WADHAMINI wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wamesema wanatarajia kuweka wazi mkataba wao mpya watakaoingia na Shirikisho la Soka Nchini (TFF), kabla ya kuanza msimu mwingine wa ufadhili wake.
Vodacom inatarajia kumaliza mkataba wake wa miaka mitano wa kudhamini ligi hiyo mwakani.
Akizungumza jana katika semina elekezi ya Wahariri wa Habari za Michezo, iliyoandaliwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza, alisema nia ya kuweka mkataba huo wazi ni kutaka kuifanya ligi hiyo kuwa na uwazi kwa klabu shiriki pamoja na wadau wengine wa soka.
Rwehumbiza alisema kumekuwepo na maoni mbalimbali juu ya kuwepo kwa uwazi wa mkataba wake wa ligi hiyo kusema hivyo ni lazima mdhamini aheshimu maoni ya wadau wake ambazo ni nguzo ya maendeleo ya soka kwa ajili ya kuimarisha.
Alisema baada ya kuweka wazi udhamini wake, klabu zitapata nafasi ya kujua zinapata na kupokea nini kutoka kwa mdhamini wao huku TFF nayo ikipaswa kujua mipaka ya kazi zake na umuhimu wa mdhamini katika ligi hiyo.
Alisema mbali ya hilo, wanatarajia kufanya marekebisho baadhi ya vifungu katika mkataba ujao ikiwa ni pamoja na kujadili mapungufu ambayo yamejitokeza katika mkataba utakaomalizika.
Alisema ni kweli kuna mapungufu katika mkataba wake wa sasa lakini mapungufu hayo ni lazima yafanyiwe marekebisho kwa kuwa kila kitu kinahitaji kukosolewa kabla ya kuboresha zaidi.
Katika semina hiyo, waandishi walitoa maoni mbalimbali juu ya udhamini wa kampuni hiyo huku wakitoa ushauri wa jinsi ya kuboresha michezo mingine kwa ujumla na kutambua umuhimu wa ushirikiano baina ya mdhamini na vyombo vya habari.
Semina hiyo ya siku mbili ilifunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Taifa(BMT)Idd Kipingu na lengo likiwa ni kuwapa wahariri wa habari za michezo kujua wajibu wao wa kazi pamoja na kutambua umuhimu wa michezo katika jamii.
Huyo dada picha ya mwisho anahaingaika na simu matokeo yake yataonekana kwa yatakayoandikwa ktk gazeti lake!!
ReplyDeleteNamuona sapa kochi anaandika makala ya kumlaumu kocha mpya wa staz kabla hata hajaanza mzigo. Maximo oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteWahaariri wawili hawajatulia katika semina!
ReplyDelete