*AWAPONGEZA MBOWE NA DR SLAA
*AAHIDI KUCHANGIA ZAIDI
Mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, Mustapha Jaffar Sabodo amekichangia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA shilingi milioni mia moja ili kuimarisha upinzani na demokrasia nchini.
Bw. Sabodo amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha leo jijini Dar kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe aliyeambatana na Katibu Mkuu wake Dr Wilibrod Slaa na Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho Bw. Antony Komu.
Akikabidhi hundi hiyo Bw. Sabodo amesema pamoja na kwamba yeye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi lakini anapenda kuona upinzani na demokrasia vinaimarika nchini huku akikitaja CHADEMA kuwa ni chama makini na safi cha upinzani.
Bw. Sabodo amekuwa mmoja wa wazee walio wazi katika kukosoa utendaji wa serikali ya chama chake CCM hasa inapokiuka misingi ya utawala bora iliyojengwa na Mwasisi wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.
“Mimi ni mwanachama wa CCM lakini napenda kuona demokrasia ikikua huku kambi ya upinzani ikiimarika kwa kuwa na wabunge wengi bungeni ili kushamirisha maendeleo nchini……na nawachangia CHADEMA kwa kuwa natambua umakini wenu katika siasa za hapa nchini na hasa Bungeni”, Alisema.
Bw. Sabodo amesema kuongezeka kwa wabunge wa upinzani bungeni ni jambo la muhimu katika kutoa upinzani kwa CCM na kusukuma maendeleo ya wananchi huku akikitaka CHADEMA kuongeza nguvu zaidi katika harakati zake za kisiasa na kumwelezea Dr Slaa kuwa ni mwanasiasa mwenye uchungu wa kweli na watanzania.
Aidha Bw. Sabodo amesema ana mpango wa kuichangia fedha zaidi CHADEMA ili kuimarisha harakati zake za kisiasa na kuahidi kufanya hivyo atakaporejea nchini akitokea India kwenye matibabu.
Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Bw. Sabodo Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameshukuru na kutaja msaada huo kuwa ni wa kihistoria katika siasa za vyama vingi nchini.
Amesema mara nyingi imekuwa ni vigumu kwa wafanyabiashara wakubwa wa kada ya Bw. Sabodo kuchangia kwa uwazi tena kiasi kikubwa cha fedha na kutaka hatua hiyo kuigwa na wafanyabiashara wengine nchini.
“Kwa kweli tunashukuru sana hii ni historia mpya katika siasa za vyama vingi nchini, ni wajibu wa wafanyabiashara wakubwa kuona umuhimu wa kusaidia vyama vyote makini nchini bili kuwa na ubaguzi wala woga, Mzee ameonyesha njia naamini itakuwa ni mfano kwa wengine wenye uwezo, Alisema Bw. Mbowe.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Dr Slaa ameshukuru kwa mchango huo na kudokeza kwamba mchango utatumika kwa kadiri ya vipaumbele vitakavyopangwa kwenye Kamati Kuu ya chama inayotarajiwa kufanyika tarehe 20 Julai 2010 ikilenga zaidi katika kutekeleza mipango endelevu ya kuimarisha chama kama Operesheni Sangara na utekelezaji wa mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
“Nawaomba watanzania wengine wa kada na uwezo mbalimbali kuichangia CHADEMA ili kuondokana na ukiritimba wa chama kimoja kwani ni hatari kwa maendeleo na usalama wa nchi kama michango yote ikielekezwa kwa chama tawala pekee.
"Natoa mwito kwa vyombo vya dola kuacha kuwatisha watanzania wenye mapenzi mema wanaochangia vyama mbadala kama CHADEMA kwani kufanya hivyo ni kuhujumu taifa na kukwamisha maendeleo ya nchi”, alisema
Imetolewa tarehe 12 Julai na:
Erasto Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Wakati watu wakibadilishana hela kama hizi, hebu tuwakumbuke watu kama hawa:
ReplyDeletehttp://vijana.fm/2010/07/11/kibera-slum-survivors/
Jioni njema!
Huyu Sabodo anaijua CCM au anaisikia? Na hivi kaamua kujitangaza kwenye vyombo vya habari, imekula kwake. Wenzake huwa wanachangia vyama vya upinzani kwa siri. Yeye anaanika hadharani hivi. Ataona kama hawajamfilisi hawa magaidi wa CCM.
ReplyDeleteyale yale,mshkaj wa karibu wa jetuu patel amekuwa mdhamini wa chadema,eti mimi ccm lakin i napenda wapinzani,njaa hizo chadema na mnaaibisha upinzani.ama kweli chama pekee tz cha upinzani ni cuf.
ReplyDeleteeti nini,nchi imeisha hii,ccm wanaidhamini chadema,now ndo naelewa kwa nini chadema kila mmoja hataki kugombea urais.
ReplyDeletealianza mrema juzi kusifia,leo chadema wanasaiddiwa na mdhamini wa ccm.duh,kwa hiyo wamebaki cuf na nccr mageuzi.mtikila alishakopa siku nyingi kwa rostam aziz na hajalipa hadi leo.kazi kweli kweli
ReplyDeletesafiii! ila CCM chonde chonde msianze kumhujumu baba wa watu Demokrasia maana yake pia Upinzani wenye nguvu wenye kushindana nanyi katika uwiano sawa! kifwedha
ReplyDeleteukiienda jamii forum now lazima watakuwa wanamsifia jamaa ni mfanyabiashara safi.na masifa kibao kumpa.wapinzani wanatafuta kula na wakuna kingine.
ReplyDeletealafu hapo si kwa sabodo.duh jamaa wameenda ofisini wenyewe.cheki slaa anavyocheki.hahahaha
ReplyDeleteHongera SABODO kuchangia CHADEMA..na wengine wajitokeze...Upinzani unahitajika kuimarika nchini...
ReplyDeleteDah hii safi sana...nina mpongeza sana Mzee Jaffer Sabodo kwa mchango wake kwa Chadema kwani hakuna upinzani kuwa Chadema ndio chama mbadala wa CCM. Kwa muda wa miaka takriban 10 hivi Chadema imeonesha kuwa chama makini na chenye mikakati maridhawa yenye kupigania kiukweli maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa watanzania wote. Nina waombeni WaTZ wenzangu tutoe support ya nguvu kwa Chadema ili kiweze kuleta upinzani wa kweli kwa CCM na tuachane na manungayembe akina TLP, UDP na vingine vya aina hiyo! CUF itaweza kututoa kimasomaso Zanzibar na Chadema bara then ipo siku Inshallah vitakuja kuungana na kuimarisha nguvu bara na visiwani! Hongera Mzee Sabodo na nina hakika watu makini akina Mbowe, Slaa, Zitto etc watazitumia vizuri fedha hizi kufanikisha malengo! Niko na furaha sana...and this is A MILE STONE TO TANZANIA.
ReplyDeleteLETS SEE IN FEW WEEKS TO COME,TRA WILL BE CRACKING DOWN AS THERE HAS NEVER BEEN BEFORE ON THIS GENTLE MAN.THE GOV. UNDER CCM WILL NEVER LET IT LOOSE,THEY WILL JUST DO ANYTHING TO AMBARASS THE MAN EVEN IF HE HAS DONE NOTHING WRONG AND THATS WHAT WE CALL DICTATORSHIP REGEME,LETS PEOPLE PRACTICE POLITICS WITH NO THREATS WHATSOEVER,THIS IS A GOOD BEGINNING,WE NEED A STRONG OPPOSITION PARTY IN TANZANIA THAT WILL REALLY CHALLENGE THE RULLING PARTY,THIS WILL BE THE ONLY WAY TO BRING AND HOLD ACCOUNTABLE FOR ALL WHO ABUSES POWER,STILL TAX PAYER'S MONEY AND ALL THAT.BUT IF CCM WILL CONTINUE TO REIGN THEN FORGET ABOUT ANYTHING GOOD TO COME IN NEAR FUTURE.WELL DONE SABODO
ReplyDeleteHongereni CHADEMA na Hongera Bw Sabodo. TUnawaomba na akina Manji zile wanakwiba kutoka NSSF warudishie watanzania kwa njia hiyo.
ReplyDeleteDemokrasia ya vyama vingi ina faida kubwa kwa taifa. Watanzania wengi bado hawaelewi maana ya demokrasia kutokana na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na chama tawala na wakereketwa wake. Nilisikia huko kwenye mkutano mkuu wapinzani wakiimbwa kwenye nyimbo kama maadui au watu wenye kasoro. Hii inaonyesha kuwa uwezo wetu wa kiakili bado mdogo sana. Kwa kuwa anayefahamu umuhimu wa "checks and balances" hawezi kufanya utumbo wa namna hiyo.
ReplyDeleteTunahitaji vyama mbadala vyenye nguvu kwa manufaa yetu sote. well done Mr. Sabodo
asante sana kwa kuweza kusaidia chama changu ninachokipenda kwa roho yote!!
ReplyDeletemdau krogs
Big Up Mzee Sabodo. Hakika wewe umefungua njia dhidi ya siasa za kutishana kuwa ukichangia upinzani biashara zako zitafilisiwa.
ReplyDeleteWatu majasiri kama wewe ndio wanatakiwa kuipeleka Tanzania mbele.
Hongera Bw Sabodo kwa kuonyesha njia. Huu ndio uzalendo wa kweli usiokuwa na woga wala unafiki.
ReplyDeleteYeye ni CCM lakini anapenda Demokrasia ya kweli hivyo anachangia Chadema...I mean this is so beautiful.
Sasa CCM usijemletetea longo longo kama mlivyofanya Bakhresa 1995 alipowachangia CUF.
Kwa wasiowahi kumsikia Sabodo, miaka michache ya nyuma alitoa USD Mil 1 = Bil 1 kwa Nyerere Foundation.
Hongera sana CHadema.
Huyu Bw.Sabodo ajiandae biashara zake zote kufilisiwa.
ReplyDeleteTRA, PCCB, Usalama wa Taifa, Traffic Police wote wataelekezwa kumfanyia kazi ipasavyo.
Ni watu wachache sana Tanzania wanaweza kuwa na moyo kama huyu mzee.Mungu akubariki uishi maisha marefu
ReplyDeleteNinachojiuliza hivi kwanini? Uongozi wa juu wa Chadema ni wachaga watupu! Kulikoni,Komu !Mchaga,Dr.Silaha ! Mbowe ni mchaga! kulikoni kwanini? hakuna mseto
ReplyDeleteHengera na hivi ndio inavyotakiwa sio vyama kuenda kupeleka mabakuli yao na kuomba watu wasio hata na kijisenti kuchangia...
ReplyDeleteNdio mwanzo na Mungu yupo tutafika tu....
SIJAWAHI KUSIKIA UJINGA KAMA HUU!!!
ReplyDelete" Mimi ni CCM lakini...." mpaka kafikia kuchangia chama kingine si atoke huko CCM?
....Afu watu humu wanaocomment kwa kuangalia udini na ukabila mnaboa sana yaaani aah....
ReplyDeleteufinyu tu wa firkra,anyways tutafika tu taratibu taratibu ndo uhuru wa kujiexpress huo.
Wewe mtoa maoni unayezungumzia ukabila una shida gani?.Hili jambo la kutazama ukabila wa mtu badala ya matendo ya mtu ndilo linarudisha maendeleo ya watanzania nyuma.Kuna haja gani ya kuwa na mchanganyiko wa makabila kama watu wenyewe ni kama wewe wenye mawazo mazee chakavu na mgando? Ni vyema kuangalia Chadema inafanya nini, kuliko kuangalia ni mkabila gani yuko Chadema. Saboda sio mchagga, amechangia kwa kuona wanachokifanya. Ni ukweli usiopingika kuwa Chadema na vyama vingine vya upinzani vimebadilisha utendaji wa CCM, kubali usikubali,na hilo ndilo tunalolitaka, awe mchagga, au mkwere au mzaramo hilo sio jambo la kujadili hapa kwenye mtandao wa watu wenye akili. Lakini kwa kuwa akili yako imezikwa kwenye fikra finyu, na elimu ya kukariri, isiyohangaika kujifunza vitu mbadala ila status quo na yale uliyofundishwa shuleni zamani basi unaacha hoja za msingi unarukia hoja uchwara za ukabili na udini. Hivi maoni yako hayo yamesaidia nini katika hoja ya msingi? na kuonyesha ulivyo wa hovyo unakosea hata jina la Dr Slaa kwa kumuita Silaha!! Hayo mambo ya ukabila hayapo tena TZ, Mwalimu Nyerere aliukomesha ukabila, kama bado wewe unauhubiri basi lazima una shida katika akili yako. Kama unataka kujua kweli maana ya ukabila nenda nchi jirani, ndio utajua joto la ukabili. Kwa kukusaidia tu Dr Slaa na sio Silaha sio mchagga, na haoni tabu kufanya kazi ya kulikomboa taifa hili na hao unaowaita wachagga. Badili fikra zako,nchi nyingi zimeendelea kwa kuwa na checks and balances kwenye political systems. Auditor (mkaguzi) ya siasa ni kuwepo kwa upinzani imara. Kama vishirika vidogo tu vinahitaji audit kwa mujibu wa sheria, je si zaidi kwa mfumo wa utawala na siasa unaohusu maisha yetu ya kila siku. Kama hakuna upinzani imara na wa kweli, nani atakosoa utendaji wa serekali iliyopo madarakani. Si watafanya wapendavyo. Kwa mfano, kuna mtanzania gani anayefurahia kuuzwa kwa nyumba za serekali kulikofanywa na awamu ya serekali iliyopita? lakini si waliziuza na wakapeana wenyewe wakazikarabati na sasa wamezipangisha na wanakula madola ya kutosha ya kodi?. Je kama upinzani imara ungekuwepo unadhani serekali ingethubutu kufanya jeuri na kiburi kama kile? Na upinzani ninaouzumgumzia hapa si wa wabunge wachache wa upinzani kupiga kelele bungeni, ni uwingi wao kutosha kuweza kuzuia hoja mbovu za serekali iliyopo madarakani ndani ya bunge kwa njia ya kura. Kama budget ya serekali haiwezi kupita bila kuwa na idadi ya theluthi mbili za wabunge, then serekali iliyopo madarakani kama haina hiyo theluthi mbili haiwezi kupitisha budget bila kura za upinzani, na kura ya mpinzani siku zote ina uzito na gharama-- ni kama audit quarrel ambayo serekali inabidi kuiadress kama itahitaji kupitisha budget, lazima ifanye marekebisho kuadress hoja za mpinzani ili kuipata kura yake. Hiyo ndio inaitwa vibrant political system, hiyo inawatesa maraisi ya nchi kama marekani etc sio upuuzi wako unaousema wa ukabila. Wewe na Watanzania wenye mawazo chokoraa inabidi kuamka, kujifunza kutoka kwa wenzetu badala ya kudanyanywa na watu wenye mawazo kokoro kama ya kwako na baadhi ya waumini wa mfumo wa chama kimoja. Hongera Sabodo,umefungua njia, CCM na serkali yake haviwezi kumfanya chcohote kwa kuwa ninaamini biashara zake ni halali. Wafanya biashara njaa, wenye kutumia njia za rushwa na upendeleo kutoka kwa watawala, ndio waoga, wanahofia kufungiwa mifereji ya neema kwa bishara zao kutoka kwa hao watawala. Lakini kama unafanya biashara halali, unalipa kodi, unatunza mahesabu na yanakaguliwa kila mwaka, utakuwa na hofu gani? Tunamuombea ndugu Sabodo afya njema na arudi salama kuja kuwasidia Chadema kuleta mabadiliko ya kweli ambayo watanzania tuna "kiu" nayo sana
ReplyDeleteThis SEBODO is really brave. He is not afraiding to be deported back to India for supporting opposition party.Big up Uncle SEBODO and GOD bless you always, for supporting my favourate Party.
ReplyDeleteKuisaida CHADEMA kwa mahela yote hayo sio tatizo, tatizo ni CHADEMA kutokua na wagombea ubunge wa maana, maana kama hizi hela zitatumika eti kuwasaidia wasanii wa bongo flava, wanaotukana wenzao kwa matusi makali na kuwatishia kuwaua, hapo sasa ntaona hii hela inapotea bure bure!
ReplyDeleteKWA UJINGA ZOTE ZITATUMIKA KUNUNULIA MAFUTA YA HELIKOPTA HAKUNA KUIMARISHA CHAMA WALA NINI SABODO UMELIWA WACHAGA HAO!
ReplyDeleteBaba yangu mzee Mustapha ni kwa kisa gani unatusaliti?...bi ayyi dhammbin? Baba tulikuamini tukaamini ni mwenzetu halafu leo baba bila soni unadiriki kumpa adui silaha atuangamize? Baba niliwahi kukuomba unidhamini nitangaze nia kwa jimbo la Segerea kwa tiketi ya CCM ukanikatalia baba kumbe nia ilikuwa umpe nguvu mpinzani wangu aweze kunishinda...baba nimekukosea nini? bado tunakuhitaji CCM, tupe sisi hizo fehda zituwezeshe kushinda kwa kishindo...bado tuna kete turufu baba....
ReplyDeleteHivi wee Annony wa Tarehe Mon Jul 12, 10:13:00 PM. Huwezi ukajiweka pembeni uwaache wenye hoja wa-coment maana unaturudisha nyuma sana mambo ya ukabila siyo mahala pake hapa kwenye blog yetu wala hapa nchini kwetu. Wewe ni baadhi ya vijitu vinatumia vibaya uhuru wa kujieleza vinginevyo kikomenti chako Michuzi angekiweka pembeni.
ReplyDeletemzee jaffar haijui ccm eeee!!!!jaman muelewesheni huyu mzee au km vp aende mwanza akamuulize yule yule kada wa ccm aljifanya anawdhamin upinzan nin alifanyiwa kwenye hotel yake na TRA pale kapripoint karibu na ikulu!!!
ReplyDeleteGggrrrrrr Watanzania tunapenda sana Wafadhili..!!!!
ReplyDeleteMtu mmoja kuchangia fedha nyingi kiasi hicho kwenye CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA NI HATARI KWA DEMOKRASIA.
Watanzania tupende tusipende ni lazima wote kwa kidogo tulichonacho (kifedha na kimawazo)tuwe na sauti ndani ya hivi vyama (vyote); hiyo ndiyo demokrasia ya ukweli itayotuletea maendeleo ya kweli.
Tulitakiwa kuwa na sheria inayoweka kikomo kwenye viwango cha misaada ambayo vyama vyote vya siasa vinaruhusiwa kupokea. Kinyume na hapo tusije kushangaa tukijikuta Sheria Bungeni zinatungwa kuendana na matakwa ya Matajiri Wachache wanaochangia vyama vyetu vya siasa.
Soames Phares,
Reading, UK.
BAADA YA KUMWONA MREMA AKISAKATA DANSI NA MAKADA WA CCM UKUMBINI,I FELT GOOD FOR MYSELF WHY I SUPPORT CCM!!! IT WAS SHAME!!! POLITICAL SUICIDAL SPEECH AND CONDUCT.....!!!! SEBODO SUPPORT FINANCIALLY CHADEMA DOESN'T SOUND AS A NEWS TO ME!!!! VISIONARY PEOPLE KNOW WHAT KIND OF TRAP SETTING,ONE DAY WE HEAR SOUND OF A PREY...!!! LET US WAIT AND SEE
ReplyDeleteKIDUMU CHAMA TAWALA....!!!!
Chadema ,duh hao ni mangi watupu hebu wacheki walivyotoa macho....hiyo hela imetegeshwa makusudi...
ReplyDeleteCCM HAWAJAWAHI KUWA WAJINGA HATA DK 1!!Soon watu wataanza kuweweseka,,stay tuned!!!
Pendekezo kwa bwana Misupu mtu yeyote atakayeongelea ukabila au udini habari yake isipostiwe kwenye Blog ya Jamii.
ReplyDeletemh kumbe kuchangia inakua hivi?
ReplyDeleteaisee
uyu muhindi ni mtanzania?
ReplyDeleteso ana haki ya kugombea na kuchaguliwa kuwa rais wa jamhuri ya tanzania
.......bubby trap! or Road side Boom!watch ur steps.
ReplyDeleteDUH! CHADEMA JAMANI NI KIJIWE CHA WACHAGA?HAKUNA HATA MCHANGANYIKO KTK UONGOZI WA JUU????????????HAIBU GANI????
ReplyDeleteSasa hapa sijaelewa CHADEMA vinara wote wa juu wanatokea mkoa moja au? balance iko wapi?wakati Baba wa Taifa alituhusia kuwa vyama visiwe vina wingu la ukabila na udini,lakini hapa CHADEMA naona kuna mvuke mvuke wa joto la ukabila
ReplyDeleteyaani wale wenye comments fupi kama pua nadhani watoto wajuzi juzi miaka 30 kurudi nyuma tena walioko nje ya nchi kazi kuweka mkia matakoni kwa woga! hawana upeo comment zenu zimejaa chuki na woga!hazioni mbali... mara hamuwajui CCM mara huyu baba mtanzania...nini nyie???. Sabodo huwa ananunua media either 2pgs au a page kwenye gazeti la chama na serikali akiikosoa serikali na wana iprint itakua huo mchango. Sabodo is aged, been there done that! He aint scared shit!he is one solid man who can print his will on a front page stating what he have and who is leaving what.about 50% ya mali zake akifa kawaachia mayatima wa lindi. na kuna mtoto wake aliyekimbilia india huyo hapati kitu mpaka arudi kufanya kazi TZ anaamini jasho la wa TZ ni jasho la wa TZ not india.This is one man i salute one true Tanzania! yule alieandika about kibera slums ukaombe hela kwa wabunge wa kenya waliojiongezea mishahara huku kwetu hakitoki kitu endeleeni kuiba shadow za mount KLM......am a true sista!
ReplyDeleteAmesoma alama za nyakati. Huku yupo na kule yupo.
ReplyDeleteSafi sana.