Marehemu Cleophas Angello Ruigalabamu

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametoa salamu za rambi rambi na pole kutokana na kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, Bw. Cleophas Angello Rugalabamu kilichotokea mapema leo nchini India ambako alikuwa anatibiwa.

Bw. Rugalabamu (64) alilazwa katika Hospitali ya Appolo mjini Chennai tangu
Juni 20 mwaka huu na alifariki dunia leo alfajiri.

Mipango inafanywa ya kurejesha maiti yake nchini kwa ajili ya mazishi.
Katika salamu zake alizozituma kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Yohana Balele, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Pinda alisema kifo cha Bw. Rugalabamu kimeleta majonzi makubwa.

“Alikuwa kiongozi hodari na muaminifu. Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba
yangu mimi mwenyewe binafsi, natoa rambirambi na pole kwa familia ya
marehemu, ndugu jamaa na marafiki kutokana na msiba huo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,” Waziri Mkuu alisema katika salamu hizo.

Imetolewa na: Ofisi ya Waziri Mkuu
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM
Jumatano Julai 21, 2010


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. RIP Rugalabamu..pole ziwafikie familia ndugu,jamaa na wakazi wa jiji lote la mwanza.


    RIP

    ReplyDelete
  2. Karungula, Deo. L. Esq.July 22, 2010

    Buriani Bw. Cleophas Angello Rugalabamu !!! Pole kwa wafiwa wote na namuomba Mwenyezi MUNGU mwingi wa rehema awape nguvu kwa kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kipenzi chenu (Bw. C. A. Rugalabamu). Roho ya Marehemu ipokelewe na ilazwe mahali pema peponi na ipumzike kwa amani. Amina !

    ReplyDelete
  3. Kweli wema siku zote hawadumu! Ulikuwa kiongozi safi, mchapa kazi hodari, mpenda watu, hukubagua watu wa chini. Tumekupoteza hatuna jinsi. Mapenzi ya Mungu hayana mpinzani.

    Poleni sana wanafamilia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2010

    RIP Mr. Rugalabamu. You will be missed.

    ReplyDelete
  5. We miss you late DC C.A.Rugalabamu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...