Marehemu Profesa
Jwani Timothy Mwaikusa


Habari zinasema Wakili na Mwanasheria nguli na Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. Jwani Timothy Mwaikusa amefariki dunia baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati akirejea nyumbani kwake maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam.

Prof. Mwaikusa pia alifanya kazi katika mahakama ya kimataifa ya I.C.T.R Arusha na alikua rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowasilisha kuhusu mgombea binafsi.

Kwa wale waliosoma literature A- Level kama mimi, Prof. Mwaikusa pia alikua mwandishi mzuri wa poems ambazo wengi wetu tulizijibia mitihani.
Pamoja nae pia ameuwawa mwanae aliyekua akitoka nje kumfungulia geti, na mtu baki aliyekua akipita njia.

Kwa jicho la kawaida tu, haya yatakua mauaji ya kisasi au ya kumnyamazisha kuhusu jambo fulani kwakua habari za awali zinasema wauwaji hao hawakuiba kitu chochoteSee More

Na Mdau Nkundwe Mwakilema
NILIYOYAFAHAMU:
Career:
* Professor of Law, Faculty of Law, University of Dar es Salaam 1999
* Mkono & Co Advocates since 1998
* Advocate, High Court of Tanzania since 1988
* Managing Editor of the Tanzania Law Reports.
Qualifications:
* Ph.D., School of Oriental & African Studies, University of London, UK, 1995
* LL.M, University of Birmingham, UK, 1985
* LL.B (Hons), University of Dar es Salaam, Tanzania, 1981.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 54 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2010

    This is a clear work of an assassin!

    Mungu iokoe nchi yetu na mambo ya jinsi hii.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2010

    wamefaidi nini wauaji? kisasi gani hadi kwa mtoto na mpita njia? habari hizi zimenishtua sana. The world is not fair siku zote. na wao siku zao zitafika watakufa tu. Jamani tumepoteza mtu muhimu sana Tanzania. Tunaomba vyombo husika vifanye kazi za ziada kuwapata wahusika. sijui tutaishi wapi kwakweli. RIP Prof. You were a great lecturer UDSM. I realy remember your times

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2010

    aluta kontinua!!!
    hawawezi kuua mawazo na fikra zako.
    ulishafyatua vifaa kibao.
    tutakuenzi kwa kuliendeleza libeneke la kutetea haki na demokrasia.
    RIP Prof!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2010

    Dah!!! R.I.P Prof,Amu ,Baraka na familia yote kwa ujumla poleni sana

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2010

    IT IS MORE THAN SAD. I DONT EVEN WANT TO IMAGINE, THAT THE GURU IN LAW, MY ROLE MODEL ON ADMINISTRATIVE LAW, CONSTITUTIONAL LAW, IS NO MORE, THAT HIS HUMBLE VOICE AT YOMBO CLASSES I & II, NKURUMAH HALL, NYERERE THEATERS, SEMINAR ROOMS WILL NO BE HEARD AGAIN! OOH GOD! WHAT IS THIS? HOW? WHY JUAN T. MWAIKUSA? SINCERELY, HE WAS A GRACE THAT PLACED ITSELF.

    ReplyDelete
  6. So sad!!Mungu amlaze pema peponi. I remember tukiwa UDSM 2000 alitufundisha ADMIN LAW. He was good!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2010

    Inaonyesha kuna siri kali sana mpaka kufanya hivyo ili kupoteza ushahidi kabisa, hao watakuwa watu wake wa karibu sana au watu wenye wadhifa sana.Umafia huu utaisha lini??Uchunguzi utagundua mengi!! anzeni na kazini kwake.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2010

    Poleni sana wanafamilia!Mama Mwaikusa Baraka,Msa, Amu, Adolf na wengine. Tupo pamoja katika kipindi hiki kgumu. yan wa2 Tz wanaishi knyama sana sasa kumuua baba wa wa2 wamefaidika nini?? RIP Prof Jwani Mwaikusa.2takukumbuka daima. AMEN

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2010

    OMG RIP Prof am speechless na hii nchi ,Watanzania tusali na kuomba malipo ni hapa hapa duniani

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2010

    HII NI HASARA KUBWA KWA JAMII YA WANASHERIA NA NCHI YA TANZANIA KWA UJUMLA.

    KWA HALI YEYOTE ILE HILI JAMBO HALIKUBALIKI. HUYU PROF AMEFANYA NINI KIKUBWA HAPA AUWE YEYE NA MWANAYE?

    HIKI NI KITENDO KIBAYA SANA AMBACHO HAKISITAHILI KUFUMBIWA MACHO. NI MATUMAINI YAKE KUWA WALIOHUSIKA WATATAFUTWA NA KUCHUKULIWA HATUA KALI SANA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2010

    too bad,unyama wa aina hii utaisha lini?mzee wa watu wamemkatili vibaya,je wao wataishi milele?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 14, 2010

    Nimesikitika sana.Hata sijui nianze kuelezea vipi hisia zangu.Alikuwa mwalimu mahiri wa Administrative Law wote waliopita Faculty of law Mlimani wanajua hili.Mungu amlaze mahali pema peponi.
    Lakini pia nataka niseme kuhusu mauaji haya.Hatimaye sisi wote ni wanaadamu kwa hiyo hata hao waliomuua kwa kutumwa au kwa sababu nyingine yoyote mwisho wa siku ile hali ya kuwa nao walipewa maisha kama alivyopewa Prof Mwaikusa itadhihiri maana nao watakufa.Mwenyezi Mungu ametujaalia kifo kuwa kama malaika mlinzi wetu hakitakuja kama muda wake haujafika na hakitachelewa muda wake ukifika.Kwa heri profesa nasi pia tunakuja.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 14, 2010

    poleni sana Baraka msafiri Amu na dolph kwa kufiwa na baba yenu pamoja na mama yenu! MAY HE REST IN PEACE

    wadau wa chuo kikuu..

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 14, 2010

    Ndo mnasema hii serikkali ndo ya haki wakati tunaondokewa na watu muhimu namna hiyi.
    ok,kama mantiki yenyewe ndo hiyo kwanin waue na mtoto wake,ambaye alikuwa ametoka kumlaki baba yake.na sio hivyo tu,hata mpita njia?

    HIVI VYOMBO VYA SERIKALI KWANINI VINATUMIKA KTK UHAINI NA UGAIDI WAHALI YA JUU.

    Nakuambia damu itamwagika hapa.waliofanya mauaji washajulikana na watakiona cha moto.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 14, 2010

    Marehemu wapumzike kwa amani. Wamekufa vifo vibaya sana. Pole kwa familia.

    Prof. Mwaikusa nakumbuka alitufundisha Local Governments Law, Administrative Law kidogo, na Constitutional Law kidogo.

    Prima facie, alikiwa anaonekana kama mtu asiekuwa na maneno na mtu, ndio maana nashangaa hasa kulikoni mpaka watu wafikie maamuzi ya kumuua?

    Ni adversaries wake katika kesi ambayo hiyo kesi Marehemu Prof. Mwaikusa alishinda au alikuwa anaelekea kushinda, ama vipi? Au kuna deal alilipata ambalo hilo deal kuna watu wengine walikuwa wanalitaka, ama vipi? Ama ndio alikuwa ana information nyeti ambazo zingeweza kuwamaliza watu fulani fulani, ndio wakaamua wajihami?

    Inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 14, 2010

    Kuua kichwa kama hiki ni kupoteza rasilimali kubwa ya taifa,JARIBU KURE-CALL ALIVYOISHAURI MAHAKAMA KUHUSU MGOMBEA BINAFSI..HAKUMUNG'UNYA MANEO KAMA YULE MWENZAKE.Wanafunzi wake wengi wameumia sana,a peace man,kichwa na mkweli! Kama wamemuua kulipiza kisasi,na wao yatawakuta,malipo humuhumu duniani..RIP Prof..Pole familia,UDSM na watanzania kwa ujumla.
    Mdau -UDSM

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 14, 2010

    Poleni wafiwa. Tanzania sasa ilipofikia inabidi kuwa na exclusive 'gated areas'(yaani wilaya nzima izungushwe ukuta kama wa Gaza, kuingia unaahojiwa na G4S n.k) kama za huko USA, South Africa n.k ili kujichunga na majambazi.
    Mdau
    Johannesburg.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 14, 2010

    Soma shairi la Prof. hapa... changamoto jamani:

    http://vijana.fm/2010/07/14/watanzania-tunaomboleza/

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 14, 2010

    Jamaa mmoja alifuatwa mafichoni South Africa wakampiga risasi kisa siasa. (KULA).

    Sasa mgombea binafsi haina link na hichi kifo kibaya kabisa?
    Siasa chafu na haki kukataliwa!

    This is really bad, turudi bongo? he? ili? duh!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 14, 2010

    Correction: aliyeuwawa sie mwanae ni binamu yake alikuwa akiishi nae na mwingine ni jirani yake

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 14, 2010

    HII NI MAUAJI YA WATU WABINAFSI WANAOICHUKULIA TANZANIA NI MALI YAO. INANIKUMBUSHA KIFO CHA KOMBE NA BALALI.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 14, 2010

    Very very sad. Nilikuwa simfahamu Prof. lakini hili tukio limenigusa sana jinsi nchi yetu inapoelekea. Kwa wale tuliopo nje ya nchi na tunategemea kurudi nyumbani karibuni haya sio maisha ambayo tungependa kuyasikia. Serikali imekuwa ikihamasisha kupeleka wawekezaji nyumbani na kuwaambia kuna usalama. Sijui kama hao wawekezaji ambao wanatoka kwenye nchi zenye "freedom of speech" wakisikia matukio ya namna hii itakuwaje ila kwa upande wangu ni hali ambayo haipendezi. Vitendo kama hivi vinatakiwa vimekomeshwe. RIP Prof.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 14, 2010

    JAMBO MOJA NI VYOMBO HUSIKA VIONYESHE KUWA VINA MKONO WA KUTOSHA.NINAFIKIRIA ISSUE ILIYOTOKEA HAPA UINGEREZA JUZI YA KUMSAKA MUUAJI MMOJA TU JESHI LA POLISI LILIKUWA KAMA LIKO VITANI NA MAGAIDI HATARI. SASA ILI KUTOENDEKEZA HAYO MAOVU KUJIRUDIA LAZIMA POLISI HAO WA KWETU WATUONYESHE KAZI YA ZIADA WATUKABIDHI MUUAJI.JESHI HAPA LILIAPA KUWA WASINGEACHA HATA JIWE MOJA BILA KULIGEUZA NA KWELI SIKU CHACHE WAKAMNASA.WATANZANIA TUNAWEZA.JESHI LA POLISI LIHAKIKISHE LINATUPATIA HAO WATU.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 14, 2010

    R.I.P profesa Mwaikusa,japo omendoshwa duniani kinyama fikra zako bado zitaishi

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 14, 2010

    OMG..This is really unbelievable...
    Yani of all the people Prof. Mwaikusa wa watu jamani?

    How sad and shocking..tena kuuwawa kikatili namna hii jamani??where is our country heading to?

    You will always live in our minds..u were one of the greatest...ulitufunza vema sana Admin Law pale UDSM mwaka 2007.
    My condolenses to the family...poleni sana.

    Naomba vyombo husika vifanye kazi yake haraka na wenye kuhusika wafikishwe kunakostahili.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 14, 2010

    IMENIUMA SAANA NASHINDWA HATA KUULEZEA.MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI AMINA

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 14, 2010

    Jamani bongo sasa tunakwenda wapi?mtu asijaribu kuishi maisha yake, tayari mnammaliza, inabidi vyombo vya sheria vipambe moto kukomesha uarifu kama huu.pole kwa familia yote kwa kifo cha ghafla.polisi na nyinyi amkeni na muache kuwaza hongo na mfanye kazi.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 14, 2010

    Lo pole sana wafiwa na ndugu wa Prof. Mwaikusa.
    Tuliingia wote pale UDSM 1978

    Jambo la kututia moyo ni kwamba hawa wauaji hawataishi zaidi ya miaka 50 ijayo, muda mchache sana ujao.
    Na watamkuta Prof katka chemba ileile kabla ya hukumu yao kutoka kwa Mwokozi wetu.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 14, 2010

    Tupo Zimbabwe au Tanzania? Tusubiri tuone kama polisi watafanya kazi yao, tusubiri tuone kama mahakama itafanya kazi yao? Tusubiri tuone watu wa haki za bianadamu tanzania watsemaje?tusubiri tuone kama kura yako ya mwaka huu itafanya kazi. Pole sana kwa hiyo familia na vijana wote ambao mungu alipanga wangenufaika na huyo mwl. Na badala yake wataishia mitaani kama unavyoona jiji limejaa matapeli.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 14, 2010

    I didn't know him but nimeumia sana
    R.I.P prof Mwaikusa

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 14, 2010

    Anoni 02:10:00 uansema waliofanya mauaji washajulikana na watakiona cha moto. Tudokezee nasi kwani tuna haja ya kuunganisha nguvu katika kufanya mambo ya hasira kali. Usichelewe jazba zitakwisha.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 14, 2010

    RIP John Mwaikusa. Ni masikitiko makubwa sana kuuawa namna hii. Nilikufahamu nilipokuwa mdogo pale st Peter Claver Seminary. Ulitutetea sana wannyonge. Kumbe ilikuwa matayarisho yakuwa mwanasheria baadaye.
    Poleni wanafamilia Mungu awape nguvu ya uvumilivu kwa wakati huu mgumu

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 14, 2010

    RIP Prof .Mwaikusa,kweli watu ni wabaya kitu gani,basi naserikali iwajibike kusaka wauwaji hawa-Amen

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 14, 2010

    nimetoka hapo sasa hivi, kwa kweli nimesikitishwa sana,

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 14, 2010

    RIP Profesa Mwaikusa
    Kama clasrep wa darasa la sheria lililomaliza 2008 UDSM

    nakuombea ufike salama kwa baba Mbinguni. Kapumzike, shetani kaifunua mikucha yake lakini hatumuogopi kwani Yesu alishamshinda.

    Jamani tuhuzunike lakini tuwe na matumaini kwamba hapa si nyumbani basi tumuombe Mungu kadiri ya imani zetu tujiandae na safari.

    Aliyoyafanya ya kutetea wanyonge ni mengi na hii inathibitishwa na kifo chake kwani angekuwa anatetea wabaya, basi wasingemuua mbaya mwenzao. Poleni wanafamilia, Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe Milele.

    Madam President Yombo 2

    Sweden

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 14, 2010

    THIS IS TRUE THAT, THERE IS NO PEACE AT HOME,THERE IS NO SECURITY AT HOME, THERE IS NO WHERE TO GO AT HOME, THERE IS DEMOCRACY AT HOME, THERE IS NO LAW AT HOME, THERE NO FREEDDOM AT HOME, THERE IS NO HAPPY AT HOME, THERE IS NO HOME AT HOME, THERE IS NO TRUTH AT HOME, THERE IS NO FAMILY AT HOME. ONLY I SEE IS BLOOD. WHAT A SHAME. MANY DEATH LIKE THIS HAPPEN IN THE PASS. WE'RE REALLY SCARED.

    R.I.P PRO.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 14, 2010

    Sasa hii MIJITU/JITU lililofanya mauaji linafkir halitokufa(litaishi milele)??????????????????????

    Kwa upande mwingne PROF alikuwa m2 muhimu tena sana japo hajawah kunifundisha but wadhifa wake unajieleza. Cdhan kama atatokea m2 kama yeye kuliziba pengo hili.
    POLEN SANA WAFIWA
    POLENI wana UDSM.

    Mdau-ALGERIA

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 14, 2010

    HII INAKUWAJE MAANA ADVOCATE MWINGINE WA MKONO & COMPANY ADVOCATE PIA ALIUAWA 2007 NINGEPENDA KUJUA MAELEZO KWA KINA INAKUWAJE HAPA WOTE NI MAPROFESA WA SHERIA KWENYE KAMPUNI MOJA WANAUAWA?

    ReplyDelete
  39. AnonymousJuly 14, 2010

    we used to call prof "kichwa cha kampuni"....akipewa kesi tulikuwa tunajua anashinda!
    MUNGU akulaze pahali pema prof. sasa ni muda wa serikali kuacha kukaa kimya tunauwawa maeneo ya kimara na mbezi...siku hizi tunalala mpaka guest kuyakwepa. Ile kasi ya Kikwete iko wapi????SHAME!!!.....

    ReplyDelete
  40. NyakarunguJuly 14, 2010

    RIP Prof.
    Hakika uchache wa maandishi yangu hapa ni wingi wa huzuni niliyonayo tokana na unyama huu uliofanywa wa kumwondoa Msomi Mbobeaji huyu miongoni mwa jamii yetu.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 15, 2010

    Kwa sisi tunaofuatilia matukio ya Rwanda lazima tujiulize, baada ya wapinzani wa Kagame kuuliwa Kenya, Malawi na jaribio lililofeli Afrika Kusini, na baada ya kusikia BBC na CNN kuwa kuna wakili MMarekani aliyefanya kazi na Prof Mwakusya amekamatwa na kutiwa ndani Rwanda, je hiki kitendo ni ujambazi au jaribio lingine la kuwzima watu ambao wanaonekana kuwa wanawatetea Wahutu? J.M. (Mha wa Ngara)

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 15, 2010

    Kwa sisi tunaofuatilia matukio ya Rwanda lazima tujiulize, baada ya wapinzani wa Kagame kuuliwa Kenya, Malawi na jaribio lililofeli Afrika Kusini, na baada ya kusikia BBC na CNN kuwa kuna wakili MMarekani aliyefanya kazi na Prof Mwakusya amekamatwa na kutiwa ndani Rwanda, je hiki kitendo ni ujambazi au jaribio lingine la kuwzima watu ambao wanaonekana kuwa wanawatetea Wahutu? J.M. (Mha wa Ngara)

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 15, 2010

    nasikia alikuwa wakili wa mhutu huko mahakama ya rwanda...

    ReplyDelete
  44. R.I.P Prof
    Inasikitisha mauaji kama haya yanapotokea,naomba uchunguzi ufanyike kimakini maana hamna kitakachojificha na kisionekane milele.
    Pole familia ya marehemu,ndungu,majirani bila kusahau wanachuo wote na wahitumimu waote wa chuo hicho.

    E.Motto
    Toka Moscow Russia

    ReplyDelete
  45. AnonymousJuly 15, 2010

    tatizo tanzania hao wauaji hawatopatikana au wakipatikana watalisha wakutwe hawana makosa au wakikutikana nayo makosa basi watalisha watoroshwe jela. sijui tutafika lini kwa kweli. mimi lakini mbona nimesikia ni watu wawili wamefariki. prof na mjomba wake ambaye alikua na umri mdogo kama miaka ishirini na kitu sasa sijui hadithi ipi ya ukweli. prof alikua ni mtu mpole mwenye ukarimu na asiye na matatizo na watu hivyo ukatili aliofanyiwa hauingii akilini kabisa. mungu amlaze mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 15, 2010

    Hichi kofo kimetusikitisha wengi, bado siamini. Ameacha pengo kubwa, sijui kama kitapata wa kuliziba na makala hii inajaribu kutoa changamoto kwa sisi vijana http://vijana.fm/2010/07/14/watanzania-tunaomboleza/

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 15, 2010

    ANNON HAPO JUU... hakuna aliyekufa mkono & co kwa kuuawa zaidi ya huyu Prof. wengine waliokufa walikuwa ni Prof Gondwe na Mr Mukami kwa ugonjwa. maybe unaye msema wewe ni Kapinga hakuwahi kufanya kazi Mkono na alikuwa lawyer wa Mkapa> Mkono bado wanae Dr.W B Kapinga. Tofauti na yule kapinga aliyeuwawa na hse boy wake ingawa ni ndg. Bado nauliza kasi ya kikwete iko wapi? ridhiwani kama unasoma hapa mwambie baba wakati nyie mnajifunika mashuka mnalala usingizi mtamu. kuna wengine tunaoomba usiku usiingie! naomba baba asilale apeleke hata JKT kutulinda.naogopa ninaposikia baba yako anasema kasi zaidi wakati hata kasi mpya haijafanikiwa. Kama anataka kubaki na pumba bungeni aache wanainchi wenye moyo wanaoweza kujenga nchi wauwawe.
    RIP Prof. KICHWA CHA SHERIA.

    ReplyDelete
  48. AnonymousJuly 15, 2010

    We have just lost a distinguished academic person who can never be replaced. I truly feel sorry for the diseased and the family as well. So far I believe this professor wasn’t, at present, an inner circle figure in current government, but I also believe he might, to a certain stage, in the past three country’s leadership phases been one amongst the inner circle. So he strategically knew a lot about the past and even the current GVT affairs. To my understanding “the system" is the system and constantly works from inner circle to outer circles, but it is not often that those who are in outer circles are well informed on high profile issues. They say to be a member in an inner circle you have to make choices and some options may even cost your own family or yourself. And although we don't know the low down to what happened which draw up his death, there is a high degree of apprehensive in the manners in which these killings have been exercised. Has he been Kolimbage? Has he been Kombage? Has he been Bilaliage? Has he been Rutihindage? All these questions need answers. To me this typifies mesons work in Mafias chapter if you like, but all carried out in what we call a peaceful Tanzania. We should not let this happen even in the sake of “the system”. The truth will immaculate no matter what. My theory is there is no secret when an issue, which termed to be secret, is ultimately shared by two groups/ people. However, whilst searching for the truth, I would suggest members of his family to ensure that they protect themselves or seek refugee somewhere safe.

    ReplyDelete
  49. AnonymousJuly 15, 2010

    Ni habari ya kuhuzunisha Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema. Issue who is next leo kwa prof.hawajapata kitu lazima waendelee kuua raia wema Nafikiri ni kipindi muhimu kwa jeshi la wananchi na JKT kuchukua ukanda hasa yale maeneo korofi polisi wameshindwa kazi. Tunataka Serikali ije kwenye msibani wasitueleze marehemu alikuwa mtu mzuri waeleze wanamkakati gani wa kukomesha vitendo hivi. isije ikawa wapo bussy na uchaguzi

    ReplyDelete
  50. AnonymousJuly 15, 2010

    hii yote sababu itakwua ile kesi ya ICTR tu! wale wahutu aliokuwa anawatetea ile side ya pili nina uhakika wamehusika. Wawabane wale jamani
    RIP prof

    ReplyDelete
  51. AnonymousJuly 15, 2010

    utasikia TZ tuna AMAN tuilinde aman yetu asa kunatofauti gani na palestina au burundi!!!hv mnadhan kwa nini watu palestina wanajitolea muhanga!!!ni kwa mambo hayohayo!!!unadhan mwanae akifikiria mauaji ya baba yake na ndugu yake lazima itamfanya awe na roho ya ajabu na anaweza fanya tukio lolote!km halijakukuta utaona km wapalestina majuha vile!!!hebu fikiria uko kwenu mnavamiwa then unashuhudia mama yako,baba yako na ndugu wengine wanachinjwa km mbuzi wewe kwa bahati unanusurika lkn unamjeraha kibao unadhan itakuwaje kila ukikumbuka!!!TAFAKARI

    ReplyDelete
  52. AnonymousJuly 15, 2010

    Kwa kweli tumehuzunika sana, POLE KWA FAMILIA YA ya Late Prof. Mwaikusa. RIP, We will remember you all the time.
    WAUWAJI TUNAWAOMBA BASI MUWE NA ROHO ZA KIBINADAMU MAANA NANYINYI NI BINADAMU. MMEFAIDIKA NA NINI....????
    TUNAELEKEA WAPI ?
    KWA UWEZO WA MUNGU AWASHUSHIE ADHABU....!

    ReplyDelete
  53. AnonymousJuly 15, 2010

    HIVI TUNAPOSEMA TANZANIA KUNA AMANI HUWA TUNA MAANISHA NINI? NAOMBA WATANZANIA MNISAIDIE. HIKI KIFO KIMEPANGWA NA WATU WALIOZOEA KUTUKANDAMIZA WATANZANIA ILI WAENDELEE KULA NCHI HII BILA KUVIGUSA VITI WALIVYO KALIA NAICHUKIA SANA HII ROHO

    ReplyDelete
  54. AnonymousJuly 15, 2010

    JAMANI MIMI NAFIKIRI SASA TUNAHITAJI KURUDISHA ULINZI WA SUNGU SUNGU KAMA ULIVYOTUSAIDIA HAPO NYUMA. KWA KUFANYA HIVI ITAKUWA RAHISI SANA HATA KUMJUA JIRANI WA KWELI NI YUPI, HAIWEZEKANI HAWA WATU WAKAPITA MAENEO HAYA USIKU BILA MAJIRANI KUSHTUKA KUONA SURA MPYA MAENEO YAO. MREMA JAMANI UPO WAPI UWASAIDIE HAWA MAPOLISI NA TUKO TAYARI TUKULIPE MSHAHARA KWA HILO. POLENI WAFIWA KWA KIFO CHA KUSIKITISHA NA CHA GHAFLA. BONGO INAKWENDA KUBAYA EVERYDAY NDUGU ZANGU, TUSAIDIANE KIKAMILIFU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...