WANANCHI wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao bure Julai 24 katika kituo cha afya cha Ahueni Medicare kilichopo Tandika, Mtaa wa Berege No. 17 Dar es Salaam ili waweze kujua hali zao kiafya.
Wito huo umetolewa Dar es Salaam jana na Msemaji Mkuu wa Kituo hicho, Bi Gladys Mkony alipokuwa akizungumza na blog ya jamii.
Amesema kuwa kituo hiki kimeona kuna haja ya kutoa huduma hiyo kwa jamii kutokana na jamii kubwa kutokuwa na tabia ya kujua hali zao kiafya.
Amesema zoezi la upimaji litakuwa la mfululizo ambapo litaanza July 24, mwaka huu saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni na litafanyika kwa siku mbili.
Afisa huyo amesema vipimo vitakavyotolewa bure kuwa ni pamoja na kisukari,virusi vya UKIMWI (VVU), shinikizo la damu na uzito na kwamba vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya upimaji vinapatikana pia vimekidhi ubora kwa matumizi ya afya ya jamii.
Ameongeza kuwa zoezi hili litakuwa ni la kudumu na taasisi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa wa eneo lilipo kituo hicho, itatoa utaratibu amabao utaeleza ni lini mchakato huo utaendelea.
Amesema kutokana na matakwa ya baadhi ya wakazi kilichopo kituo hicho uongozi wa kituo unatarajia kuanza zoezi la upimaji wa afya kwa wazee ambao hawawezi kutembea kutokana na umri mkubwa kwa kuwafuata majumbani.
Amesema ili kufanikisha hilo kituo hicho kinahitaji ushirikiano wa kutosha na uongozi wa serikali za mtaa na wakazi wa eneo husika.

tatizo lenu mnataka kupimangoma tu magonjwa mengi kwani hakuna then matibabu je ?nayo yawe bure basi!1
ReplyDeleteHongera mwenye kituo na Mungu akuongezee. Watu wengi TZ wanaishia kufa kwa magonjwa ya kuzuilika na wengine kwa vile wamengunduliwa wakati ugonjwa umeshasambaa mwilini mzima.
ReplyDeleteNi jambo zuri sana hilio mlilofanay na natumaini watu wengi watachukua hii nafasi na kuja kupiama.
Na pia mangeengeza vipimo vya wanawake kama pap smear na mammogram. Ni wanawake wanagapi wanakufa na cancer ambazo kama wangetibiwa mapema wangeishi.
Nawapongeza sana kwa hili na natumaini watu wengi wenye facilities kama zenu watafuta moyo wako,
SHUKRANI NYINGI ZIWAFIKIE HAWA NDUGU WA AHUENI KWA KUTOA HUDUMA HII BURE KABISA. HII INAONESHA WAZI KUWA KITUO CHENU KINATHAMINI HASA AFYA ZA WAKAZI WA TANDIKA. NA HII HUDUMA YA KUWAFUATA WAZEE NADHANI NI YA KUIGWA SI KILA MTU ANAUWEZO WA KUMSAFIRISHA MZEE KWENDA KITUONI KWA AJILI YA KUPATA HUDUMA YA VIPIMO.
ReplyDelete