Rais wa RBP OIL & Industrial Technology Tanzania Limited,Rahma Al Kharoos akiongea na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam,kulia ni Meneja Huduma wa kampuni hiyo Ibrahim Khatrush


Rais wa kapuni ya mafuta ya RBP Oil & Industrial Technology Tanzania Limited,Rahma Al Kharoos ametangaza ziara ya timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars kwenda nchini Marekani kwa mafunzo mbalimbali wiki ya kwanza ya mwezi Agosti.

Akizungumza kwenye mkutano na wandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam,Rais huyo amesema anaamini kuwa ziara hiyo itakuwa ni chachu ya mafanikio ya timu hiyo wakati itakapokwenda kucheza katika fainali za kombe la mataifa ya afrika kwa wanawake mwezi septemba nchini Afrika Kusini.

Amesema akiwa kama mlezi na mdhamini wa Twiga Stars na kwa kushirikiana na wenyeji wa ziara hiyo huko Marekani ambao ni taasisi ya FREEDOM WASHINGTON wamejipanga kuhakikisha ziara hiyo inakuwa ni ya mafanikio makubwa hasa ukizingatia kwamba timu ya Twiga Stars imeweka historia kwa nchi yetu ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo makubwa ya mpira wa miguu kwa wanawake.

Ameongeza kuwa Twiga Stars ikiwa nchini Marekani itacheza michezo minne na timu za nchi hiyo wa kwanza utakuwa ni wa kuchangia timu hiyo ambapo watu mbalimbali watachangia timu yetu ili iweze kujiandaa vyema na mashindano hayo.

Twiga Stars ilifanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake itakayofanyika nchini Afrika kusini mwezi septemba mwaka huu baada ya kutoka sale ya magoli 3-3 na timu ya Eritrea.

Mama Rahma alisema anaomba wadau, wapenzi wa soka la wanawake kuiunga mkono timu hiyo ya Twiga Stars ambayo imeiletea sifa na heshima ya kubwa taifa letu la TANZANIA kwa kupata nafasi hiyo ya kushiriki michuano mikubwa zaidi barani Afrika kwa wanawake. anasema kwamba anaamini kuwa sasa milango ya wachezaji wanawake kucheza soka la kulipwa nje itatimia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2010

    MH.MKUU WA NANIHII,TUNAOMBA UTUTAFUTIE RATIBA YA MICHEZO TIMU YETU ITAKAPOKUWA HAPA ILI TUJITOKEZE KWENDA KUISHANGILIA/KUCHANGIA.ASANTE SANA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2010

    Sasa unataka tufanye nini? tuwachangie?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2010

    Safi sana. Michezo inahitaji sponsors na si kiingilio peke yake.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2010

    Umeamua kuwa wewe sponsor mkuu unataka nani tena achangie?Bongo Tambarare ukitaka kujulikan wewe ni mtu wa ........ shurti uwe sponsor japo kiduchuuuuuuuuuuuu!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2010

    Tunatumai 'Twigar Stars' watafanya vizuri kwenye hayo mashindano.

    Wasije tu wakaligoroga, watalinywa huku wanalia, kama nanihii, ambaye yuko kule nanihii.

    Maana kama kugharamiwa, wamegharamiwa, sidhani kama kuna walichokosa.

    ReplyDelete
  6. Hongera sana kwa jitihada zako za kusaidia jamii.

    Tunakuombea kwa MOLA akuzidishie.

    Jumuiya ya Maendeleo Ya Waislamu Kigamboni.

    ReplyDelete
  7. Bw. Michuzi

    Sina Maoni ila sisi Viongozi wa Taasisi ya Kigamboni Musilm Development Initiative, tunaomba fursa (appointment) ya kukutana na Mama Rahma Al-Kharoos.

    Tungependa kuonana nae na kujadiliana mambo mawili matatu. Kwa tunaomba utupatie contacts zake au utufikishie ujumbe huu, kwa kuwa sis tumeshindwa kupata contacts zake.

    Kwa mawasiliano tumia namba hizi 0754 680 670 au 0658 680 670 au Email: korongo.a@gmail.com

    Tunategemea msaada wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...