Mwanamuziki ambaye pia ni mpiga gitaa maarufu aliyewahi kuwa Mshindi wa pili wa Bongo Star Search mwaka 2008, Rogers Lucas akilicharaza gita lake kwa hisia kubwa usiku huu katika tamasha la ZIFF linaloendelea katika viwanja vya ngome kongwe,kisiwani Zanzibar.
Msanii wa Hip Hop toka nchini Marekani,Spark Boogie akiapafomu baadhi ya nyimbo zake katika tamasha la ZIFF usiku huu,ngome kongwe.
Msanii wa Bongo Freva,Sultan King akifanya vitu vyake jukwaani usiku huu.
Baadhi ya vijana wa kikundi cha sarakasi kiitwacho Stone Town wakionesha umahiri wao wa kucheza sarakasi aina ya Capoera katika viwanja vya ngome kongwe usiku huu.
Kikundi cha muziki wa asili toka jijini Dar,Tatu Robo wakilinogesha tamasha la ZIFF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2010

    haya ndo mambo yenye akili,mnakuwa na matamasha ya utamaduni kama hivi sio ndombolo ya zaire ilojaa bongo
    siku moja nataka sana nihudhurie hili tamasha

    keep the good work organizers

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...