Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametoa salamu za rambi rambi na pole kutokana na kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, Bw. Cleophas Angello Rugalabamu kilichotokea mapema leo nchini India ambako alikuwa anatibiwa.
Bw. Rugalabamu (64) alilazwa katika Hospitali ya Appolo mjini Chennai tangu
Juni 20 mwaka huu na alifariki dunia leo alfajiri.
Mipango inafanywa ya kurejesha maiti yake nchini kwa ajili ya mazishi.
Katika salamu zake alizozituma kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Yohana Balele, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Pinda alisema kifo cha Bw. Rugalabamu kimeleta majonzi makubwa.
“Alikuwa kiongozi hodari na muaminifu. Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba
yangu mimi mwenyewe binafsi, natoa rambirambi na pole kwa familia ya
marehemu, ndugu jamaa na marafiki kutokana na msiba huo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,” Waziri Mkuu alisema katika salamu hizo.
Imetolewa na: Ofisi ya Waziri Mkuu
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM
Jumatano Julai 21, 2010
RIP Rugalabamu..pole ziwafikie familia ndugu,jamaa na wakazi wa jiji lote la mwanza.
ReplyDeleteRIP
Buriani Bw. Cleophas Angello Rugalabamu !!! Pole kwa wafiwa wote na namuomba Mwenyezi MUNGU mwingi wa rehema awape nguvu kwa kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kipenzi chenu (Bw. C. A. Rugalabamu). Roho ya Marehemu ipokelewe na ilazwe mahali pema peponi na ipumzike kwa amani. Amina !
ReplyDeleteKweli wema siku zote hawadumu! Ulikuwa kiongozi safi, mchapa kazi hodari, mpenda watu, hukubagua watu wa chini. Tumekupoteza hatuna jinsi. Mapenzi ya Mungu hayana mpinzani.
ReplyDeletePoleni sana wanafamilia.
RIP Mr. Rugalabamu. You will be missed.
ReplyDeleteWe miss you late DC C.A.Rugalabamu
ReplyDelete