JK akila pozi na Majaji wa Mahakama Kuu 10 wapya na Msajili wa Mahakama ya Rufaa baada ya kuwaapisha July 31, 2009 Ikulu Dar. Marehemu Jaji Eliamani Mbise ni wa tatu toka kushoto mstari wa nyuma ya JK.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Eliamani Mbise amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Msajili wa Mahakama ya Rufani Francis Mutungi imesema Jaji Mbise imesema Jaji Mbise amefariki majira ya saa nne na nusu tarehe 29/7/2010 .
Taarifa hiyo imesemakuwa taratibu za mipango ya Mazishi ambayo yatafanyika Arusha itatolewa baadae baada ya utawala kuwasiliana na ndugu wa marehemu.

Aidha Bwana Mutungi amesema msiba umewekwa kwa muda nyumbani alipokuwa akiishi marehemu Mikocheni kwenye nyumba za viongozi wa Serikali.

Marehemu Mbise alikuwa akifanya kazi katika kituo cha kazi cha Mahakama kuu ya Tanzania .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2010

    Haieleweki ni yupi hapo? Eleza tena.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2010

    May She rest in Peace.

    Pole kwa familia ya marehemu na wote walioguswa na msiba huo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2010

    Mwenye Miwani

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2010

    Marehemu ni wa mama wa tatu kutoka kushoto masitari wa kati nyuma ya JK au mama mweupe kuliko wote mstari wa kati na katika picha. Jina lake si Eliamani ni Eliamini Mbise

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2010

    michu eeeh, watatu kutoka kushoto juu ni mwanamke sasa ni yupi hapo?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 30, 2010

    Ukiangalia picha kuna mistari miwili na nyuma ya msitari wa pili kuna jaji mmoja mwanaume ambaye hana mstari. Sasa msitari wa pili wenye baba mwenye suti nyeusi (asiye Kikwete) kushoto kwako, ni wa tatu kutoka kwake, au ukihesabia ukitokea kulia kwako kwenda kushoto, msitari huo huo wa pili ni wa nne (mweupe).

    Binafsi namkumbuka wakati nikiwa idara ya mahakama huko mawilayani, akiwa Msajili Mahakama Kuu, alikuwa akifika mikoani kufuatilia maendeleo, pamoja na cheo ni mtu aliyekuwa mnyenyekevu sana.


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 30, 2010

    R.I.P.
    Nimesoma nae na nimefanya nae kazi.
    Mama mnyenyekevu na mpenda watu.
    Poleni wafiwa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 30, 2010

    salam za pole kwa familia,na tasnia nzima ya sheria.. Really,she was very humble,hana makuu kabisa mama wa watu..May her soul rest in eternal peace ..AMEN

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 30, 2010

    RIP

    Alikuwa mnyenyekevu sana, wala sio uzushi kwa sababu amefariki, alikuwa anaheshimu kila mtu bila kujali cheo, hakika watu kama hao huwa hawaishi muda mrefu sana kama kina nanihii vile...Poleni sana wanafamilia na wanazuoni wote

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 30, 2010

    Kwanza naanza kwa kusema Mwenyezi Mungu ailaze roho yke pema peponi.
    Pili na mrudia hyo anayesahihisha mwenzi eti mistari miwili. Hata kama nyuma kungekuwa na mtu mmoja kitu ambacho si kweli maana wapo wawili bado huo ungekuwa mstari mwingine

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 30, 2010

    So sad news! R.I.P mama Mbise.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...