HAYATI JAHIYA BAKARI MWERI

Familia ya Bakari Mweri Tajiri ya Mwananyamala, Dar es salaam, Inatoa shukrani za dhati kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wote kwa kushirikiana nasi katika kipindi kigumu cha msiba uliotokea tarehe 12.05.2010 ghafla Mwananyamala wa Mpendwa wetu Jahiya Bakari Mweri.


Kwa kuwa sio rahisi kumshukuru kila mmoja peke yake, tunaomba mzipokee shukrani zetu kwa namna ya pekee na Mwenyezi Mungu awajaalie kila la kheri kwa upendo wenu.

Tunapenda kuwakaribisha kwenye Kisomo (Arobaini) inayotarajiwa kufanyika tarehe 19.06.2010 nyumbani kwa Mzee Bakari Mweri Mwananyamala kuanzia saa 6:00 Mchana.

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati
Wana Familia ya Mweri

Mawasiliano:
(i) Madaraka Mweri (0655300892)
(ii) Mwanahamisi Mweri (0754285332)
(iii) Habibu Mweri (0713222671)
(iv) Saumu Mweri (0712337494)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2010

    Jahiya tulimpenda sana ila Mungu pia alimpenda ,let her soul RIP

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wafiwa na Mwenyezi Mungu azidi kuwatia nguvu kwani nasi huko ndiko tunako elekea.R.I.P

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2010

    Pole sana rafiki yangu Habibu Mweri,mwenyezi mungu awape nguvu wakati huu.

    Mikah Kinondoni

    ReplyDelete
  4. Zaina BuuzoheraJune 20, 2010

    Inalilah wa ina ilah rajiun!Poleni sana wafiwa,tulimpenda sana Jahiya lakini Allah alimpenda zaidi,tumuombee dada yetu kipenzi Jahiya katika safari yake yenye neema na isiyokuwa na adha yoyote,Alhamdulilah.Tunawapa pole sana sisi ukoo wa buzohera.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...