshafariki.
ReplyDeletemdau wa kwanza hapo juu ni kweli kipenzi chetu keshatangulia mbele za haki ni mda tu sasa, na mumewe medy hatunaye tena naye keshatangulia mbele za haki mwaka jana, Mungu awarehemu, amen
ReplyDeleteMichu, jamaa yangu mmoja ni mkemia (chemist). yeye anashuku kuwa dalili zilizosababisha kifo cha Amina ni za zile ambazo kwa kingereza zinaitwa 'arsenic/heavy metal poisoning symptoms' ambazo hata huku USA haziwezi kutambulika katika maabara za kawaida. Kama alivyosema mdau wa tatu hapa juu, wauza unga ni watu ambao hawafai kabisa. tazama huko mexico na colombia wanavyofanya unyama. wauza unga ni watu wa shetani lucifer na wana laana. AMINA RIP.
ReplyDeleteR.I.P dear amina,Yako mbele yetu nyuma,tumuenzi kwa yale mema aliyopigania mendwa wetu,Mdau wa kwanza pole sana kwa kutopata taarifa mapema ila huzuni zaidi ni kwamab hata MED hatunae tena ametangulia mbele ya haki!wameacha mtoto yatima!Allah amlinde kwa kila jambo.Inshaallah!
ReplyDeletezawadi.
We KARUME huyo "Medi" naye uneyempa pole kafa. Sasa ndugu yangu ata kama Box uwe unapitia vyombo vyetu ata kwa vichwa vya habari, sie wenyewe tukirudi Box angalau dk 2 tunapoteza kuangalia yaliyojiri. Siku ingine utasikia ...kafa pia na usijue.
ReplyDeleteAnkal Mithupu umekosea bwana...usiseme tangu atutoke..ila tangu wamuondoe.....nadhani hiyo ndo sahihi kabisa..
ReplyDeleteanonymous wa kwanza hapo juu pia Medi alifariki. RIP Amina and Medi
ReplyDeleteMwanamke shujaa, anayejiamini ambaye ndoto zake zimezimika ghafla na kutoweka katika uso wa dunia hii, kila nikisikia jina lake au kuona picha yake, moyo wangu unaumia sana, kamwe sitomsahau, mungu amsamehe mazambi yake na amuweke mahala pema.
ReplyDeletetunamuombea ALLAH ampunguzie adhabu za kaburi inshaallah. Kila nafsi itaonja umauti tufanye maandalizi inshaallah
ReplyDeleteJamani nimesikitishwa sana na comment za huyu mwenzetu mbeba box wa UFINI kuhusu kifo cha dada yetu Amina Chifupa, napenda kumjulisha tu kuwa hata huyo Medi unayempa pole naye ni marehemu (RIP. Pole sana mtoto Rahman, pamona na kukosa wazazi wote Mungu atakusaidia.
ReplyDelete