Ankal,
Moja ya vioja vya neshno stediam jana. Luninga ilikuwa inaonyesha haya wakati wa mechi. Sijui, kuna mtu alikuwa anatuonyesha mafaili ya ofisi kwanini?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2010

    Duh Kazi kweli bado ipo!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2010

    Hii kiboko.. Made in Tanzania.

    Nimecheka hadi basi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2010

    What a game, an eye opener to taifa team.
    What disappointed me was to see so many empty seats around the stadium.May be a lot of people could not afford it,but tell me why the organizers did not feel generous enough and give free tickets to school children, it would have been a lifetime treat for them
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2010

    hiyo mechi ilijaa vioja kuanzia mkuu wa nchi kuchelewa kuwasili uwanjani, watoto wote kuvishwa jezi size moja, camera 2 uwanjani na moja ikiwa na matatizo ya rangi,taa za jukwaani kuzima, askari sijui walikuwa wapi mpk mtu anaingia uwanjani mpk anatoka hakuna ndio askari wanakurupuka

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2010

    Hey, mbona makubwa sasa ndiyo nini hicho?Huku mnasema mnataka muwepo kwa lulinga kuonyesha mnavyojua kulisakata dimba.
    Hahaha aibu tupu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2010

    inaonesha jamaa walikuwa wanatumia projector kuweka matanngazo yao kwenye big screen.matangazo yalikuwa yanatako kwenye laptop loool.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2010

    Na mna bahati hakubofya mafaili yake ya picha na video za ngono...ingekuwa kali ya mwaka kutokea...Hiyo cha mtoto, ikaja ya nyimbo za Taifa...yaani nyimbo ya Taifa ya Brazil inapigwa huku vijigoma vinalialia kwenye nyimbo yao mpaka wakawa hawaelewi kinachoendelea, nahisi walikuwa wanajiuliza hii nyimbo yetu ya Taifa ina remix huku Tanzania au? baada ya hapo nyimbo yetu ya taifa nayo ikawa imekwama kwenye "IBARIKIII TANZA TANZA TANZA TANZA TANZA", Hakyanani sijui DJ alikuwa anafanya manjonjo au sijui ndio CD ilikwama, yaani nilifedheheka...TFF hawakujiandaa kabisa, wangeangalia mfano kwa wenzetu wa Zimbabwe...toba, na mbaya zaidi eti wakaleta mipira katika box wakawa wanawachoresha wachezaji wetu kipindi cha half time eti kila mchezaji wa bongo aende kwa wa Brazil akachukue autograph na wala si kwa hiari yake, ili tu mipira ile ikauzwe kwa bei mbaya madukani kisa ina sign ya mdau Kaka, Lucio au Robinho...Mungu ibariki hii nchi yangu...Amen.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 08, 2010

    Wimbo wa Taifa wa Brazil ulisindikizwa na ngoma kwenye Big Screen, hahahahaaa, Wimbo wa Taifa wa Tanzania CD inakwama kila siku hivi inauzwa shilingi ngapi tuwachangie jamani semeni tu hahahaha TFF yaani TumeFeliFeli

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 08, 2010

    we have a long way to go....

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2010

    Jana tulimpa Dunga kitu muhimu sana. Japo tulifungwa lakini tulimpa somo Dunga kwamba Brazil wapo dhaifu kwenye counter attacks, zaidi ya mara 4 tulikaribia kuwafunga kwa counter attack kama si kukosa umakini pale. Kitu kingine nachoishangaa timu yangu ya Taifa ni kutojifunza namna ya kubadilisha uwanja. Tangu nilivyoiona kwenye mechi dhidi ya Msumbiji hadi leo bado tupo vilevile kukimbia tu na kucheza pasi za upande m1 hivyo kuonekana tunafata mpira,licha ya kwamba tumecheza na timu kubwa kama Senegal,Cameroon, New Zealand, Ivory Coast lakini wapi Stars wanashindwa kuiga. Mbona tunaweza kuiga vitu vingine inakuaje tunashindwa kuiga kucheza kama timu nlizozitaja hapo?

    ReplyDelete
  11. Marangu OneJune 09, 2010

    Narudia nilichosema tangu zamani. HILI WANJA HATULIWEZI KULIENDESHA WABONGO. Tulikodishe kwa wataalam waliendeshe ki weredi na kibiashara.

    Mambo ya TFF kutaka kuhodhi kila kitu ni uroho tu wa pesa walionao viongozi wa TFF kwa maslahi yao binafsi.

    TUKIENDELEA KUENDESHA HUU UWANJA KWA NAMNA TUNAYOFANYA SASA, HAUTADUMU HATA MIAKA MITANO.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 09, 2010

    nafurahi sana kucheka asanteni wadau mliokuwepo uwanjani, uzuri watanzania tunasifika kwa kujieleza madhaifu yetu, ila sasa sumu yasitoke kwa mtu asiye raia wa tanzania, naamini nchi zirani wanachukua haya yote hususani kama walifuatilia kuhusu kamau, iwe wakenya, waganda, warundi, warwanda...

    nashukuru kwa fursa ya kucheka na kusikitika, usanii ukiisha tutasonga mbele

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 09, 2010

    MIMI BINAFSI SIMKUBALI TENGA NA TIMU YAKE.NI WABABAISHAJI MNOO. ATUAMBIE HIZO PESA BIL3 AMEZITOA WAPI NA ZIMETUMIKAJE? MANAKE KAMA NI UWANJA HAUKUJAA, AFU HAKUKUWA NA TANGAZO LOLOTE LA KUITANGAZA NCHI YETU KIMATAIFA,MAANDALIZI FINYU MPAKA NYIBO ZA TAIFA MNASHINDWA KUZIANDAA? HUO WOTE NI UROHO WA PESA KWANI KUNG'ANG'ANIA KILA KITU KUKIANDAA NINYI WENYEWE MATOKEO YAKE NDIO HAYO

    ReplyDelete
  14. abhachina!June 09, 2010

    Kuna jamaa alialikwa kuendesha semina kwa Maaskofu na Wachungaji juu ya Ujasiliamali.

    Power-Point ikamgomea ghafla picha ya ngono ikafunguka kwenye screen kubwa ukutani!

    Ndiyo haya tuliyoyaona juzi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 09, 2010

    Dundu ku dundu ku dundu!!!(vingoma).ALAJI,ALAJI! aka Wimbo wa taifa wa Brazil.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...