Mtaalamu toka Kenya aliyeshinda tuzo, Samwel Minoti, wa kampuni ya Sky Link, akimfafanulia Baraka Baraka wa Urban Pulse, namna sayansi ya kutumia kinyesi cha ng'ombe kutengezea umeme na mwangaza unavyoanza kuwafaidia wananchi wa Kenya.
Mtaalamu na mshindi wa Kimarekani, Ned Tozun, akimfafanulia Baraka Baraka namna umeme huu wa jua na mali asili unavyotumika kirahisi, mjini London, Jumatatu. Tanzania ni moja ya nchi chache duniani zenye ofisi ya kampuni yake yaani D Light. Picha zote na Freddy Macha

WANANCHI WA AFRIKA MASHARIKI
MIONGONI MWA WASHINDI WA TUZO LA MAZINGIRA BORA UINGEREZA
-Na Freddy Macha, London

Nchi zetu Afrika Mashariki ni miongoni mwa Washindi sita waliopata tuzo la kimataifa la Ashden mjini London. Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka na duka maarufu tajiri la Kiingereza Sainsbury kwa wataalamu wanaosaidia kujenga mazingira bora na kuendeleza maisha ya wananchi.

Kati ya washindi ni Mkenya Samweli Kinoti na Mganda Chris Mulindwa waliokutana nami na mtengeneza sinema wa Urban Pulse, Baraka Baraka, jana mjini London.

Wananchi hawa wanaongoza mashirika yanayoshirikiana na makampuni mengine ya kimataifa kuunda umeme unaotegemea jua na kinyesi cha ng’ombe. Mwangaza huo ni wa bei nafuu na rahisi kutumia kiasi ambacho mategemeo ya miaka mbeleni ni kila wananchi wa kawaida (hasa vijijini) kutopata tena shida za umeme, TANESCO na kero za mgao unaotesa wazalendo kila siku.

Tuzo la Ashden iliyoanzishwa mwaka 2001 na Bi. Sarah Butler-Sloss humzawadiya mshindi wa kwanza paundi 30,000 na wawili wengine 20,000 kila mmoja. Mwaka huu tuzo zimekwenda kwa wananchi toka Marekani, Vietnam, Uholanzi, Brazil, Uganda, Kenya na India.

Serikali za Afrika Mashariki zimeombwa kuendelea kuunga mkono jitihada za kujenga umeme unaotegemea jua na mali asili kwa kuwa ni wa bei nafuu na rahisi zaidi kutumiwa na mamilioni ya wananchi vijijini.
Soma habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Aisee Michuzi hebu hariri kichwa cha habari AFRIKA MASHARIKI OYEE...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...