TIMU YA GLOBU YA JAMII IMEPIGA MBIZI NA KUIBUKA NA LIBENEKE LA KUPIGIA KURA MAAJABU MAPYA YA DUNIA AMBAPO MLIMA WETU KILIMANJARO UMO ILA ILI KUPENYA KWENYE TUNDU HILO LA SINDANO INABIDI TUPIGE KURA KUUWEZESHA UORODHESHWE KWENYE MAAJABU SABA MAPYA YA DUNIA. SHIME SHIME WADAU NA TUPIGE KURA. UKIBOFYA HAKO KADUDE KA KIJANI JUU YA PICHA YA MLIMA UTAPELEKWA KWENYE UKURASA WA KURA. TAFUTA KILIMANJARO KISHA BOFYAAAAA!BOFYA HAPA KISHA FUATA MAELEKEZO HALAFU PIGA KURA YAKO !


MBONA TUNABOFYA TUNAKUMBANA NA KILUGHA AMBACHO HATUKIELEWI MICHUZI
ReplyDeleteNi kihispania nadhani. kwenye page kulia juu wameandika "ESPANOL", kuna kama mshale hapo wa kuchagua lugha click huo mshale halafu chagua english endeleza libeneke.
ReplyDeleteHAYA NDO MAMBO, UKITAKA KUSUBIRIA WIZARA HUSIKA UTASHTUKIA TU KUAMBIWA HAKUNA BAJETI, HAHAHAHA!
ReplyDeletemjomba jitaidi sana ututafutie ufafanuzi zaidi coz hatuelewi ukibofya unaombwa namba ya kujilegista sasa tutaipataje kwa kweli tunaomba elim zaidi tafadhali sana
ReplyDeleteWizara ya Maliasili wanafanya kazi gani? Mbona hao ndio wangetuletea hiyo habari pamoja na maelezo ya kutosha?
ReplyDeletekwa nini tunakimbilia kupiga kura bila ya kuhoji ukweli na uhalali wa hali halisi na matokeo?
ReplyDeleteHivi kweli kama kilimanjaro ni natural wonder, kuna haja ya leo kuanza kushindana na kupigiana kura dhidi ya vitu vingine ambavyo vinajulikana na kueleweka?
Tusiingie kichwakichwa ndugu zangu. Ninachojua mimi UNESCO ndio yenye mamlaka (KIMATAIFA) ya kutanabaisha na kutoa hadhi husika. I'm sure wizara imekaa kimya kwa kutambua hili. Tusikurupuke na kuushindanisha mlima wetu wenye hadhi na heshima kubwa ktk mashindano ambayo hatuyajui.
Ni Mtizamo wangu, kuukubali au kuupinga ni ruksa
Naungana na mdau wa Thu June 24,08:22:00AM.
ReplyDeleteWe anonymous wa Thu Jun 24, 08:22:00AM, Napingana na wewe, Watanzania mbona link ipo na magazeti yameandika ama kweli hii ni MBOGOLALA usitufundishe nidhamu ya woga wee endelea kulala sisi tunapiga kura. Mnabaki kulalamika Kenya wanatangaza kilimanjaro iko Kenya imetokea hiyo sasa mjitangaze tena hamtaki. Work-up man, we Tanzanian we have to be aggressive like Nigerian.
ReplyDeleteKila kitu tuko nyuma kazi kupiga domo, siasa tuuuuu kila mahali.
www.new7wonders.com/community/en
Ni mtazamo wangu, hii kitu haimake sense wala nini, maaana tu ya kawaida ya neno "wonders" kiswahili ni "maajabu" sasa Mlima wetu wenye hadhi kubwa ya urefu wake una maajabu gani? ni mlim atu kama ilivyo milima mingine, hakuna maajabu pale ya kuufanya upigiwe kura, acheni ubaki na heshima yake ya kuwa mrefu afrika, kwisha, mambo ya maajabu Ngorongoro Crater inatosha. Ankal upo?
ReplyDeletewewe mdau wa 10.32 am unaishi dunia gani? hiyo ni sifa kubwa sana kama mt kilimanjaro itashika number 1. jaribu kuuliza kwanza wanaamanisha nini na neno hilo
ReplyDeletekuna neono wazungu husema nani amesema hamna snow africa? je umefika kilimanjaro? hayo ni maajabu kwao juu wanaamini sisi jua ni jan hadi dec.
ReplyDelete