Kaimu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Edwin Mng`ong`o (kati) akifungua rasmi warsha ya siku moja jijini Dar es salaam kuhusu utafiti wa hali ya biashara haramu ya watu Tanzania.(kulia) Mkuu wa Kitengo cha Habari Elimu na Mawasiliano wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi (NACP) Dr. Bennett Fimbo.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja kuhusu Hali ya Biashara Haramu ya Watu Tanzania jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi jamii Dr, Edwin Mng`ong`o (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi huo.
Mtaalamu wa Utafiti kutoka chuo cha sayansi na Tiba kutoka Muhimbili Dar es Salaam (MUHAS) Dr. Switbert Kamazima (mbele kulia) akitoa Ripoti ya utafiti aliyoifanza kuhusu hali ya biashara haramu ya watu Tanzania katika warsha ya siku moja iliyofanyika jana jijini Dar. Ripoti hiyo imetolewa kwa wafanyakazi wa Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii chini ya mpango wa Taifa wa kudhibiti ukimwi. (NACP) ambapo imezitaja baadhi ya sehemu kuu za biashara hizo ambazo hutoa na kupokea ni Mikoa ya Iringa,Singida,Mbeya, Dodoma,Tanga,Shinyanga na Manyara.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya Afya Dr. Geoffrey Kiangi (katikati) akibadilishana mawazo na watafiti kutoka chuo cha Sayansi ya Tiba kutoka Muhimbili (MUCOS) jana katika warsha ya siku moja ambapo iliwasilishwa RIPOTI ya utafiti wa baadhi ya mikoa iliyochaguliwa kufanyiwa utafiti kuhusu hali ya Biashara haramu ya watu Tanzania. (kulia) ni Mtafiti Dr,Switbert Kamazima na Mwengine ni Mtafiti Dr. Medhod Kasanga.
(Picha na Mwanakombo Jumaa wa Globu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2010

    hivi serikali yetu ina pesa sana, kuna mawaziri,manaibu waziri, katibu wakuu,manaibu katibu wakuu, katibu wenezi,muktasi, manaibu bla,bla,bla

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2010

    Biahara haramu ya watu ndio biashara gani hiyo body harvest au ni biashara ya kuuza watu wazima wazima? mimi sijaelewa naomba munieleweshe...

    nakumbuka tukiwa wafogo tulikua tunaambiwa kuna watu wananyonya damu halafu ikaja kuna watu wanachuna watu ngozi....hebu tuambieni hii ni biashara ya nini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2010

    Anony wa kwanza hapo juu, ni ukweli usiofichika kwamba hii ndiyo cream inayogawana robo tatu ya keki ya taifa. Rais na Baraza la Mawaziri, makatibu wakuu, wakamishna, wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya na wabunge. Hawa ndio wenye haki ya kuhudumiwa na serikali tangu chakula, entertainment ya wageni, magari bure, nyumba bure and whatever. Tuliobaki tunagombania robo ya keki inayobaki. Hawa NACP ili watafune fedha kabla ya 30/06/2010 sasa wanafanya kongamano la biashara ya watu na ukihoji watakupa data.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2010

    Ukiritimba wa kufungua account kwa kianzio, mfn $50 umepitwa na wakati, ndio maana watz awapendi kufungua a/c kwenye mabenki za TZ.

    CRDB fungueni macho acheni ukiritimba, biashara ni ushindani sio tamaa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2010

    Is this man in a blue shirt operating the computer Joel Ndayongeje? I presume.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 27, 2010

    Aliyeleta mada hii pamoja na taswira ajitahidi kuwa mwana habari aliyekamilika kwa kutoacha watu wameachama vinywa wazi bila majibu ya kueleweka.

    Jaribu kutoa ufafanuzi juu ya biashara haramu ya watu, kwani kwangu sijapata jibu ni biashara haramu gani ya watu wanayoifanyia kongamano badala ya kutathmini watu wanavyokufa kwa ajali kila kukicha.

    Hiyo ni mbinu tu ya kumaliza pesa za bajeti ya mwaka uliopita ndo maana wanabuni njia ya kujaza mifukoni pesa hizo kabla bajeti mpya hazijaingia.

    ReplyDelete
  7. Biashara haramu ya watu "Human trafficking/trafficking in persons" ni shughuli ya kiharamia, kilaghai, kinyonyaji, kinyanyasaji na kitumwa inayohusu uchukuaji wa wanyonge wasiokuwa na fursa ya kazi, elimu wala vtega uchumi vyenye tija kutoka maeneo yenye umasikini, ufinyu wa fursa au migogoro ya kisiasa kwa njia ya mabavu, ulaghai, utekaji na kuwapeleka maeneo mengine kwa ajiri ya kuwatumikisha kwa kazi za lazima, biashara ya ngono, utumikishwaji wa nyumbani nk. kwa Tanzania wahanga wengi (takribani 300,000) ni watoto wanao safirishwa kutoka mikoani kuja DSM kwa ahadi ya kusomeshwa au kupatiwa kazi yenye tija badala yake wanatumikishwa majumbani, kwenye madanguro au kupelekwa zanzibar, uarabuni na china kutumikishwa. wahanga wanateseka wala hawana sauti ya kujitetea wala hawajui watarudi vipi nyumbani. Wakikosa namna wanakubli hali zao na kuendelea kunyonywa nguvu kazi, kunyonywa kingono nk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...