
Warembo 18 watakaoshirki kinyanganyiro cha kumtafuta Redds Miss Ilala (pichani juu) wataondoka kesho asubuhi kuelekea Tanga kwa ziara ya siku mbili ya kimafunzo ambapo watahudhuria pia shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga.
Wakiwa katika jiji la Tanga watatembelea vivutio vya utalii vya mji huo ikiwa ni kwenda katika mapango ya Amboni, kutembelea fukwe na sehemu nyingine za jiji hilo.Warembo hao wataongozana na Mwalimu wao Leila Bhanji, Matron Leila Bhanji na Viongozi wa kamati ya Miss Ilala.
Warembo wa Ilala pia watahudhuria sherehe za ufunguzi wa mashindano ya magari yatakayofanyika Jumapili katika jiji hilo.
Huu ni mwaka wa tatu mfululizo, warembo wa Ilala wakifanya safari kama hizi za Kitalii na mafunzo. Mwaka jana, Kampuni ya Dar Metropolitan Promotions inayoandaa mashindano ya kumtafuta mrembo wa Ilala iliwapeleka warembo katika mbuga za wanyama za Manyara na Tarangile zilizoko Mkoani Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...