Naibu Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa Bi. Generose Bateyunga akitoa mada wakati wa semina elekezi kwa mawakala wa bidhaa (clearing and forwarding agents) ukumbi wa Karimjee jijini Dar. Mambo mengi yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma ya upakuaji bidhaa bandarini na viwanja vya ndege na mapendekezo kadhaa yametolewa kupunguza kama si kuondoa kabisa kero ya urasimu na shida zingine kama vile gharama za ushuru zisizo linganifu n.k. ambapo TRA imeahidi kuyafanyia kazi
baadhi ya mawakala wakisikiliza kwa makini
ukumbi ulifurika mawakala ambapo wengi walichangia hoja mbalimbali
mawakali seminani
umakini ulikuwa wa hali ya juu
Meneja Msaidizi kitengo cha Inland Container
Depots Bw. Robert Manyama akitoa mada
sdemina ikiendelea
mawakala wakisiliza
baadhi ya mawakala wakifuatilia kinachojadiliwa









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. ta paidia ta teknaJune 09, 2010

    kila kitu UWAKALA mpaka imnatia uzembe kazini.

    Hivi watumishi wa TRA wameajiriwa tena kwa mishahara mizuri ili wafanye nini?

    Kutoa vyeti vya uzazi na vifo navyo UWAKALA! Jamani kazi yetu watumishi wa umma ni nini ? Nauliza, huu si uungwana.
    Kwa nini tusiwaajili hao mawakala na tupunguze wale waliostahili kufanya kazi hiyo?

    Tukiendekeza uzembe huu tutaweka MAWAKALA mpaka kwenye ndoa zetu halafu tusije mlilia mtu baadaye eti tunapime DNA za watoto.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2010

    IDARA YA FORODHA NDIYO KIKWAZO KIKUBWA KATIKA UONDOSHAJI WA SHEHENA KWENYE VITUO VYOTE VYA FORODHA NCHINI TANZANIA.KASI NA UWEZO WA MAAMUZI WA MAOFISA WAKE NI KIGUGUMIZI KITUPU.BANDARI IANAPAKUA MAKONTENA SAA 24KWA SIKU 7 NA WAO WANAONDOA FAILI NGAPI KWA SIKU.JE KUNA SABABU YA KUWAZUIA KUFUNGUA VITUO VYAO KWA MTINDO HUO?JE KWANINI MAGARI YANASHUSHWA MELINI DATA ZAKE ZISIINGIZWE MOJA KWA MOJA KWENYE DATABASE YAO ILI KUEPUKANA MTINDO WA KIZAMANI WA KWENDA KUTEMBEZANA KWENYE VUMBI ILI KUKAGUA MAGARI CHINI YA MALALAMIKO YA MAOFISA WENYE KIBURI[MIUNGUWATU]WANAODAI KUWA WAPO WACHACHE NA KAZI NYINGI?JE KUJAA KWA BANDARI SIYO NEEMA KWA PATO LA SERIKALI?MAOFISA HAO WENYE MAHEKALU NA MAGARI YA KIFAHARI WANGEYAPATA WAPI HAYO BILA KUJINYIMA KWA WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI WA NCHI HII?SEMINA ZA TRA HAZINA TIJA KWA UMMA BALI MATENDO YAO MEMA NDIYO MTAJI WA TAIFA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2010

    Hivi kuna mawakala wangapi nchini tanzania? wangapi kati ya hao ni wa kuaminika na wanatambulika kimataifa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2010

    Michuzi mbona unatusanifu kaka?Body language za Wadau zinaonyesha jamaa wanaboeka halafu wewe unasema wako fulu swingi(full swing)??Body language zao ziko closed jamaa wanawaboa tu na malekcha yao mpaka wengine wamelala!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2010

    hii inaosha kabisa hao wawakala wenyewe hawafurahi kazi yao, concentration zero. pili ukumbi kama ule unawaweka watu seminar hata sehemu ya kuandikia tu hawana. how can they be in the mood kukusikiliza. na mbaya ziadi umetumia pesa ili watu wakusikilize kupa ukumbi kama huo utadhani watu wako kwenye foleni ya kupata ticket za kuangalia movie, do the best and do not do things as a custom always.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...