Wadau, nafurahi kuwatangazia kuwa mwanangu Camara Kadete amefunga ndoa na Shalanda Wills, huko Maryland. Walikutana wakiwa wanasoma Chuo Kikuu. Sherehe iliandaliwa na familia ya bibi Arusi kwa mila za KiMarekani. Nilicheka Mchungaji aliposema jina la mwanangu ni ngumu kutamka. Tongue Twister.

Tunaandaa sherehe hapa Boston baadaye mwaka huu. Sherehe hiyo itakuwa na mambo ya kimila na kiAfrika zaidi. Wenye ideas wanitumie chemiche3@yahoo.com

ZAENI MATUNDA MEMA WANANGU!
Da'Chemi Chemponda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2010

    So beautiful lady!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2010

    ati nini huyo padri kasema wakati wao wana majina yetu kabisa nimeonana na dada mmoja anaitwa "MAISHA" ila eti wanamwita "MAYIISHA" hawa wamarekani wanashangaza na kuchekesha mno mi wakati nilivyokuja nilidhani mi ndo mshamba kumbe wao ndio kabisaaaa eti ananiuliza africa unaweza kwenda na basi hahahahahah

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2010

    mi nilikuwepo hapo kaka yetu kapata ila tafadhali kuanzia leo mabibi wa nje marufuku.... si mbongo, si mmarekani mfano ona kwa kina kamichu katulia na kwake, marafiki ni marufuku tena angalia chagua wale waliokuwa na wake sio masingo watakuharibia nyumba. siajabu hapo wanasema oooh kaoa sababu ya karatasi mara nini ilimradi tu wakutilie nuksi. kazi kwako bwamdogo.

    NB: Hashim hamjamwalika au?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2010

    Suti ya Bwana Harusi tu! GPA (ya Mlimani - Faculty of Law) 4.8.

    Hongereni, mmependeza. Maisha Mema ya Ndoa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2010

    Ni Kadete (marehemu Prof)? Jamani mmenitonesha roho - alinifundisha UDSM (Electrical Engg).

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2010

    sio Electrical Engg ni elektroniki engg!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2010

    Nawatakia Maharusi maisha mema ila nawapa Watanzania woote tadhari na huu utaratibu wa ndoa za Makaratasi.
    Zinameremeta siku au miaka ya mwanzo na baadaye tunajua ni kitu gani hutokea unapokorofishana na wamarekani. Marekani kuoa na kuacha ni kama kupanda dala dala hapa Ubungo na kushuka hapo Migomigo. So kuoa na kuachana siyo deal.

    Halafu wanasema Mila na desturi za Kimarekani...What?? Hakuna mila wala desturi za Kimarekani? Marekani haina mwenyewe bwana kila mtu ni wa kuja hapa acheni utani wa kutudanganya....watch out on America and God bless you

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2010

    mimi mnanihudhi sana watu mnaozungumzia makaratasi kila mkiona harusi za watu wa asili tofauti ni makaratasi. imekuwa mbaya kwamba hata wenyewe kwa wenyewe mkioana, mnauliza nani kampa mwenzake karatasi.
    SWALI: nyie watanzania kwa watanzania hususani mliopo tanzania hamuachani? wamarekani/waingereza/wazungu wenyewe kwa wenyewe hawaachani?kama hamuachani mbona kiswahili kina neno talaka?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2010

    Hongera Dada Chemi ..Wewe nakuaga nakulinganisha kama majika ya dada yangu vile. Haa jamani mwanao ameoa kesho utakua grand ma..siamini nisikie na mimi leo nephew au niece wangu wameoa/kuolewa..nikiwaangalia naona kama vile wamelingana na watoto wa dada yangu tu hawa...bado wadogo sana masikini ...Hongera zao tunawatakia maisha yenye baraka na furaha pia...

    ReplyDelete
  10. Mdau wa 10:57, ndiyo baba yake mzazi ni marehemu Prof. Henry Kadete ambaye alikuwa Head of Electrical Engineering pale UDSM.

    Asanteni wote, na bado nakaribisha ideas zenu kwa ajili ya sherehe hapa Boston. Marehemu alikuwa Mnyamwezi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...