JK akisalimiana na Ruge Mutahaba ambaye ni kiongozi wa Nyumba ya Vipaji (THT) ambaye yuko Dodoma na wasanii nyota kibao ambao watatumbuiza wikiendi hii kwenye Fiesta 2010. Jana JK aliwaalika Ikulu Ndogo ya Chamwino na kupata nao dina la mchana
JK akisalimiana na Chegge
JK akisalimiana na Fid Q
JK na Cpwaa
JK na Mh. Temba
JK akipeana mikono na Dully Sykes
JK na Mwanafalsafa
JK na Barnaba wa THT
JK na wasanii
JK akisalimiana na Fellah, kiongozi wa Wanaume TMK
JK na mwamba wa Kaskazini Joe Makini
JK na KR wa TMK Wanaume
JK akisalimiana na Marlaw
JK akisalimiana na msanii wa THT
Mama Salma Kikwete akimsalimu Marlaw
Mama Salma Kikwete akisalimia wasanii
Ni wakati wa maakuli

















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Michuzi.
    Mheshimiwa Rais wetu amekutana na wanasanaa wa hapa nyumbani.anastahili pongezi kwa kutambua mchango wao.

    lakini

    Mbona katika hawa wanasanaa waliokutanishwa na mheshimiwa rais hakuna hata mmoja mwanasanaa kutoka kule visiwa vya karafuu ZANZIBAR.


    Au kule hakuna wanasanaa?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2010

    Hahahahahahaha wasanii wakongwe poleni jamaa hana haja nanyi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2010

    mbona tshirt zinamnadi kikweteee!!!! Dina pamoja na wasanii au?

    ReplyDelete
  4. Mdau no 5July 14, 2010

    Misupu huyo sio kalapina bwana, huyo ni K R MULLA .

    kuwa makini na uandishi, kama vp we sema msanii tu usichafue hewa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2010

    HIVI HAWA WASANII WAMEJIULIZA KUWA HAWA WANASIASA WALIOKO MADARAKANI WAMEWASAIDIA NINI?
    NI MARA NGAPI TUMESIKIA WANAKUTANA NA RAIS, NA JE AMEWASAIDIA NINI KUTATUA MATATIZO YAO HUSUSANI KATIKA SEKTA NZIMA YA SANAA TANZANIA?
    TATIZO KUBWA LA HAKI MILIKI ''COPYRIGHT'' LINALOKWAMISHA WASANII LIMEFUMBIWA MACHO, NA WASANII NAO WOTE VIPOFU, WALA HAWAELEWI SHERIA HII INA UMUHIMU GANI KWAO.
    TATIZO LA UHARAMIA (PIRACY)LINAENDELEA KUTAFUNA SANAA NA KUUA VIPAJI VYA WASANII, NA DAWA PEKEE NI SHERIA KUPEWA MENO MAKALI PANDE ZOTE.
    SHERIA IMEPITISHWA TANGU MWAKA 1999, LAKINI HAKUNA LOLOTE,KUTATUA TATZO HILI, HATA VYOMBO VYA HABARI HAVIWAELEMISHI WASANII HAKI ZAO KWA MUJIBU WA SHERIA ZAIDI YA KUTUMIA TU KAZI ZAO KATIKA RADIO NA TELEVISHENI, NA HAKUNA ROLALITIES WALA NINI.
    TUNAONA SASA WANASANII KAMA WAMEKATA TAMAA NA SASA WANADHANI KUINGIA AU KUJIPENDEKEZA KATIKA SIASA NDIO NAFUU YAO.
    HII NI KAMA KUJIUZA KWA BEI RAHISI, KUMBUKENI KAZI ZENU ZINATHAMINI ZAIDI YA HIYO, SIMAMENI KIDEDEA, MSHIKENI RAIS SHATI, AWASAIDIE KULETA MAPINDUZI KUILINDA SEKTA YA SANAA KWA KUWEKO SHERIA IMARA YENYE MENO ILI MUWEZE KUFAIDIKA NA KAZI ZENU.
    SHERIA KALI PEKEE NDIO INATAKAYOWAOKOA NA SI KAMPENI ZA KISIASA.
    MSIIACHE SEKTA NA VIPAJI VYENU VIKAWAFAIDISHA WACHACHE TU, WANAOJIITA MA-DISTRIBUTORS AU MAPROMOTORS, WANAJENGA MAGOROFA YA KIFAHARI NA KUNUNUA MAGARI YA KIFAHARI KUTOKANA NA KAZI ZENU HUKU NINYI MKIAMBULIA VIJISENTI.
    IKIWEZEKANA ANDAMANENI KUISHINIKIZA SERIKALI ILETE MAPINDUZI KULINDA WASANII KWA MUJIBU WA SHRIA KALI, NA MFUMO IMARA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2010

    hahahahaha hii serikali yetu inatisha,Hakuna lolote hapo anataka kura zenu tu wasanii na huo ni mpango wa Ruge baada ya kuona Mr.2(sugu) anagombea ubunge pamoja na nakaya sumari kupitia chama cha chadema sasa ccm inahofu inaweza ikapoteza kura kwa vijana wengi.Pia Ruge anatata kujisafishia jina Kupitia wasanii wakongwe,Chege,Temba,MwanafA,FidQ na wengine amkeni nyinyi acheni kuuzwa kwa bei raisi( ya Ubwabwa).

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2010

    Hakuna dress code katika ikulu yetu ? Yaani watu wanaweza kuvaa nguo kama hizo halafu wakaongea na Rais....hii inachefua.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2010

    Kaaaazi kwelikweli. Sasa rais akutane pia na wanenguaji kama vile kina Aisha Madinda na Super Nyamwela kwani nao wana mchango ktk jamii

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2010

    mmmmh watanzania sisi we acha tu,kula huku kubaya sana,bora ushinde na njaa siku mbili ule miaka mingi ijayo kuliko kula mlo mmoja ukae na njaa miaka mingi jayo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2010

    HUWA TUNAWASEMA WANANCHI WA KAWAIDA TU KUWA WANAHONGWA PILAU ,,,,

    ReplyDelete
  11. This is nice move by the incumbent party...music groups are very influential to the young supporters..no doubt you get their votes already... Excellent approach wana CCM!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 14, 2010

    BREAKING NEWS......
    PROF JWANI MWAIKUSA AUWAWA NA MAJAMBAZI...
    Wakili na Mwanasheria nguli na Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. Jwani Timothy Mwaikusa amefariki dunia baada ya kuuwawa na majambazi usiku wa kuamkia leo wakati akirejea nyumbani kwake maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam. Mwaikusa pia alifanya ka...zi katika mahakama ya kimataifa I.C.T.R Arusha na alikua rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowasilisha kuhusu mgombea binafsi.
    Kwa wale waliosoma literature A- Level kama mimi, Prof. Mwaikusa pia alikua mwandishi mzuri wa poems ambazo wengi wetu tulizijibia mitihani.
    Pamoja nae pia ameuwawa mwanae aliyekua akitoka nje kumfungulia geti, na mtu baki aliyekua akipita njia.
    Kwa jicho la kawaida tu, haya yatakua mauaji ya kisasi au ya kumnyamazisha kuhusu jambo fulani kwakua habari za awali zinasema wauwaji hao hawakuiba kitu chochoteSee More

    41 minutes ago · Comment ·LikeUnlike · Share

    Nkundwe Mwakilema NILIYOYAFAHAMU:
    Career:


    ... See More

    * Professor of Law, Faculty of Law, University of Dar es Salaam 1999



    * Mkono & Co Advocates since 1998



    * Advocate, High Court of Tanzania since 1988



    * Managing Editor of the Tanzania Law Reports.

    Qualifications:




    * Ph.D., School of Oriental & African Studies, University of London, UK, 1995



    * LL.M, University of Birmingham, UK, 1985



    * LL.B (Hons), University of Dar es Salaam, Tanzania, 1981.

    ReplyDelete
  13. Ralph NahatoJuly 14, 2010

    I will quote the late Mr. Julius Nyerere, " Hakuna kitu kibaya duniani kama umaskini wa akili...." R.I.P. Mr. Nyerere.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 14, 2010

    UNAJUA MTU AKIWA NA NJAA SANA UNAKOSA UWEZO WA KUFIKIRI VIZURI. HAWA WASANII NI NJAA ZINAWASUMBUA. WATAENDELEA TU KALALAMIKA WAKATI ANAYETAKIWA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YAO WANAMLAMBA MKONO.

    WENGI HAPO KUPIGA PICHA NA KIKWETE BASI WAMESHASAU MATATIZO YAO. MTAISHIA TU KULIPWA HIZO ELFU HAMISINI NA LAKI MOJA MOJA MPAKA MNAZEEKA. KUMBUKENI MUZIKI NI WA MUDA MFUPI SANA, MAISHA YA MBELE UTASHI VIPI WAKATI SAUTI NA KUCHEZA KWENYE MAJUKWAA KUTAKWISHA.

    KWELI WAJINGA NDIO WALIWAO.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 14, 2010

    hiyo picha ya kwanza imenihudhi.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 14, 2010

    tuna mwendo mrefu adi tuelimike,pesa ni sumu ya mtu.na umemsahau flora mbasha na mumewe maana ndo walinchosha kabisaaaa.

    "mimi nimechangia ww je?"

    kaaaazi kwelikweli...siwaelewi

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 14, 2010

    chege umeniudhi wewe?

    ReplyDelete
  18. WASANII WA BOMGO FLEVA NI WACHAFU SANA.....MINYWELE KAMA MACHIZI VILE, DAMN....UNAKUTANA NA RAISI, ANGALAU UWE MSAFI KIDOGO...

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 14, 2010

    Hata siamini macho yangu kuona wasanii wote hawa wanakuwa brain washed with this guy RUGE yaani hamna maamuzi ya peke yenu nyiewatumwa wakubwa. Sikutegemea wasanii wanaimba lkn hawafuati yale wanayoweka kwenye mashairi yao. Njaa tu na kuchoka kwingi ...Wengine wanajidai wasomi kumbe zero tu..hamwezi leta mabadiko nyie. Choka Mbaya, Chege. MwanaFA umeniudhi sana

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 14, 2010

    hahaha1 SASA KILA MSANII BONGO ameweka LOCKS!!! mikumbo hii jamani ya wabongo! na miwani nyeusi:))))
    inaelekea huko ukikatza na miwani nyeusi lazima wakupore

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 14, 2010

    sisemi sana ila big up sugu

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 14, 2010

    SASA APA CCM HATUCHUKUI KWELI JAMANI

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 14, 2010

    ankal, kwema?
    we anonymous uliyezungumzia COPYRIGHT, napenda kukuambia kama hujafanya utafiti usizungumzie jambo, kwa taarifa yako sheria inawalinda na now adays wanapata mirahaba yao, isipokuwa wasanii wengi sio wanachama wa cosota na cosota ina limitation katika utendaji, but marekebisho ya sheria ni ya muhimu. haki zao zinalindwa, na kwa taaarifa yako huwezi kukomesha piracy, unapunguza.
    refer Copyright and neibhouring rights act no.7 of 1999 and other regulations.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 15, 2010

    Kila mtu ana uhuru na haki ya kukisapoti chama anachokitaka. Just face it: that's reality. Pongezi wasanii wetu.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 15, 2010

    I support you 100% Ralph

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 15, 2010

    CHA MUHIMU NI TIMING..HAWA VIJANA WANANJAA HIVYO KAMA UNA WAYS AND MEANS ZA KUWAMIX KWENYE HIGH PROFILE GATHERING..BASI UNAWA BRAINWWASH KAMA HIVI..HATA MIMI NINGEKUWA RUGE NINGEWAFANYIA THE SAME...UJANJA NI KUJIKITA KWENYE SYSTEM ILIYOPO YENYE NGUVU..NCHI HII UKIJIFANYA MWANAMAPINDUZI SIJUI UNATAKA MABADILIKO,UTAKUFA NJAA...MTU KAMA MR II SUGU NI KWELI ANAUCHUNGU NA NI MPIGANAJI LAKINI NAMUONEA HURUMA SABABU ATAPOTEA TU NA TUTAMSAHAU...JUST STICK TO THE SYSTEM ILI ULE KIULAINI..HAKUNA MAPINDUZI YA KWELI TUACHE UNAFIKI

    Chalii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...