Trafiki akimpiga bao mdao aliyetanua kwenye barabara ya Old Bagamoyo road baada ya uzalendo kumshinda kutokana na foleni ndeeeeeefu ielekeayo Msasani.

Kaka michuzi pole na kazi na
hongera kwa kuendelea kutuhabarisha.
Kuna mdau alichangia suala la jiji la dar es salaam kuwa na foleni,ningependa kuongezea katika hoja yake hiyo.


Kaka mji wetu ni mji ambao tunategemea aina moja tu ya usafiri yaani ni daladala kwa akina sisi na usafiri binafsi kwa wenye nazo.


Wazo langu linaanzia hapa, mji wa dar es salaam umezungukwa na reli karibia katika kila eneo,kuanzia ubungo,tabata,mabibo,mbagala na maeneo mengine mengi sana.Kama jiji lingeweza kuzitumia hizi reli kwa kutafuta vichwa vya treni na mabehewa yasiyozidi matatu katika kila eneo nafikiri kwanza tungepunguza tatizo la usafiri na pili tungepunguza foleni.

Kwa kuwa treni ni usafiri wa haraka kufika mjini nafikiri hata wale wenye magari binafsi wangeyaacha ili kukimbia foleni na gharama za mafuta kwa hiyo kwa kiasi kikubwa foleni zingepungua kwa kuwa magari ambayo yangebaki namba yake tungeweza kuicontrol.

Pili tutakuwa tumempunguzia gharama ya maisha mtu wa hali ya chini kwa kuwa kivyovyote gharama za treni zitakuwa ndogo tofauti na ilivyo katika daladala.


Hatuhitaji reli mpya au treni za umeme kwa sasa kwa kuwa bajeti yetu haieleweki isipokuwa tunachohitaji kwa sasa ni kuanzisha mfumo huu mbadala wa usafiri wetu wa jijini,reli tayari tunayo,treni zipo na mabehewa pia yapo ni kiasi tu cha kukutana na shirika la reli na kupanga utaratibu utakuwaje.


Mwisho kaka michuzi kuhusu foleni tunahitaji kutumia barabara za mitaani kwa sasa na inabidi polisi wa barabarani wawalazimishe madereva.Kwa mfano kama mtu anatokea ubungo na polisi anajua kuwa magomeni kuna foleni basi gari zilizopo manzese zitafutiwe njia nyingine ya mtaani hata ikibidi wapite kigogo mpaka zile zilizo kwenye foleni zitakapopungua.
asante kaka ni ushauri tu.
mdau Haruna bin Rashid

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Ndiyo, usafiri wa treni ungefaa sana hasa pia kwa watoto na wanafunzi ambao mnataka kuwatenga na jamii kwa sababu za ubinafsi wenu.Pia maboti kama yale ya kamanga kutoka kunduchi, jangwani beach, kawe beach,slipway,kijichi huko kote kuwe na Ferry boats tuepuke nyanyaso za foleni na wenye daladala wanaopenda nauli lakini hawatoi huduma stahiki.Au vipi. Tubadilike. Longolongo tuu mach.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2010

    VERY GOOD POINTS !!

    Bongo kuna vichwa aiseee!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2010

    nakubalina na issue ya treni, ila kusema treni ni rahisi kuliko magari no, treni ni expensive, nchi za wenzetu wanatoa ruzuku kubwa sana kwa ajili ya mashirika ya reli despite hela ambazo tunalipa ( at least am sure for netherlands) ila kwa kweli dar tukiwa na treni itasaidia sana

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2010

    Sitaki hata kupoteza muda kutoa ushauri,maana yote yanaishia humu humu,sioni kama kuna yanayofanyiwa kazi,wadau wengi wanatoa ushauri mzuri tu,sasa sijui ni viongozi wa nchi mabomu au ni pesa za kutekeleza ndio hakuna?,yakija ya kukarabati nyumba za vigogo (Gavana BOT)na kuleta Brazil kwa billions yanawezekana fasta tu.Bul shit hili li nchi!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 15, 2010

    ushauri wangu kwa wananchi wenzangu
    mfano
    unakuta nyumba 1 ina magari manne
    a) baba ana lake kazini
    b) mama ana lake kuendea kazini
    c) watoto wana lao la kuwapeleka shule.
    d)mkata majaniya ng'ombe ana la kwake la kukatia majani

    tufanyeje juu ya hili nina mfano mmoja hapa ofcn kwetu mtu na mume wake tuko nao ofc moja wanatoka nyumba moja kila mtu anakuja na gari lake ofcn hata kama kila mtu ana program zake lakini mkipeana lift wakati wa kuja ofcn kuna tatizo gani? tuache ulimbukeni wa kujionyesha, au kuwahi na kuwapitisha watoto kwanza shuleni kwa gari moja halafu ninyi mkaelekea ofcn kuna shida gani? hatukatai magari mtu ananunua kwa nafasi yake na kwa raha zake lakini mwisho inakua karaha kwako na watu wengine tujifunze kwa wenzetu walioendelea.

    solution
    1. tungeomba serikali isimamie ,mfano gari ndogo mtu akiamsha gari ili iingie kuanzia kariakoo,na posta lazima kuwe na ushuru fulani ambao watakao umudu ndio wapeleke magari mjini,asieweza basi ataamsha gari siku moja moja( namaanisha gari ndogo sio daladala na gari za wanafunzi)

    2.serikali iboreshe usafiri wa abiria

    3. serikali iboreshe miundombinu ya vichochoroni

    4. na hizo njia alizotaja mdau hapo juu

    nawakilisha

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 15, 2010

    Mbali na daladala zilizopo, serikali iruhusu luxury town bus ambazo bei yake itaanzia sh.1000 na zaidi. kisha iweke parking nje ya mji ili wenye magari binafsi waache magari yao nje ya mji mfano wanaotokea barabara ya morogoro wapark Ubungo, watokao Bagamoyo wapark Mwenge,watokao tabata wapark Buguruni, mbalagala waache Kwaazizi ali nk. Atakeyekomaa kuingia na gari yake City Centre kuwepo na ushuru mkubwa.

    ReplyDelete
  7. Giriki MbogoJune 15, 2010

    Mdau Haruna,hauko mbali sana na ukweli kuhusu tatizo hili la usafiri kwa DSM. Cha msingi kwa serikali ni DHAMIRA YA DHATI katika kutekeleza mipango ya maendeleo wanayoweka. Mfano, mradi wa DART(mabasi yaendayo kasi)umefika wapi hadi hii leo?utakuja shangaa kusikia ile hela iliyotengwa imekwisha kwa masuala haya ya kutafuta sijui mkandarasi n.k. Huu ni uzembe ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na SIASA ZA KUFAHAMIANA,KULINDANA. HAKUNA KABISA TABIA YA UWAJIBIKAJI!
    (Haruna umerudia neno 1 mara 2 --- ROAD v BARABARA)

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 15, 2010

    Hiihoja ni ya maana sana kwa mfano watu tunaokaa gongolamboto treni inatufaa sana toka stesheni hadi pugu yaani ingependeza zaidi.tunaomba serikali iangalie kwa undani zaidi.mbona foleni isingekuwepo . ila sijui kama itawezekana maana hao viongozi ndio wenye biashara ya daladala. tuombe mungu tu kama wataweza.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 15, 2010

    hilo wazo ndio hata mimi siku zote ndio nalifikiria kuwa ndio njia mbadala ya kupunguza foleni hapa Dsm.Usafiri wa treni umekuwa ukitumika duniani kote.sijui kwa nini serikali inasitika uanzisha ufumo huu,au wanaogopa biashara za daladala ambazo zinzmilikiwa na vigogo zitakufa???tatizo la foleni dsm sio tu ni kero kwa wananchi ila pia lina negative impact katika uchumi.tuanze hata na reli ile ya kutoka Pugu hadi stesteni kwa majaribio wataona jinsi foleni itakavyokuwa imepungua katika barabara ya nyerere.Reli ipo,mabehewa yapo so sioni ugumu uko wapi!!!tuache ndoto za fly over au mabasi ya kasi,lets start by using available resources.hakuna mwananchi anaependa kutumia private car kama kuna reliable public transport!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 15, 2010

    TATIZO BARABARA NI CHACHE NAWALA SIO WINGI WA MAGARI!!
    TUNATUMIA BARABARA MOJA TU KUELEKEA MJINI SOLUTION NI KUJENGA BARABARA ZETU ZILIZOPO MITAANI YANI NDANI NASIO KUTEGEMEA HIGHWAY!!
    TANZANIA UKIONA MTAA UNABARABARA HATA KAMA NI YA VIFUSI UJUE KUNA KIGOGO AMA FISADI ANAKAA HUO MTAA SASA IMAGINE UKUTE MTAA UNARAMI

    ReplyDelete
  11. MIMI NISHINDWA KUWAHELEWA KWA NINI MUNA PIGAPIGA MAYOWE HETI FOLENI NDEFU KWANZA KILA KUKICHA MUNASEMA BONGO TAMBARARE SASA FUJO YA NINI KAENI MULE LAHA TU HUKO MUKICHOKA MUJE HAPA READING HAKUNA FOLENI MAISHA MATAMU BOKSI LINAPIGI MUKWANJA UNAKATIWA KILA WIKI BILA TATIZO NA BIA TUNAKUNYWA KILA SIKU KAMA 5 SAINGINE 10 NI MIDA MIDA YAKO TU NAKWAMBIYA KUNA LAHA WEWE MUULIZE MICHUZI HAKIJA HUKU LONDON KILA MARA MASHAVU YANAKUWA YAMETUNA ANACHEKA NA KUSHANGAA SHANGAA TUNAVYO TANUA MATANUZI BREAKIFAST NI MAYAI MUCHANA KUNA WALI MWINGI TU NA WAKUFA MUTU USIKU UNAMALIZIYA NA MATUNDA NA KILAULI. YAANI BONGO NYIE MUNACHEZA SASA MUPAKA SASA MUNALIYA NA BALABALA CHA MUSINGI NI KUACHA KUNUNUA MAGALI PANDENI DALADARA TU KWA WINGI ITASAIDIYA AMA HAMIYENI VIJIJINI MUANZISHE MAKAZI NA MATANUZI MAPIYA KABISA. NI HAYO TU NIMEONA NIWAMBIYE BILA KUWAFICHA

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 15, 2010

    HAMENI NENDENI VIJIJI VYA UJAMAA HAKUNA FOLENI KABISAAAAAA

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 15, 2010

    Kaka Michuzi,
    Majibu ya Foleni ni haya yafuatayo
    (1) Serikali kupanua barabara zote na kuongeza nyingine (lane nne na kuendelea)
    (2) Serikali kuwekeza kwenye reli/treni za mijini: Hatuhitaji hata kupita chini ya rdhi. Miji mingi tu treni zapita juu. mfano treni mya ya hapo kwa Mzee Zuma (Gautrain) na kule Zurich Uswiss, zote ziko juu ya ardhi.
    (3) Serikali kufuta utaratibu wa sekta binafsi kuenmdesha usafiri mijini. (nina maana daladala zote futaa)..why? Kwanini?...SIMPLO hakuna nchi yeyote iliyo na usafiri wa maana mijini unaoendeshwa na sekta binafsi...Hakuna. Usafiri wa Umma ndiyo suluhisho. Unawekeza katika mabasi makubwa na unaondoa vurugu. Kwanza ni gharama nafuu kwa kuwa yanaendeshwa bila faida na walipakodi wanachangia kulipia gharama kupitia kodi.

    *****PESA ITATOKA WAPI??
    GOOD: Pesa itatokana na yafuatayo
    (1) Serikali kuachana na biashara ya kununua maghari ya kifahari na kuwekeza kwenye hiisekta,
    (2) Mheshimiwa na Timu yake kuacha/kupunguza safari zake hasa za kule kwa mjomba wetu wa DC,
    (3) kupanua wigo wa kodi ikiwa ni pamoja na kuzipa mamlaka za Jiji kubuni kodi. km penalty kubwa kwa waendeshao hovyo, wakojoaji hovyo, ushuru wa magahari nk,
    (4) kupunguza ukubwa wa serikali mfano..kupunguza Wizara/Mwaziri na Taasisi za Serikali zinazoongezeka kama uyoga, kupunguza idadi ya Wabunge, Wakuu wa Mikoa/Wilaya nknk,
    (5) pale kariakoo kodi iko mingi sana, hizi sherehe za harusi nazo tuzitwange kodi, nyumba je??...TRA fuatilai hilo,

    (6)...(20) inaweza ongezewa na Ankal Kamau maana naye ni Raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ana haki ya kuchangia.


    ASANTE

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2010

    wee anony 5:02, 6:29 na 6:33 khaaa mtu huyo huyo box halipigiki leo au ulipata lift ukawahi nyumbani. Hebu usitupotezee muda watu wanadiscuss mambo ya maana wewe unatype na upper cases zako hapa unamshoutia nani?. Hebu kapige box muda wote huo uko kwenye topic moja tu...khaaa na hata kiswahili chenyewe hujui unakazania kuongea utumbo...

    Some people!!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 15, 2010

    Suala la reli lilishaongelewa wakatishirika lilipokuwa na wataalamu, na halikufatiliwa , kwa sasa shirika limejaa wezi na watu wasiokuwa na ujuzi je unafikiria ni mambilioni mangapi yatapotea kuwekawezesha hizo reli kufanya kazi, Sababu kumejaa wezi bei ya kununuwa vichwa vitatu basi kitanunuliwa kimja na kilichotumika.Kumbuka kwamba wataalamu wote walishaingia mitini wanakazi nyingine, kwa hivyo kizazi kilishapotea hapo hakuna elimu iliyoachiwa kizazi cha sasa ili wawe wafanisi na kuendeleza mradi huo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 16, 2010

    kiukweli hii ndo nia mbadala ya kupunguza msongamano wa magari,hizo njia nyingine zote hazitokuwa na suluhisho kwa mfano trafic light kuongezwa muda hii pia sio njia ya kudumu kwa kuwa hata akikaa polisi bado anaweza kutumia mda mwngi kupitisha magari ya upande mmoja lkn akirudi upande wa pili magari yamejaa.Treni ndo kitu kinachoweza kutupunguzia maumivu tunaypkutana nayo sasa ya kusafiri kilomita 10 kwa masaa 2....

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 16, 2010

    Solution ni kuing'oa CCM madarakani. Kila tatizo wanahusika. Hata leo mji unajengwa bila mipango ya 100yrs to come,unategemea nini.Kama Mwinyi na Mkapa wangepanga mji vizuri kama laivyoanza mtangulizi wao tatizo lisingekuwa kubwa hivi. Unategemea nini kwa kizazi kijacho 50yrs ahead,mji ni vichochoro vitupu, foleni mpaka mlangoni.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 16, 2010

    Upembuzi yakinifu ulishafanywa miaka ya 90 mwishoni kuhusu matumizi ya reli,wakati huo reli ya mabibo-gerezani-ilala shaurimoyo-kurasini-pugu-buguruni ilikuwa haitumiki baada ya viwanda vingi kufa ubungo,ilipendekezwa waanze kuitumia kwa usafiri wa ndani,lakini kama mnavyojua nchi yetu haijapangwa hata kiduchu,kama kuna kichaa kwenye wizara basi sahau hoja kupita yeye hakigoma.

    Usafiri wa majini pia ni rahisi kwa Dar,maji kutoka bwagamoyo mpaka mbagala ni sisi tu na mipango ya wiki endi twende wapi.Pia mito kama msimbazi na mingineyo ikichimbwa inaweza kuwa kiungo kizuri sana kwa usafi wa ndani dar es salaam,ukitembea mji ya watu,mito inasaidia sana usafiri mjini na mji baina ya mji,sisi hapa twawaza twende muziki wa bendi gani? Tunaiga maisha.

    Asanteni

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 16, 2010

    Hallow MICHUZI,
    Kaziunayofanya nakubaliana nayo. Napenda kutoa ushauri kwenye hii blog yako KERO zozote wadau wanazoziwakilisha hapa ingefaa kama wewe ungetake another level kuinterview WAHUSIKA WA KERO HIZO ingekuwa 1 + 1 = 2. Lakini kwa mwendo huu wadau wanawakilisha kero wanazitolea maoni, na kutoa solution za maana kwa mfano Maswala kadhaa yaliokwisha wakilioshwa katika blog hii kama, KERO YA TRA, FOLENI, BODI YA UTALII( Kujitangaza) na mengine mengi Ukifuatilia what we discussed on above issue utaona kwamba haKUNA HATA INTERVIEW MOJA ULIYOFANYA NA WAHUSIKA KUWASAIDIA WANABLOG KUELEWWA wanafanya nini?? kutatua matatizo hayo...Ndugu michuzi hilo tu ndo nilikuwa nalo moyoni linanikera. Mdau USA

    ReplyDelete
  20. Swala la treni, usafiri wa boti za kasi, kupanua barabara na kupaki magari nje ya mji ni POA.

    ILA pia pale mjini kuna uwezekano magari yakaingia mjini na kupata parking kwenye parking spaces kwenye maghorofa kadhaa yatakayojengwa, yenye level nne mpaka tano, hili wazo kwanza litawapatia ajira watu, nyomi kwa makampuni au halmashauri ya mji. Bila kusahau maghorofa yote mapya mjini lazima yawe na parking, hasa underground.

    Bila kutengeneza flyovers kwenye junctions hasa pale mwenge, ubungo, magomeni, fire, salander bridge, tazara, chang'ombe, kamata, shule ya uhuru, buguruni, Peugeot motors na pale DSA kilwa rd.

    Kuimarisha public transport, maana bila hili hata tufanye nini bado tatizo litakua pale pale.

    Kukaribisha matumizi ya baiskeli na pikipiki.

    Kukaribisha congestion charges kwa kila gari inayoingia mjini, sema kuanzia salander bridge, labda sh. 300 kwa kila gari.

    Lazima daraja la kigamboni lijengwe, na tuangalie uwezekano wa kujenga daraja lingine litakaloanzia kenyatta rd mpaka ocean rd.

    Asanteni

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 16, 2010

    Hii kutumia treni ni njia nzuri, ila dawa pekee ya kutoa hizi foleni ni serikali kutimiza ahadi yake ya kupeleka makao makuu yake Dodoma hapo utaona wizara nyingi mno zitaamia huko na dar yetu itakuwa imekimbiza tatizo sugu la foleni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...