Misupu habari za kazi, pole na majukumu,
Kuna hili suala la ku-name maeneo yetu mengi ya Tanzania kidogo hua linanipa shida sana, kuna hili poli la ziada SELOUS GAME RESERVE, ndani ya hili poli kuna 50% ya tembo wote waliopo Tanzania,, kuna mbwa mwitu wengi kuliko sehemu yoyote Duniani, kiasi cha 2,000 hivi,ni poli ambalo ni urithi wa dunia, WORLD HERITAGE SITE chini ya UNESCO,na ni poli lililo katika uangalizi mkali (protected area,PA), lakini jina la SELOUS limetokana na Mwingereza aliyeitwa FRIEDRICK CORTNEY SELOUS ambaye alikua ni mwindaji mkubwa hasa wa Tembo, inasemekana aliondoka na Pembe za ndovu nyingi sana toka Afrika enzi zake, leo hii tunapigana na uwindaji haramu a.k.a ujangili na kumtukuza muwindaji haramu kwa kulipa poli letu jina lake...tusiwe watu wa kufuata tu 1st world wanachokisema, nadhani ni muda pia muafaka wa kuyatazama upya majina ya maeneo yetu muhimu hapa Tanzania na kuyafanyia kazi..
Yyapo mengi ila kwa leo hili kwanza
Mdau Remsi Sungwa
Iringa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2010

    Poli? ndio poli lalamikia hilo au vipi? watu wanakula na kufuja mamilioni ya pesa zetu wewe unalalamikia jina la pori (samahani poli).

    Mamilioni ya pesa za misaada zinaingia kizani kila mwaka na watu hali ya maisha inazidi kuwa mbaya lakini la kulalamika zaidi ni jina la poli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2010

    Mdau unakwenda mbali. Utajikuta unabadilisha majina ya mikoa yote ya bongo, ziwa victoria, ml. K'njaro, kariakoo, nk nk. Mbaya zaidi hata jina lako unaweza kulibadilisha manake linatukuza wengine

    ReplyDelete
  3. MDAU RESMI SUNGWA NIMEFURAHI KUONA KUWA UNAFUATILIA MAMBO NI WATZ WACHACHE SANA AMBAO WANAWEZA WAKAJUA HICHO ULICHO TUANDIKIA!!NIMOJA YA RASILIMALI KUBWA SANA KULIKO WENGI WANAVYODHANI MAANA KUNA MTU KAKRITISIE ILA NI UHURU WAKE, CHA MSINGI TUNACHOTAKIWA KUFAHAMU NA LABDA NDICHO KILICHOWACHANGANYA ULIPOSEMA NI PORI!HILO SIO POLI TU BALI LIMEPEWA THAMANI NA LIKAWA GAME RESERVE AMA KWA KIFARANSA TUNAITA RESERVE DE GIBIE DE SELOUS!!
    PIA NINGEPENDA KUKUJIBU SWALI LAKO ULILO ULIZA KWANINI LIMEPEWA JINA LA HUYO POCHER WA KIZUNGU NI KWA SABABU ALIKUBALI KUACHA KUWINDA NA YEYE NDIYO AKAWA MHAMASISHAJI KUACHA KUWINDA WANYAMA.
    NIMEANDAA RESEARCH INAYOELEZEA OUTCOMES ZA UTALII KIUCHUMI TANZANIA!UKISOMA UTAFAIDIKA KUJUA RAWMATERIAL TOURISTIQUE TULIZONAZO NA SOMEHISTORIE ZAKE!!PIA UTAJUA WORLD HARITAGE ZA UNESCO(PATRIMOINE MONDIALE D'UNESCO) ZILIZOPO TZ NA KWANINI WAMEAMUA KUZIPA THAMANI YA ULITHI WA DUNIA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2010

    DONDOO ZA SELOUS:
    Réserve de gibier de Selous :
    En 1982 la réserve a été nommée comme le patrimoine mondial de L’UNESCO. Avec une superficie presque 50.000kilometre carrée, Selous est la plus vaste réserve d’Afrique. Elle est plus vaste que le Danemark ou la Suisse .Elle couvre 6% de la surface terrestre de la Tanzanie et elle est trois fois plus vaste que le parc de Serengeti. La réserve se situe dans le sud de la Tanzanie à environ 250 Km de Dar-Es-Salaam. (Voir annexe n°7)
    Selous est le plus grand bassin fluvial d'Afrique de l’Est, traversé par de nombreux fleuves et affluents comme les fleuve Rufiji, Beho-Beho, Luwegu. Cette abondance d'eau et la variété des écosystèmes, les zones de savane, de bois, de prairies, de marais, de canyons rocheux (gorges de Stiegler). La réserve est très riche en espèces animales avec 200.000 Buffles, 60.000 éléphants, rhinocéros noir, les zèbres, 40.000 hippopotames, les girafes, les lions, léopards, les crocodiles et 1113 espèces d’oiseaux, avec un plus grand nombre de chiens de chasse d’Afrique.
    La rivière Rufiji serpente à travers la Miombo bois, reliée par des ruisseaux à cinq lacs attrayants, qui regorgent d’hippopotames, de crocodiles et d’autres animaux sauvages. En effet, la réserve de Selous abrite des nombreux oiseaux qui se trouvent surtout au tour de la rivière Rufiji .La réserve de Selous a passé dans une période difficile de braconnage (chasser sans permis) où les rhinocéros noirs ont été attaqués, un fait qui a causé la diminution du nombre de cette espèce d’animaux dans la réserve.
    Le gouvernement tanzanien a établi des mesures de protection de ses animaux et aussi la protection et la conservation des espèces dans cette réserve et l’écosystème.
    BY MDURBAN THE KING!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2010

    mdurban king nasikia kizunguzungu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2010

    haijalishi, hakuna matata kama huyo SELOUS ni binadamu na si shetani, kwanza hakuhama na hilo pori, sasa shida yako ni nini? hakuna tija yoyote kiuchumi kwa kubadilisha hilo jina.Tuongelee mismanagement ya hizo rasilimali, sisi tumeharibu kuliko huyo SELOUS. RIP MR SELOUS!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2010

    Kimsingi uwindaji wa wanyama pori ni halali nchini Tanzania hivyo kama ni Halali basi jina la Selous siyo shida kwani na mwenye jina shughuli zake Tanzania zilikuwa halali kisheria. Uwindaji wa wanyama umehalalishwa Tanzania na ni moja ya agenda nyeti ambayo ilipelekea mkutano wa CITES nchini Qatar hivi karibuni kutolea nje ombi la Tanzania kutaka kuuza pembe za ndovu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2010

    Kuna watu wengine bana. Mpaka kila kitu kiitwe Julius Nyerere something ndipo watapotulia.

    Sasa na sema hivi, thubutu kubadilisha jina la Selous, linalojulikana ulimwenguni kote, halafu uone utakuwa ume-achieve kitu gani.

    Watanzanian tupunguzeni siasa jamani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2010

    Anony wa Sun Jun 13, 10:35 PM. Hii lugha sisi wengine hatuiwezi. Naomba Mike Ngura atutafsirie. sababu alielezea kitu fulani kuhusu Lakers kwa lugha inayofanana na hii. Nawakilisha

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 14, 2010

    SASA JAMANI KUTUWEKEA KIFARANSA MNATAKA TUWATUKANE?? MNAJUA KABISA WADAU WA HII BLOGU WALIVYO NA MMEFANYA MAKUSUDI... MNATAKA TUWATUKANE: Hamna adabu nyote, kuanzia aliepost hicho kifaransa na ankal!!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 14, 2010

    ..There are names of various chiefs who defended our nation, who even their legend, myths and heroism made possible for the sighteeng of even the few species of flora and fauna in this reserve......i agree some may say some chiefs dissapointed us...but these peolpe we are naming after ous special places were even worse, i wonder if our ancestors would rise up and see whats going on....then wadau msipende kuponda tu kila kilicho mbele yenu, fatilieni kiundani, najua kilema tulicho nacho cha kutopenda kufatilia mambo lakini tuwe tunajitahidi angalau..

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 14, 2010

    Sasa jamani kila mtu aongelee njaa, umasikini na ufisadi? kumbukeni ni haya madogo ya zamani ambayo tunayapuuzia na kuyaona hayana msingi ndio yanayoleta makubwa ya sasa yanayoumiza vichwa..

    ReplyDelete
  13. WADAU MNISAMEHE SANA KWA KUPOSTI COMMENTI YANGU KWA KIFARANSA ILA NIMEGUSIA KIDOGO JUU KWA KIMATUMBI/KISWAHILI ILA NILICHOKIANDIKA KIMOJAWAPO NDICHO HICHO ALICHOELEZA MDAU NA NIMEWAPA DODONDOO KIDOGO KUWA HILO SIO POLI BALI NI HIFADHI YA WANYAMA KWA AJILI YA UWINDAJI YANI GEMU RESERVE KWA HIYO UNARUHUSIWA KUWINDA NA PIA MWAKA 1982 UNESCO ILIPA CLASS YA KUWA URITHI WA DUNIA NA PIA NI KUBWA KULIKO NCHI YA DENIMARK NA USWIZI, PIA NI KUBWA MARA 3 YA SERENGETI, INACHUKUA ASILIMIA 6 YA ARDHI YA NCHI YETU!!NA MAMBO MENGINE.
    PIA GEMU RESERVE INARUHUSIWA KUWINDA TOFAUTI NA MBUGA HAIRUHUSIWI, KUNA AINA YA UTALII TUNAIITA CINEGETIQUE TOURISME AU TOURISME DE CHASSE NI AINA YA UTALII YA UWINDAJI!!WADAU MTANISAMEHE SISI WENGINE KIMATUMBI CHETU CHA MBAGARA MCHANGANYIKO WA RUGHA ZOTE KIMASAI, KIYAO,KIDIGO,KIMAKONDE,KINYAMWEZI, KISPANIOLA, KIARABU, KIFARANSA N.K
    ILA BLOG YETU RUKSA MAANA KUNA WATU KILA SIKU WANATUWEKEA KIINGILISHI HUMU.Blog yetu international ILA NASAPOTI NA NINAKIFAGILIA KIMATUMBI
    MDAU WA UTALII MDURBAN THE KING

    ReplyDelete
  14. WADAU MKITAKA NIWE NAWAPA DONDOO ZA UTALII WETU NA UTAJIRI WA MALIASILI TULIZONAZO KWA KIREFU KWA LUGHA YA KIMATUMBI MUMWOMBE ANKAL ASITUBINYIE TUWE TUNAPOST ILI WATZ NAO WAJUE THAMANI YA VITU TULIVYO NAVYO NA VINACHANGIA ASILIMIA NGAPI KTK BAJETI YETU YA NCHI NA WATU WAIJUE VIZURI NCHI YAO!!
    UTALII NI INDUSTRY MUHIMU SANA KULIKO HATA MADINI TULIYONAYO INACHANGIA PATO LA NCHI YETU ZAIDI HATA MARA 8 YA PATO LINATOKANA NA MADINI KTK BAJETI YETU
    MDURBAN1/ THE KING

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 14, 2010

    Kwanza kabisa mimi sijapenda hiyo lugha ambayo imetumika ... tumia lugha ambayo watu wengi wanaelewa sawa?
    halafu watanzania muache kulalamika au kutoa hoja mabazo haziana msingi saana

    sijaona mtu hata mmoja aliyetoa hoja hap. awe ni anayelalamika klwamba mdau anataka vitu vidogovidigo kama majina vibadilishwe au wanaozungumzia mabo ya mafisadi


    tatizo la sisi watanzania tunataka kuzungumzia mabo makubwaaaaaaaaaa na akuacha kuzungumzia mabo madogo madogo kwanza//KUMBUKA MTOTO HAZALIWI TU NA KUANZA KUTEMBEA/ ni lazima apitie hatua fulani fulani////.sasa hao wanaokimbilia kusema mabo ya mafisadi...je wanadhali ufisadi ulianza tu kama ufisadi? kuna kitu au katabia kalianza kabla ya ufisadi ndio ukafika hapo ulipo...

    MBONA SIJASIKIA WATU WAKIZUNGUMZIA MABO YA KUBADILISHA KATIBA YETU?

    na ni k wanini watu /watanzania hawasimami wakadai haki zao au wakafanya sauti zao zisikike? anzia hapo ulipo.iwe ni kijijini au mjini jadili na watanzania wenzio ni jinsi gani tutabadilisha katiba yetu ...na hao majirani au ndugu zako na wenyewe watasa mabza hiyo hoja kwa watu wanaowajua ... tatizo au haya matatizo yako kwenye mfumo mzima wa siasa na katibe NA mpaka vibadilishwe au kufanyiwa kwanza n mapinduzi ya kweli ndio tutaachana na matatizo au kero ndogondogo

    TUANGALIE KWANZA CHANZO CHA TATIZO LOLOTE KABLA HATUJAANZA MJADALA.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 14, 2010

    Mdurbun...the King,
    Ni kweli kabisa Utalii wachangia kwa asilimia kubwa sana katika bajeti na pato la taifa, tuna vingi mno vya kujivunia katika utalii, ila kaka Selous Game Reserve ni pori la ziada, pia kuna utalii wa uwindaji(hunting tourism), na utalii wa picha(photographic tourism), south and north of the selous respectively, selous ni protected area (PA) ya kwanza kabisa duniani, ni kubwa kuliko zote Afrika, kuna fauna and flora wengi na adimu kuliko sehemu nyingine Afrika, na mto RUFIJI umepita katikati ya pori, pamoja na kusifika kwa mazuri, pia inasifika duniani kwa ujangili uliokisiri, pia kuna vyanzo vingi ambavyo vingetumiwa vizuri vingeweza sababisha upatikanaji wa umeme wa msongo mkubwa sana, mfano STIEGRERS GORGE n.k...kwa mwaka pori hili peke yake huchangia mabilioni ya shilingi..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...