Na Woinde Shizza,Arusha
WAKATI mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yakiendelea Afrika Kusini, Kombe la Afrika Mashariki (EAC Cup) limeandaa tamasha la michezo la vijana ili ‘kuwawezesha kupitia michezo.’
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na EAC Cup, tamasha hilo linatarajiwa kuanza Juni 22 hadi 27, mwaka huu.
Tamasha hilo litakalowajumuisha vijana wapatao 1300 kutoka Zambia, Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda, litafanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Ilisema katika hali halisi tamasha hilo ni zaidi ya soka kwa kuwa hakuna hata mmoja atakayepiga mpira hadi atakapohudhuria na kupewa mafunzo katika stadi za maisha, uongozi, tamaduni na urefa.
“Hii pia inajumuisha mada kuhusiana na masuala ya Ukimwi na kuwapatia uelewa kuhusu Virusi vya Ukimwi, huduma ya kwanza na namna ya kutatua migogoro.
“Ingawa ubora wa soka ni wa hali ya juu…timu zinazofanya vizuri katika tamasha la EAC Cup zinapelekwa kushiriki matamasha makubwa ya michezo katika nchi za Skandinavia, kama ya Dana Cup na Norway Cup,” ilisema taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, George Kamau, amewahimiza wasichana wengi kujitokeza kushiriki kwenye tamasha hilo.
Alisema hadi kwa sasa ushiriki wa wasichana ni katika uwiano wa 55 kwa 45 lakini lengo ni kufikia katika usawa wa 50/50.
Hata hivyo, Kamau alisema wasichana wameanza kujitokeza na kushiriki kwa wingi hali ambayo inazidi kukua mwaka hadi mwaka.
Tamasha hilo litahusisha michezo katika makundi manne, ambayo ni wasichana na wavulana wenye umri chini ya miaka 16, na wenye umri wa miaka chini ya 13.
Taarifa hiyo ilisema moja la lengo la EAC ni kuendeleza maendeleo ya ushiriki wa wasichana katika jumuiya zao ambapo pia mkazo utawekwa kwa kushiriki semina na mazoezi ya viungo katika kuboresha ushiriki wa wasichana.
Washirika katika tamasha hilo ni Norwegian People’s Aid (NPA), Kristen Idretts Kontakt (KRIK), Mathare Youth Sports Association (MYSA) na Christian Sports Contact (CHRISC).
Wengine ni BBC, Right to Play, Norway Cup, Norges Idrettsforbund, Fredskorpset, Statoil, Ultimate Security Tanzania, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraza la Michezo la Taifa (TNSC) na Norad.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...