Home
Unlabelled
askari uwanja wa ndege dar wanaogopa wazungu??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hawa jamaa ni kero sana pale airport,elimu zao zenyewe uchuro,wanaomba passport ukishawapa wanshindwa kusoma na kubaki kuuliza ,unafanya nini huko,una muda gani?Hii kero,tuwaumbue hawa,wana tabia mbaya sana.
ReplyDeletesi unajua kimombo hakipandi... hawataki kuaibika, ila sasa ndo itatukosti
ReplyDeleteTatizo ni njaa wanaendekeza,na elimu ya kukariri hiyo
ReplyDeletehahahaha lugha mkuu,wataongea nini? nakumbuka wakati tuko ma-teenager askari/trafiki wakitusimamisha tulikuwa tunaongea kiingereza gari nzima haichukui hata dk 2 utamsikia polisi akisema go go go.
ReplyDeleteMdau Polisi kiingereza hawajui, sasa wataongeaje na wazungu?
ReplyDeleteNdio maana wanaongea na wabongo tu hapo airport.
Ila hii ni utendaji mbaya. Wazungu wakishajua hawakuguliwi airport yetu kuna baadhi yao macrook watajaribu kuvusha madawa.
HII NDIO TABIA YAO HAWA WATU, HAWAJAANZA LEO SIKU NYINGI TU. MI ATA SIJUI WANATAKA NINI KWA WAMATUMBI, LABLA WATUAMBIE KUSUDI LAO NI NINI.
ReplyDeleteyaan mdau hapo hata mimi yamenikuta wanaogopa wazungu kinoma. halafu hawajiamini kabisa
ReplyDeletewakati wa kuondoka unatakiwa na safari njema maswali unaulizwa kwa busara. subiri utue
ankal me imenikuta hiyo, nimerudi safari yangu nilikuwa nimeenda kutembea kidogo nchi jirani, kidogo naona naitwa dada pasport, wakti hapo nimekutana na watu kama wa nne wanaingalia, nawapa maswali ya kijjinga eli ulienda kufanya nini jibu kusalimia , ni nani unamaliza hapo kunawanaojificha pembeniya mlango wa kutoke utasikia oya pasiport, unampa tena. wamekagua weeeee, unakaa wapi, nikawatajia unafanya nini nikataja nikajibu, mbona unaoneka umeenda uganda, sijiu, ghana kataja boda zote, nikamwambia me huko naenda kikazi, mara ya kwanza nimewaaambia nasoma ili niwaone wanataka anini, enh unafany kazi wapi, nikawatajia sehemu moja nyeti sana, mbona walinirudishia haraka nikataka kuwapa id, wakakaataa. ila wale wazungu walipita sie akina juma majimarefu tunasumbuliwa kweli.
mbona nchi za wenzetu si wasumbufu hivi, kwanini hapa kwanini , yaan wanasumbu sana wakiona umeingia boda nyingi hata kama kwa miaka tofauti wanadau siju utakuwa unaunga au gaidi, me wananiketa kwanza hawajasoma kwanini wazungu wanawaogopa,
hawapendi kweli tusafiri zaidi ya kibaha chalinze, mbeya ila ukivuka boda tu wananuna wanaona kama umeenda kuchukua mamilion, me naongea kwa uchungu kwani yamenikuta two tymez, yaan wanatusumbu sana,
Huwa sicomment lkn kwa hili leo najirusha ulingoni! Hawa jamaa wamegeuka kuwa Matonya, kauli kama ''tuachie basi hizo hela (madafu) za nini huko unakokwenda?'', airport za ugenini tunyanyaswe na za nyumbani pia! hii ni ubaguzi wa rangi, hata kama ni random sample - inabase kny rangi? Pia ni kukosa kujiamini kwa polisi,na approach zisizo na kichwa wala miguu mf ''unasimamishwa na kuulizwa umeniletea zawadi gani - sikujui wala hunijui?'',Tubadilike jamani anza na salamu mf.pole kwa safari nk ndio uanze hiyo kazi yako, viongozi wengine haya hamyaoni? hamjifunzi mnapotembelea viwanja vya wengine? wapelekeni nje wakajifunze, shule(lugha), kauli(approach), usafi binafsi(awe kny sare au bila sare)polisi mkiwa hapo ni kioo cha nchi na sio kama mtu binafsi!
ReplyDeleteMichuzi usiibanie hii comment ili iwasaidie ktk kuboresha kazi zao
Mdau Netherlands
NB:Nawashauri wafungue blog yao kuwasaidia wananchi kutoa mawazo yao
Hakuna cha ajabu hapa ndiyo kasumba ya mtanzania. Nadhani Tanzania ndiyo nchi pekee dunia ambayo mgenia anaheshimika zaidi ya mwenyeji. Ajabu kubwa sana.
ReplyDeleteTatizo huwa ni LUGHA. Askari wetu hawajui akimsimamisha mzungu atamwambiaje?...kwa hiyo anabaki kufuatilia wamatumbi tu. Ukitaka kuhakikisha kwamba hii ni kweli, ukisimamishwa tu ongea kizungu...utaona mara moja unaruhusiwa kupita...
ReplyDeleteKwa kweli sio haki hata kidogo, mbona hao wazungu ukiingia tu kwenye airport zao wanakudaka haraka haraka yaani weusi ndio ma suspect wakubwa wao kwa wao utaona wanaonyesha passport zao wakiwa wamezishika bila hata kuhand over kwa manjagu wao. Kwa nini kwetu iwe oposite??
ReplyDeleteni kweli bwana,wamezidi hao.Tatizo
ReplyDeletelao ni makanumba ndio maana wanawaogopa wazungu. then wanatuonea sisi wenye nchi
Ni kweli mdau na tatizo kubwa la mapolisi wetu ni kutojua lugha ya Kiingereza 'Ung'eng'e' wenyewe wanaita hivyo ndo maana wanaogopa kuwahoji wazungu hakuna zaidi ya hilo...
ReplyDeleteme naona wajipange tena wanafanya kuwe kama kariakoo manaana hawana utaratibu eti umesafiri lini unakumbuka ulisafiri mara ya mwisho lini, miswali kama umeua, we mtu anamambo yake ya kawaida tu, unaanza kumshuku mpaka unamuwekea wakt mgumu. wananichefua sana, sijui std 7 hawa, maana maswali yao yamekaa kutotaka usafiri uogope usisafiri tena. maana meusumbufu ya pale balaa, me nimeenda kutafuta shule me swali kama wanatoka usingizini. nimekasirika maana nilikukwa nawajibu nipendavyo unajua ifike sehemu ufanye kazi yako iheshimike na watu na wewe pia kutokana na pafomarce yako na unavyo waatend customa.
ReplyDeleteyaan anaona yeye anamamla mapaka kwenye maisha yako binafsi,hapana simamieni usala wa nchi na wananchi si kufanya hivi aibu sana, daa,
Polisi bongo wanawaonea wamatumbi kwa kuwa wanajua wengi hawajui haki zao km raia. Wazungu wako makini ktk hilo na ndio maaana wanawaogopa. Wanachotafuta hapo ni hela ya supu tu...
ReplyDeleteNadhani kwa sababu askari walio wengi "English is not reachable"!!!
ReplyDeleteHuo ni ulimbukeni sasa mimi sioni sababu ya kuwaogoga kuwasachi hao wazungu.maana wanatakiwa kujua hata sisi hutusachi sana tunapofika kwenye nchi zao mfano ukifika LONDON HEATHROW...ujiandae na ole wako ujikanyage kanyage utasachiwa mpaka basi na ukishindwa kujieleza imekula kwako.Askari wa bongo fanyeni kazi acheni uzushi.
ReplyDeleteMdau -Ukerewe!!!
Hii inaudhi saaaana, ni utumwa wa ki fikra ambao baadhi ya watendaji katika nyadhifa mbalimbali bado wanao. Wanacho hitaji hawa maaskari ni elimu ndogo ya ziada kuhusu uzalendo na wageni na pia exposure matters waone nchi zingine jinsi wageni wanavyotendewa nchi za wenzetu.
ReplyDeleteHii kweli kabisa ndugu yangu. Mie mwenyewe nime-experience. Wapuuzi sana
ReplyDeleteMdau
wataongea nini?
ReplyDeletena hii hali ipo sehemu yoyote kwenye awa wavaa magwanda,hawagusi mtu mwenye nywele zilizonyooka na asiye na melanin sijui...
kwakweli nawadharau sana izi mtu,uoga uoga uoga!!na kunyanyasa wabantu...
ni ujinga wa hali ya juu Tz
Ni kweli hii tabia ipo sana bongo tena maeneo mengi tu pamoja na airport. Wenzao mtoni wanaangalia sana wageni maana ndiyo target yao wanaweza kulata chochote...hasa hawa wathungu wana biashara nyingi mno kuna wengine wanajifanya kuja kutalii kumbe wana mambo yao mengine pia. WANAKUJA NA MZIGO WANAONDOKA NA MZIGO TENA BILA HATA KUANGALIWA TATIZO HATUFAHAMU NI NINI. WANAANGALIA WAMATUMB TU
ReplyDeleteUkivaa suti hawakugusi ukiwa na Tshirt au jeans unalo, Hawajiamini na wana wivu sana askari wa eapoti.
ReplyDeleteNi kweli mdau alicho kisema, na hiyo ipo kwenye viwanja vyote vya Afrika Mashariki na nchi nyingine za kiafrika. Inasikitisha mtu anarudi inchini mwake lakini anakukumbana na usumbufu mwingi kwa askari na maofisi wanaotukagua.
ReplyDeleteMmatumbi akienda nje ya nchi anapata usumbufu huo na akirudi anakuta usumbufu huo huo tofauti na wazungu ambao inakuwa tambalare kwao.
Kamanda Mwema upo hapo? Kova mh!
ReplyDeleteTatizo lao lugha hazipandi kabisa hao mapolisi, tafadhali jeshi la polisi pangeni mapolisi wasomi wenye ujuzi wa lugha sehemu kama za airport au la kila siku mtaambiwa mnapendelea wazungu kumbe mnawaogopa
ReplyDeleteMi wananikelaga kwelikweli, na maswali yao ya kizushi,eti umebeba nini?unampelekea nani?huko ulipotaka kuna vitu gani?usipojibu anaanza kulalamika unamzalau yeye yupo kazini,kazini kwa maswali ya kipuuzi ndo wanavyoajiliwa kwa huo upuuzi?
ReplyDeleteLugha baba!! iwe iwavyo tudumishe kiswahili mashuleni kwetu lakini kiingereza nacho pia tujifunze la sivyo hata wabeba unga/magaida tutawaacha wanapita kiulaiiiini! lugha ya mawasiliano muhimu.
ReplyDeleteSio tu askari kanzu, bali hata wanao kagua mizigo. kwanza wanataka pasipoti yako waiangalie halafu wanakagua mizigo wakati wazungu au watu weupe wanawaacha wapite. baada ya kukaguliwa mizigo hao askari huwa wanakaa pembeni ya geti karibu na kutoka wakiona una pasipoti ya kijani lazma wakwite au wakufuate halafu longolongo linaanza hapo.
ReplyDeletesio kwamba askari wasitukague ila wawe waadilifu na kutenda haki. Hiyo ni kazi yao na tunathamini kazi zao. Ukisafiri katika nchi za hao wazungu na wakakuona wewe mmatumbi kawaida wanakukagua ile mbaya wakati wananchi yao wakipita au wakikaguliwa juu kwa juu.
Matokeo mmatumbi hakubaliki ugenini wala kwao. kote haaminiki. Nahisi hawa polisi wetu lugha inawapiga chenga au hawajiamini. BONGO KAZI IPO.....
MDAU UTURUKI
Hao ma askari kanzu wana wivu kuwaona ndugu zao wanametoka nje kusafisha macho hiyo ni njaa tu inawasumbua wala hakuna cha zaidi.
ReplyDeleteHiyo ni kweli kabisaaa... mimi nimeoa mzungu na nilisimamishwa nikapekuliwa. Mke wangu na watoto wakaachiwa wapite... Nikatabasamu tu na sikubisha wala kutaka kusema kitu. Lakini moyoni nikawa ninawaza...kweli utumwa ungalipo hata sasa...Old stigma, low self esteem, infiriority complex na mambo yanayofanana na hayo...
ReplyDeleteHakika hii ni hatari kubwa kuwa na ukaguzi kwa matumiz tu bila ya wengineo kwa kuwa wamwera hao hawakiwezi kilugha cha kiingereza..... Iweje wawekwe hapo kama si kuruhusu madudu kuingia na kutoka? Hili liangaliwe haraka Aibu sana kwa gesh retu ra porish....
ReplyDeleteLAZIMA POLISI WA KIBONGO WAKIMBIE WAZUNGU, HAWAPATIKA RUSHWA KWA WAZUNGU, NA LUGHA HAIJATULIA, WANAOGOPA ASIJE KUULIZWA MASWALI MASWALI. AIBU TUPU..DAMN IT
ReplyDeleteinashangaza sana. ukienda ulaya na marekani wanaoandamwa ni weusi. hata huku wanaandamwa wao. jamani tutafika kweli.
ReplyDeletemzungu hampi nafasi mwafrika. hatutakiwi kuwaogopa. kwanza siku hizi wamekubuhu kwa mambo yasiyofaa.
Tatizo ni kikristu kaka....how the police gonna face white people with Kiswahili? They gotta deal with the "matumbi" as always lol, shule muhimu, I'm just saying......!
ReplyDeleteSI KWELI WANAOGOPA WAZUNGU TATIZO LUGHA ASKARI WETU WENGI HAPO UWANJANI LUGHA GONGANA,MINILIWADINDISHIA SIJUI KISWAHILI NA MKOBA WANGU WA KIKRISTO AWAKUANGALIA ATA NIMEZALIWA WAPI WAKAJUA MNYAMWEZI NIKAPETA NA SORY NYINGI,JAMBO HILI NI MUHIMU SANA MDAU KWA USALAMA WA TAIFA LETU KUNA WAZUNGU WENGINE PORI LAKINI KWA RANGI NA BLONDY WANAPEWA HESHIMA ZOTE KAMA WAZUNGU KWELI.
ReplyDeleteheheheh kweli wamenuna kama hawataki tusafiri na sisi , roho mbaya tu , na kweli wazungu wasumbuliwi , utasema wazungu malaika , sisi wenyewe watu weusi tunajidharau unadhani mtu mweupe atatuheshimu ?
ReplyDeleteKwenye kila kitu sio airport tu! jamani tunahitaji big change, waweke damu inayochemka, iliyokwenda shule kisawasawa, na wapo wengi ila ndio hayo mambo ya kibongo bongo kupeana kazi, ohh mtoto wa bosi flani... nyamafu kabisa shika mzungu huyo jama!!!
ReplyDeleteYes, Mdau....kwa kweli hawa askari wanatia aibu sana na nikero sana.
ReplyDeleteKwanza wana njaa muda wote, pia hata hawajidhamini mbele ya wazungu.
Wanadhani Mzungu = Mtu wa peponi.
Wanahitaji elimu ya kujitambua na kujidhamini.
Tunapinga racesim lakini sisi waafrika wenyewe tunaiendeleza ina one way kwa kujishusha dhamani.
HAPO IMEJAA RUSHWA TUPU, WAZEE WA KAZI INGIENI HAPO MUWANASE HAO, PILI WENGI WAO WANAJIFANYA NI WANA USALAMA KUMBE WIZI MTUPU WANAWANYANYASA SANA WABONGO WENZAO, HASA KATIKA ENEO HILO KATIKA PICHA, KULE NDANI KABISA IMMIGRATION HAWANA MATATIZO WAKO SAFI TENA WANASERVICE WATU VIZURI BILA MATATIZO LABDA MWENYEWE UWE NA MATATIZO.
ReplyDeleteAskari wa kiwanja cha ndege hawaogopi wazungu, ila njaa ndizo zinawasumbua. Serikali lazima ifikirie kuwalipa ujira unaoendana na hadhi ya kufanya kazi katika mazingira hayo.
ReplyDeleteBinafsi nikipita pale lango la mwisho kabla sijatoka nje ninasumbuliwa sana. Huwa waniambia mzee umetoka wapi? kosa uwaeleze ulikotokea Ulaya, cha moto utakiona! ila siwalaumu, bado nitalaumu umasikini unaosababishwa na viongozi wetu ambao wameja roho za ubinafsi.
Mheshimiwa umeweka kapuni mchango wangu ambao ni chachu kubwa kwa Taifa letu tukufu,sasa hata huu utauweka kibindoni?
Salam hizi zimfikie afande NZOWA popote alipo,vijana wake kiukweli wanainyanyapaa ngozi hii nyeusi na kuiona ndio ovu lakini wadhungu ndio wanawaona binadamu,matokeo yake sasa magenge ya mihadarati yanawatumia sana hao wadhungu ambao vijana wa mzee wangu NZOWA wanawaona kama hawawezi kubeba hizo dawa
ReplyDeleteNi mambo ya kuiga hayo, si ndivyo wanavyofanya viwanja vya ndege vya ughaibuni? Wazungu huachwa waende zao huku wakiwapekura wamatumbi ndani nje!!
ReplyDeleteNdio zao hao mie wamenifanyia hivyo kila mwaka nikipita hapo!!.Wajinga sana hao jamaa na ni dhiki tu ndio wanaendekeza na ndio maana unga bado unaingia kirahisi bongo.
ReplyDeleteNakubaliana na wewe 100%. airport za watu ukiwa mmatumbi lazima wawe na wasiwasi na wewe. watakusachi ile mbaya. na ukifika home same s@*t! give us a break
ReplyDeleteSABABU NI KUWA ASKARI WETU ENGLISH IS NOT REACHABLE, NDIYO MAANA "WANAWAOGOPA" WAZUNGU.
ReplyDeletebora umeletahii mada !airport yetu himeoza kabisa yani sijuhi sisi watanzania tuna matatizo gani?? mimi wlaisha niambia niweke adi ticket yangu ya kusafiria kwenye machine ya scanner !! yani wajomba wa airport wanatia sana huruma. kila mtu anataka kula. kama wafanya kazi wa airport wana kuomba pesa ndogo ndogo sasa. sasa wapo tayari kuachia vitu vingapi haramu kupita kwa sababu ya njaa zao.
ReplyDeleteI LIKE THIS TOPIC. KWAKWELI MIMI NI MSAFIRI WA MARA KWA MARA HII HALI INA UDHI SANA NA KUTIA AIBU. Kuna vitu viwili, 1- Lugha inakuwa tatizo wakiwasimamisha watawaongelesha nini? wengi kithungu hakipandi.
ReplyDelete2- Wengi wao wanatusimamisha sisi tuwape ili kitu kidogo that is very obvious.
Lakini wanasahau kuwa wazungu wengi au watu wa mataifa mengine wengi sio waaminifu wanaweza ingiza unga, silaha, biashara nk. Yote hiyo mimi nafikiri ni poor training na njaa. INABIDI TUIGE MIFANO YA WENZETU HUKU ULAYA JAMANI KHAAAAAAAA
Jamani tujifunze kutoka kwa wengine yaliyo mazuri, polisi kusimamisha wageni wanaoingia baada ya kupita immigration check sio uungwana wala kawaida sijaona nchi nyingine ila TZ. Ni kudhalilisha na haswa kama wazungu wapite wamatumbi wakaguliwe ni hatari
ReplyDeleteTATIZO LA ASKARI WETU LUGHA ZA KIMATAIFA ZINAWAGONGA NDIO MAANA WANASHINDWA KUWAHOJI HAO WAZUNGU
ReplyDeleteTatizo hawajui lugha au hawajiamini.
ReplyDeleteLUGHA LUGHA LUGHA BABAAAAAAAAAAA hahahahaha.
ReplyDeleteebwana hio nikweli kabisa naunga mkono hoja afikishiwe mh saidi mwema hawa jamaa ni premitives wanguvu wanawaogopa na kuwaheshimu wazungu kumbe hao wazungu wenyewe huku makwao hawana mpango wowote hawali mpaka waokote chupa za bia kudadadeki wanadhani kilamtu mweupe tajiri kuna mipolanda na romanians kibao wanakuja pande hizo kwa ishu za madawa lakini mipumbavu imelala tu inadhani ni wazungu macho yao mchshhhhhhhhhhhh
ReplyDeletehii inachekesha sana kuona polisi wa bongo wanawabugudhi wananchi wenzao! ni tofouti sana na nchi za ulaya mfano ujerumani katika viwanja vya ndege au stesheni za treni ukiwa mweusi basi askari polisi watakuuliza vitambulisho,na mzungu mwenzao hawana shaka nae.
ReplyDeleteLakini bongo ni noma tupu
Alafu hizi Tabia wanazo wanapenda Pesa tu Mtu ushapita Mwanzo na Kwenye mabegi washakutizama Hiyo mijamaa BAdo wanataka kutizama Passport tena mbele hapo kuonea Vijana tu.
ReplyDeleteWazungu wanawaogopa alafu Tabia nyengine watu hasa Nigeria na Wazungu wanajifanya Ambassador kumbe Passport Fake wanapita na Unga.
Hizo Tabia zifeeeeeeee. MZ.
hii hali imeweka na wazungu kila sehemu, kuna siku nilipita Ujerumani mwafrika peke yangu ndio nilisimamishwa na kusachiwa wakati wazungu wanajipitia sasa na huku kwetu inaendelezwa ,,ni aibu kubwa
ReplyDeletetawile dau jamani sio Airpot hata barabarani matrafiki nao ivo vio ukija uhamiaji watu tumekaa kwenye foleni mda tu ila wazungu wakija wanapita tu jamani ulaya tuface Urasisti na nyumbani pia???????? haiwezekani Anko tusaidie na hili jamni sie raia wakaida tena wazawa tunakandamizwa kuliko wazungu
ReplyDeleteNinaunga mada yako mdau,ni kweli askari na maafisa wanaokagua abiria wanaotua kwenye viwanja vya ndege Dar na Arusha wanaleta kero sana. Mmatumbi utakaguliwa kila kitu wakati wazungu hupita bila ya wasiwasi bila hata kuulizwa. Wekeni mashine za kukagua mizigo ili mtakae mtilia mashaka ndio mmpekue kuliko kupotezeana muda, na pia msibague mkidhani wazungu wao mambo yao ni safi. Hao ndo wanaoweza kuwa nyoka zaidi.
ReplyDeleteWamatumbi tuko kwenye tabu tu.Huku nchi za kimagharibi tunanyanyaswa tukisema twende nyumbani kazi ndio kama hiyo.Hususan ukipita kenya sijua hawa watu huona wazungu miungu watu,sijui kwanini wanapenda kuwapapatika wazungu na kuwadhalilisha waafrica wenzao.
ReplyDeleteUnachosema ni kweli kabisa! Mtazamo wangu ni kwamba, hawasimamishi/hawakagui wazungu kwa sababu hizi (1) Wengi wao hawaongei kingereza au wanaogopa kujaribu broken english yao, bila kujua kwamba "practice makes it perfect". (2) Wengi wao wanataka 'kula'.
ReplyDeleteLugha!!!!! hamna kitu!!! wanakazania kuomba hela tu wakati tunasafiri.. wazao huku wanatukomalia sisi na watu wao wanawapa First class service . lakini sisi tunabakia kubanana wenyewe kwa wenyewe... long way to go.... It's a big shame though
ReplyDeletemim sisemi mengi aku....maana yamenikuta hayoo...utadhani wamenyeshwa damu ili watuchukia watu wausi au kuwaogopa zeruzeru.
ReplyDeleteThat's the only way of expressing their frustration. It's the toughest pill to swollow seing people everyday exiting as shoe shiners and coming back as hand shakers to the president.
ReplyDeleteinasikitisha sana . nadhani wanaogopa wazungu # 1. Hutakuta Lugha haipandi, #2. Anajua mmatumbi atatoa chochote mzungu ataoi chochote namwisho ndio shida za nchi zetu za Afrika tumehamini hawa watu wenye ngozi nyeupe(mzungu, mchina Japan mwindi n.k) tunadhani kuwa ni watakatifu lakini hakuna watu wachafu kama hawa biashara zote za haramu wanazijua na ndio wanazifanya
ReplyDeleteMichuzi we wasamehe manake hawajui walitendalo, kwani wangepata nafasi ya kusafiri kwenda huko wa wazungu wenyewe ndo wangejua nini manaana na ku-search..
ReplyDeleteMa Askari wetu hawajui kiingereza ndo mana wanaogopa, kama wanacho ni kile cha kuombea maji ambacho anakuwa hana confidence akiongea. Na Wazungu hasa wa huku marekani kama hajawai kutoka nje ya marekani na hajawai kukakaa sana na watu wenye ancient, anajifanya hakuelewi unachoongea, au inakuwa ngumu kwa wao kukuelewa hasa ukiwa na uwezo kama wa mapolisi wetu lazima kuwe na Communication Barrier hapo.
ReplyDeleteHapo tatizo labda ni kiinglish! wanajiulisha wakiwasimamisha wataongea nao vp wakati lugha haipandi! Lkn sasa hivi kuna askari wengi wasomi, kwa nn hao ndo wasipelekwe Air port ili waweze kukong'oli kiinglish na wadhungu ili haki itendeke?
ReplyDeletehao askari wa hapo eapoti dar ni full vihiyo hakuna kitu hata mswaki hawajui kupiga wana vikwapa vya mdomo, pyuu
ReplyDeleteMbona hii sio mpya mm nilishatukanana na askari pale znz airport tena ujinga zaidi nilikuwa narudi nairobi tu wakataka kuzuia passport yangu na hatimae wakanirudishia baada ya kuwaachia wachukue, hii ndio kawaida yetu , na zaidi ukiwa umevaa jeans, kapelo nk, wataheshumu kidogo ukivaa suti .
ReplyDeleteHili ni donda ndugu halafu tunalalamika wazungu wanatudharaku kumbe imeanza kwa ss kujidharau.
nyie vipi?mbona toka jana comment yangu hamuiweki na so far hakuna comment yeyote iliyowekwa kuhusu ubaguzi jk nyerere intl.airport unaofanywa na vijana wa afande NZOWA,Tunaomba salamu zimfikie afande ili arekebishe hali hiyo la sivyo kitengo chake kitapoteza umaarufu kwa wananchi licha ya kazi nzuri ya afande NZOWA toka ashike kitengo hicho
ReplyDeletewafanya kazi wa airport yetu wananjaa kali sana ! awaoni hata haibu kukuomba zawadi!!! loh watanzania tabia ya kuomba omba mmenza lini
ReplyDelete