Na Shaaban Msangi
wa Jeshi la Polisi

Benki ya NMB kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi hapa nchini wamewazawadia askari wawili wa Jeshi hilo kiasi cha shilingi milioni sita kila mmoja pamoja na vyeti vya ujasiri kwa kitendo chao cha kishujaa cha kupambana na majambazi na kufanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha fedha wakati wa tukio la ujambazi lilitokea hivi karibuni katika Benki ya NMB Tawi la Maswa Mkoani Shinyanga.

Kiasi hicho cha fedha kilikabidhiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema katika hafla fupi iliyofanyika Wilayani Maswa ambapo pia ilihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi wa Maswa akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB hapa nchini Bw. Ben Christian.

IGP Mwema aliyewasili Wilayani Maswa kwa Helkopta majira ya saa 6 mchana akiambatana na Mkuu wa Operesheni Maalum, Naibu Kamishna Venance Tossi na kupokelewa na umati huo wa wananchi alikagua gwaride lilioandaliwa rasmi kwa ajili yake na hatimaye moja kwa moja kuanza na zoezi la kuwazawadia askari hao.

Askari waliozawadiwa kiasi hicho cha fedha ni G. 2001 Pc. Abas na G.4382 Pc. Kelvine ambao ndio waliopambana na majambazi wapatao saba waliovamia Benki ya NMB Tawi la Maswa Julai, 23 mwaka huu na kufanikiwa kupokara kiasi cha milioni saba lakini wakishindwa kupata fedha nyingine zilizokuwa zimehifadhiwa katika chumba maalum "strong room" ya Benki hiyo kutokana na kukumbana na upinzani mkali wa askari hao.

Kwa mujibu wa IGP Mwema wakati wa mapambano hayo ya kurushiana risasi baina ya majambazi na askari Polisi, majambazi yalizidiwa nguvu na mmoja wao kuuawa na askari hao na mwingine kukamatwa kwa ushirikiano na wananchi wa Wilaya hiyo waliotoa msaada kwa askari mara baada ya kuona purukushani kubwa katika Benki hiyo.

Akizungumza mbele ya wananchi walioshuhudia tukio la utolewaji wa zawadi IGP Mwema alisema kuwa Jeshi lake kupitia mpango wa maboresho yanayondelea ndani ya Jeshi hilo wameamua kutoa kiasi hicho cha fedha katika kutambua kitendo cha ujasiri na ushupavu kilichoonyeshwa na akari hao ambao bado ni wachanga kazini pamoja na kuhamasisha utendaji kazi kwa askari wengine.

"Muda wenu kazini bado ni mdogo kutokana na kuajiriwa tu hivi karibuni lakini mambo makubwa ambayo mumeyafanya hata wananchi wa Maswa ni mashahidi na yanahitaji kuigwa na askari wengine nchini kote na kuwa kitendo hicho ni ujasiri unaohitaji kupongezwa na kila mwanajamii." alisema Mkuu huyo wa Polisi.

"Hivyo kwa kutambua hilo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Benki ya NMB ambayo hata Mkurugenzi wake Mkuu Bw. Ben Christian tunaye hapa leo hii kwa pamoja tunawazawadia kila mmoja wenu kiasi cha shilingi milioni sita pamoja na vyeti vya ujasiri" aliongeza IGP wakati anakabidhi fedha hizo.

Aidha kwa mujibu wa maelezo ya IGP kiasi cha milioni sita zimetoka Jeshi la Polisi na kiasi kingine cha milioni sita kimetolewa na Benki ya NMB katika kutambua mchango wa Jeshi la Polisi.

IGP Mwema alitumia fursa hiyo pia kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Maswa kwa ushirikiano ulionyeshwa na wananchi hao na kuwataka kuwa ushirikiano huo uwe ni wa kudumu hususani katika kipindi hiki sambacho Jeshi hilo limeamua kuwashirikisha kwa dhati wananchi katika kupambana na uhalifu.

Aidha pia aliwaambia wananchi hao kuwa ushirikiano wao pia umelisaidia Jeshi la Polisi kwakuwa mpaka sasa watu wanaosadikiwa kushiriki katika tukio hilo wameshakamatwa kwa hatua nyngine zaidi. Aliwataka wananchi hao kuongeza juhudi za kutoa taarifa nyingi za uhalifu ili iwe msaada kwa Polisi kuzifanyia kazi kabla matukio hayajotokea.

"Watanzania wenzangu mapotupa sisi taarifa mapema za uhalifu zinasaidia kuzuia matukuio hayo kutokea kuliko kusubiri yatokea na kisha kutumia nguvu kubwa na rasilimali nyingi katika kupambana nayo" alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bw. Ben Christian alisema kuwa Benki ya NMB inatambua kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama wa Raia na mali zao na kulitaka Jeshi hilo kuongeza juhudi ili wao kama Benki waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    PESA TU AITOSHI INCASE MAJAMBAZI WAKITAKA KUWATAFUTA HAO MAPOLICE INABIDI WAAMISHIWE MAENEO MENGINE YA KAZI.NA KWAKUFANYA KAZI NZURI WAWAPANDISHE CHEO KIDOGO NA KUWAPELEKA SHULE WAJIENDELEZE ZAID NI MFANO WA KUIGWA WAMETOA HAWAOGOPA KUFA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2010

    Anon wa 04:15 umesema kweli. Wapatieni elimu na cheo ili wajiendeleza. Ila tukio hili limetokea lini? Supu ameandika JULY 23 wakati leo ni JULY 17!!!!
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  3. msemakweli -ukJuly 17, 2010

    Hii habari sijaielewa mana inasema majambazi walivamia NMB Maswa tarehe 23 Julai mwaka huu wakati leo ni tarehe 17 julai sasa waliwezaje kuvamia siku yenyewe haijafika ya tarehe 23 julai.Hebu kuweni makini bwana mnatuchanganya

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2010

    muwe mnasoma na magezeti ya tz hizo habari ziko kwenye magezeti yote ya tz mdau wa tx

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2010

    WAHAMISHIWE MKOA MWINGINE KWA SIRI KUBWA WATU WASIJUWE, NATOWA OMBI HILI KWA SAID MWEMA MWENYEWE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...