WANANCHI WA AFRIKA MASHARIKI
MIONGONI MWA WASHINDI WA TUZO LA MAZINGIRA BORA UINGEREZA
-Na Freddy Macha, London
Nchi zetu Afrika Mashariki ni miongoni mwa Washindi sita waliopata tuzo la kimataifa la Ashden mjini London. Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka na duka maarufu tajiri la Kiingereza Sainsbury kwa wataalamu wanaosaidia kujenga mazingira bora na kuendeleza maisha ya wananchi.

Kati ya washindi ni Mkenya Samweli Kinoti na Mganda Chris Mulindwa waliokutana nami na mtengeneza sinema wa Urban Pulse, Baraka Baraka, jana mjini London.
Wananchi hawa wanaongoza mashirika yanayoshirikiana na makampuni mengine ya kimataifa kuunda umeme unaotegemea jua na kinyesi cha ng’ombe. Mwangaza huo ni wa bei nafuu na rahisi kutumia kiasi ambacho mategemeo ya miaka mbeleni ni kila wananchi wa kawaida (hasa vijijini) kutopata tena shida za umeme, TANESCO na kero za mgao unaotesa wazalendo kila siku.
Tuzo la Ashden iliyoanzishwa mwaka 2001 na Bi. Sarah Butler-Sloss humzawadiya mshindi wa kwanza paundi 30,000 na wawili wengine 20,000 kila mmoja. Mwaka huu tuzo zimekwenda kwa wananchi toka Marekani, Vietnam, Uholanzi, Brazil, Uganda, Kenya na India.
Serikali za Afrika Mashariki zimeombwa kuendelea kuunga mkono jitihada za kujenga umeme unaotegemea jua na mali asili kwa kuwa ni wa bei nafuu na rahisi zaidi kutumiwa na mamilioni ya wananchi vijijini.
Soma habari zaidi
Aisee Michuzi hebu hariri kichwa cha habari AFRIKA MASHARIKI OYEE...
ReplyDelete