
Tanzania Association taifa ambayo inasimamia swala hili ikisaidiwa na ubalozi, imeyatambua maeneo matatu ambayo Dr Kamara atayatembelea na tarehe na muda kama ifuatavyo:

Inategemewa kwamba wanajumuiya waishio Luton, Oxford, Milton Keynes, Slough, Bristol, Birmingham, Coventry, Northampton na maeneo mengine ya karibu watahudhuria kongamano la London au Reading.
Vile vile inategemewa kwamba wanajumuiya waishio Leicester, Leeds, Liverpool na maeneo mengine ya kaskazini mwa UK watahudhuria kongamano la Manchester.
Hata hivyo, hakuna kinachomzuia mwananchi kuhudhuria kongamano lolote kati ya hayo hapo juu iwapo tu atatimiza sharti moja kama ilivyoorodheshwa hapo chini.
Angalizo: Ili kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata nafasi ya kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika hali ya usalama na isiyo na usumbufu, wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika mkoa ambapo kongamano wanalotegemea kuhudhuria litafanyika.
Utaratibu wa kujiandikisha kwa mkoa wa London tumia e-mail ifuatayo: talondon@gmail.com
Kongamano la London litafanyika ubalozini:
Tanzania High Commission
3 Stratford Place W1C 1AS, London.
Kwa maeneo mengine, TA taifa itatoa maelezo zaidi hivi karibuni.
Kwa wananchi Reading, kongamano litafuatiwa na sherehe maalumu - Tanzania Night. Kwa maelezo zaidi tafadhali fuatilia habari hii.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ziara hii tafadhali wasiliana na TA taifa hapa: watanzaniauk@hotmail.co.uk
07846783365 or 07536497772
KWA NIABA YA UBALOZI NA TA WOTE MNAKARIBISHWA
By Director of Communication - TA National
1. Are we to understand that you are targeting only Tanzanians / East Africans living in England only? Or the UK as a whole? What about hose who are in Wales, Northern Ireland, Scotland, and the Islands?
ReplyDelete2. Some of us would have loved to attend but have Immigration issues, thereby limited movement within the UK, how can we be helped?
I do not support the EAC at all! It has to remain as the European kind of community but NOT as one Country. We need Tanzania!We need our Land! Land is the way,we are defined on this planet-Earth. People,our grandfathers fought for it! Why are we, grandchildren give it freely again just of the EAC fantacy? Why?...We cannot live together as one State at all with Kenyans....Our Northern neighbors have no LAND!!!....They sold their land!...And we cannot tolerate their war-like violence behavior!...I cannot be convinced totally EAC to be one country! It's to remain for ONLY bussiness,security etc...purposes NOT land-ownership,allowing Immigrations or citizenship!...We were stang once in 1977,that's one lesson to learn from Kenyans! Northern neighbors have so many problems which they need to resolve as we did ours.We do not enteract we Kenyans even outside Tanzania;how are we going to live with them! EAC?...I can't believe Tanzanians fantancizing this idea at all!Chakubanga
ReplyDeleteSafari hii ni ya kichekesho kwa namna fulani.nafikiri hii safari na mawazo ya watanzania ingekuwa ya maana sana kabla na siyo kwa sasa.
ReplyDeleteBaadhi ya maswala anayotaka kuyazungumzia huyu mheshimiwa yameshaamuliwa na wakuu wa nchi hizi 5, sasa sijui hata kama sisi watanzania tukitoa mapendekezo fulani yatajumuishwaje katika mchakato mzima!
Please, namuomba huyu mh, afenye research kwanza
na ikiwezekana apate ushauri wa akina Dr shayo ambaye kwa raha zake ameamua kurudi Tanzania kulijenga Taifa kwa nafasi yake kama mtanzania
Wanablogu ya Jamii,
ReplyDeleteJumuiya ya Afrika Mashariki inalojumisha Soko Huria tayari "IMESHAWASILI". Hilo limeshafanyika, huu sio wakati tena wa kujadili iwapo tuingie kwenye Jumuiya au tusiingie. Ni kwamba tumeshingia au tumeingizwa na viongozi wetu (kila Mtanzania anatafsiri yake!!).
Badala ya kuwa na maoni hasi, wakati huu ni muhimu sana kuelewa kwa undani ni sera zipi Serikali hizi zimekubaliana na yapi hazijakubaliana. Tuelewe kiundani ni yapi ambayo Serikali yetu inaamini tutanufaika kutoka kwa nchi nyingine jirani na yapi tujihadhari wenzetu wasinufaike kutuzidi kwa mgongo wetu.
Tusipochangamkia nafasi hii ya kumhoji Waziri kwa MASWALI na kupata MAJIBU ya kueleweka tutakuja kujilaumu huko mbeleni mara tutakapokuja kuona Majirani zetu wananufaika na Jumuiya kuliko sisi.
Hima Watanzania tusisononeke na kutoa dukuduku zetu vijiweni peke yake, tujitokeze tuhoji yale yote yanayotukera na kuunga mkono yale yote yanayotufurahisha kwenye mikutano hii.
NB: Maoni yangu Kwa Wahusika - Ingalikuwa vema hii Mikutano ingepangwa kufanyika kuendana na jiografia ya UK; London (South), Birmingham (Midland) na Manchester (North).
Nimeangalia kwenye Tovuti ya Wizara husika http://www.meac.go.tz/documents/list_cat_docs.php?intCatID=15 kwenye kipengele cha “Document and Publications” ambapo ndipo panatakiwa kuwa na nyaraka zote muhimu. Hicho kiunganishi hakifanyi kazi/ hakika hizo nyaraka (ukiondoa hotuba 2 za Waziri Bungeni). Ni muhimu nyaraka hizi ziwekwe kwenye tovuti au zisambazwe kwa Watanzania kwa e-mail wiki kadhaa kabla hii mikutano. Itakuwa vema na muhimu sana maswali atakayoulizwa Waziri yatokane na Nyaraka Rasmi za Kikazi badala ya habari za Magazetini (peke yake).
Ahsanteni.
Soames Phares,
Reading , UK.
Why UK only.
ReplyDeleteJe tunafikiri kuwa mawazo ya Watz ughaibuni yanawakilishwa na kwa kujitosheleza na waTZ walioko Uingereza pekee?
I am sure something better with a wider representation could be organized.
this is stupid,
ReplyDeleteMawaziri mmeanza tena kupoteza hela za walipa kodi kwa kufanya utalii nchi za nje huku hali halisi nyumbani ikiwa mbaya. this is very funny. why should you start in UK not in mozambique, Malawi, Ethiopia, Rwanda etc. Huu ni ufujaji pesa. hayao mawazo kwa nini yasichukuliwe na wafanyakazi wa Serikali huko UK. Nini Balozi wa Tanzania anafanya na maofisa wake. thjis is wastage of taxpayers money...Mimi naita ni utaliii huuu,
Mhe. waziri najua umesoma na kuelimika ipasavyo but this is a cheap lie to taxpayers.
nakubaliana na kukusanya maoni ya wananchi popote walipo ila si kwa njia hii ya kusafirisha mawaziri huku waheshimiwa mabalozi na maofisa wao wakichapa usingizi. kama Balozi za tanzania haziwezi kuelezea mchakato wa EAC basi rudusha nyumbani wote, peleka serious pipo. Yaaani kuelzeas hizo milestone za regional intergration hadi tumpeleke Pinda,Kamala, sijui nani, sijui nani UK...you cany be serious...!
...
Ankali Michuzi...I am serious about what I write here....
Naomba ufafanuzi kuhusu saa ktk ratiba:
ReplyDeletelondon saa 10:00 mpaka 12:00 ina maanisha nini? ni
10Am mpaka 12pm au
10:00 hrs mpaka 12:00Hrs au
saa 10 jioni mpaka saa 12jioni
Maana director wa communication anaweza kuwa anafikiria kiswahili lakini masaa anaandika kiinglishi au masaa ya vituo vya treni/aepoti
Mdau
london siku ya Ijumaa saa kumi watu wawe kwenye mkutano wa waziri.wakati muda wa kazi kwisha ni saa kumi na moja jioni.
ReplyDeletehawezi kupata watu labda viongozi wa Jumuiya.
kwanini Birmingham hafanyi mkutano?sababu London na Reading ni kama eneo moja.
angefanya mkutano mmoja Reading/london halafu wa pili ukawa Birmingham au Manchester wa watatu ukafanyika Ireland kwa kina TEMU wana community nzuri na inafanya kazi kubwa.
safari ya kipuuzi kabisa. na hakika haya ndiyo matumizi mabaya ya pesa za wananchi. kama ni maoni wanaweza kutoka kwa njia nyingi na mojawapo ni waziri kutupa email yake tukamwandikia. Kweli kazi ipo. Kama ndo hivi Tanzania itaendelea kuwa maskini tu.
ReplyDelete