Viongozi na wakaazi wa wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Loliondo kuelimisha jamii juu ya sera ya kilimo kwanza.
Mkutano ukiendelea na wananchi wanaonesha usikivu na uelewa mkubwa kiasi haikuwa ajabu kuwaona wameanza kutekeleza sera hiyo kwa vitendo.
Vijana wa Ngorongoro wakitekeleza kwa vitendo sera ya Kilimo kwanza
Kilimo kwanza Lolindo. Picha zote na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2010

    kilimo kwanza kwa jembe la mkono?
    Trecta moja lingi save nguvu za watu wangapi?
    Na pesa tulizowapa Brazil wakafanye shopping Zingenunua Matrekta Mangapi?,Irrigations Sytems,Manure,Researches,Plans ,ect?????????????????
    Tupo karne ya 21 jamani,wake Up Tanzanians!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2010

    aha..! jamani hiki ndo kilimo kwanza?
    mbona yale yale ya majembe ya mkono? unategemea mageuzi kweli ama hii habari imekosewa?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2010

    HII NI KILIMO MWISHO SIO KWANZA AU TUSEME KILIMO KUFA.
    HILI JEMBE NI LA KABLA YA YESU HILO!!
    MZAWA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2010

    Kulima kwa jembe siyo sera nzuri. Jirani yangu hapa ugenini ni mkulima wa part time ingawa ni mfamasia wa full time. Shamba lake ni jumla ya eka 150 na anazilima zote peke yake akisaidiana na mke wake tu. Mtu huyu hana trekta wala mashine nyingezo za shamba, ila anafaidika kutokana na biashara ya kukodi mashine hizo iliyoshamiri hapa. Ukiwa na shamba unakwenda kukodi na kuzitumia labda kwa siku moja au mbili kulingana na mahitaji yako.

    Serikali ianziehs utaratibu wa aina hiyo badala ya hiki kilimo cha watu zaidi ya kumi kujazana kwenye kamraba ka mita kumi kwa kumi halafu tunadaia Kilimo kwanza.

    Vile vile hii sera ya Kilimo Kwanza kama ilivyo siyo ngeni hapa nchini; mimi naiona kama vile ni ile iliyoletwa na Azimio la Iringa la Siasa ni Kilimo mwaka 1973. Kama kwa takriban miaka 30 ilishindwa kufanya kazi sijui kama itafanya kazi kama haikufanyiwa mabadiliko ya nguvu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2010

    Tuachane na dhana potofu kwamba Kilimo kwanza ni jembe la mkono na kulima mahindi ya ugali majumbani kwenu....ni zaidi ya hapo!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 14, 2010

    Kaka Michuzi huyu mtu aliyetuma hizi picha za kilimo kwanza naomba atufafanulie ni za siku moja au...Its confusing in sec watu wako kwa kikao mara wako shamba...hii kilimo kwanza inanitia mashaka....sijui lkn...naomba aniweke sawa hapo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2010

    Hivi kweli hii jamii ni ya wakulima au wanalazimishwa tu kulimwa au mifugo imekuwa haina tija tena?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2010

    Huu ni uzushi na utapeli wa kisiasa. Kilimo cha wawekezaji wa kuiba ardhi yetu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2010

    Yaani sera ya kilimo kwanza ndio inatekelezwa kwa jembe la mkono? mh. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 14, 2010

    du kweli wabongo tunacheza makidamakida!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 14, 2010

    Kweli njaa haina adabu,nyie wenyewe mmeanza shika jembe,sasa sijui tuwaitaje?!wafugaji wakulima ama?

    ReplyDelete
  12. Kaka TrioJune 14, 2010

    Hicho kilimo kwanza cha Karne ya 18 hakitatufikisha mahala popote. Na kimo ndio hicho Mheshimiwa Kikwete anapigia debe basi ni uuzaji wa maneno tu hamna lolote hapo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 15, 2010

    Jamani mimi naona wanasiasa wameamua kufanya maigizo ilikupata nafasi ya kuwadanganya waha ndugu zetu wawape kura. Kilimo kwanza kitaletwa na mageuzi ya zana zinazotumika, hiyo machine aliyosema kaka hapo juu, si serikali iwezeshe SIDO izitengeneze kwa wingi?? Huku Thailand wenzetu wamebuni utundu lile jembe lilikuwa linakokotwa na ng'ombe wameli- modify kule mbele wameweka km morter inavuta huku mkulima anendelea kulima na linalima eneo kubwa kwa muda mfupi. Tuache kutuma kwenye magazeti maigizo, hebu tuweke taarifa ambazo zikisomwa zitaweza kuleta mapinduzi ya kifikra na hatimaye kuleta maisha bora kwa wakulima. Ushuri kwa SIDO jamani si mubuni nyenzo rahisi zitakazoweza kusaidia hii sera ya kilimo kwanza?? Waziri wa kilimo wape hao watu fursa ya kutoka nje waone wenzao hasa wa huku Asia wanafanyaje mambo??

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2010

    enzi za mwalimu Tulikuwa na Maazimio mawili Azimio la Arusha na Azimio la Iringa lilokuwa na msemo wa kilimo ni uti wa mgongo lakini wakati huo tulikuwa na sera ya umoja ni nguvu utengano ni udhaifu kwahiyo vijiji vyote vya ujamaa vilifanya kazi kwa umoja huku serikali ikiwajali kwa kuwapa vitendea kazi.Marehemu Edward Moringe sokoine alikuwa na muhamasishaji mzuri sana wa kilimo na ndio maana alivyo fariki wa tz tulilia sana sana nakumbuka hata babu yangu alivyokuwa mwekiti wa kijiji wakati huo alisema serikali ilikuwa ikiwajali sana hata ikaamua kuwapa vitendea kazi kama vile trekta hilo trekta mpaka leo lipo na halijafa linaharibika linatengenezwa walipewaga msaada na watu wa sweden je leo hii ningetegemea serikali badala ya kununua maprado wangeagiza kwanza matrekta ilikutekeleza sera ya kilimo kwanza maana kale kawimbo ketu katamu kalikotupeleka hekaluni pale pembezoni mwa feli kula upepo wa pwani wa maisha bora kwa kila mtz na ari mpya,nguvu mpya kasi mpya si ka sikii tena nilijua siasa sitaki tena kusikia hata haka ka wimbo ka kilimo kwanza mapinduzi ya kijani ni mbwembwe tu za kuturudisha tena madarakani halafu kimyaaaa. Mjomba wape salamu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...