Ankali Muchuzi,
Salaam to you and team.

Naomba "Msaada Tutani" kuhusu subject hii uniwekee kwenye blogu ya jamii.
Ningependa kufahamu gharama za elimu Tanzania, kidato cha kwanza hadi cha sita. na pia elimu ya juu (college/University)
Gharama hizi zinaweza kuorodheshwa kama

1). School/Tuition fees.
2). School Development Contributions/
Au contributions zozote mzazi
anatakiwa kuchangia shule.
3). Boarding Fees.
4). Books and stationary.
5). Living expenses/Pocket Money.
6). Transport Costs (per week/per month/Annual).
7). Examiniation costs (Mock exams/ Final exams).
8). Gharama zozote zingine zinazohusishwa kwenye elimu.

Ninachojaribu ni kupata hii breakdown ili kunisaidia na kuwasaidia wazazi kujua majukumu ya elimu na gharama zake.
Ikiwezekana, anayetoa comment aandike jina la shule (private/government). Course anayo/aliyochukua. Costs zingine ambazo sio specific kwa shule, naomba aambatanishe ni mji gani costs hizi zinatozwa.

Natanguliza shukrani zangu kwa wote.

Mdau Kotin karwak.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2010

    Hizo data wanazo wizara ya elimu, tafadhali wasiliana nao, au mpe homework nduguyo yoyote aliyeko TZ.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2010

    inategemea na shule, kila mtu anabei yake.uliza shule husika au chuo husika.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2010

    Asante sana mdau kwa kuweka hii ..Lakini hujaspecify unatafuta elimu ya private au public..Mimi nilikua nataka nimtumie ankal Michuzi something like this lakini kwa vile umeweka hapa najua itanisaidia na mimi kuona ninachotafuta....Mimi nataka nijue shule za public tu average ni shilling ngapi?

    Thanks

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2010

    You are not serious right? Kama una shida ya muhimu namna hiyo kwanini usimpatie mtu akafanya hiyo kazi!
    Yaani unatarijia watu tuanze 1-9 na nyongeza hapo chini za courses sijui! How can you rely on these partial information for something important like that?
    Wabongo aaah!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2010

    Mdau Kotin karwak, napenda nikushukuru kwa unachotaka kukifanya, yaani kuhabarisha jamii na wanaglobu gharama zilizo mbele yetu au gharama zinazotakiwa kulipwa na wanajamii upande wa elimu. Hii itasaidia watu kujiandaa vyema kukabiliana nazo. Lakini naona kama kiuhakika inaweza kuwa ni document kubwa kidogo kukaa kwenye blog...labda ungetoa email yako watu waweze kukutumia. Hapa watu wanaweza kuleta link na source ...wadau labda hapa tusaidiane kupata website za mashule na vyuo ili tumsaidie mdau afanye compilation, lakini mdau unatakiwa pia kufanya homework kidogo ya kupitia website za mashule na vyuo mbalimbali! wanachofanya mara zote ni kuweka gharama zao kwa sababu ndiyo information ya kwanza wanajamii wanayoitaka

    ReplyDelete
  6. ada ya shule/twisheni unaweza kupata - inarenji kuanzia 40,000 (sekondari ya serikali kutwa) hadi 5,000,000 9chuo kikuu binafsi uhandisi)

    gharama nyingine inategemea mwanafunzi anaishi wapi, anatumia usafiri gani, anaunga-unga magari mangapi mpaka afike shule) na matumizi yake ktk items of a personal nature.


    any ways: milioni kumi zinatosha kwa mwaka.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2010

    http://www.udsm.ac.tz/userfiles/file/hbook.pdf

    kila mwaka inabadilika

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2010

    Jamani, mbona unataka kufanyiwa kazi kubwa hivyo? yaani hata kusema aina ya shule unayotaka husemi, kwa hiyo mtu aanze kufikiria unataka nini ndio aendelee na hiyo research nyingine!

    ReplyDelete
  9. Hi all,
    I am very serious, na ningependa kusema kuwa ndio nipo Bongo, na wizarani nimefika, lakini, wao wansema fees hutegwa na shule husika. Mtu mmoja kujaribu kutafuta hizi data kwa nchi nzima nadhani itakuwa garama kubwa sana, na ni hope yangu kuwa wana forum hizi data watakuwa nazo na itasaidia kurahisisha kuziorodhesha hapa. Tukiwa na tovuti yenge information kama hizi nadhani itasaidia jamii kujiweka sawa kwenye lengo la kuwaelimisha watoto wao. Pengine, shule, colleges husika pia watapenda kujitangaza kwenye tovuti kama hiyo biashara zao.

    Private na public data zitasaidia decision making kwa wengi, ukienda shule A wakasema TSH150000 kwa term, nyingine TSH250000 utawezaje kujua hizi bei msingi wake ni upi kama hauna overall data za elimu nchini? Hii ndio nia yangu, kuwa na pahala figures kama hizi zinapatikana.

    e-mail yangu ni

    kotin.karwak@googlemail.com

    siku njema na kazi njema.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 14, 2010

    na mimi nilikua nataka just the average data kwa wanafunzi wa public education. nataka nianzishe memorial scholarship ya baba yangu hivyo nataka nijue nikiitangaza ni kwa wanafunzi wangaoi watafaidiaka au kwa mwaka huu itakua inasaidiaje towards education ya mtu au watu fulani...Ni hilo tu na mimi ndio ilikua nia yangu please plase wasomi tuition fees zenu ni ngapi ...Just in general.....

    ReplyDelete
  11. Email Update: kotinkarwak@googlemail.com

    ReplyDelete
  12. Hi Folks,
    Nimeamua kuweka uwanjani kotinkarwak na ku-register forum yangu kama ifuatavyo

    http://kotinkarwak.wordpress.com/

    Tuendelee huu mjadala hapa.

    Karibuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...