Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2010

    saa saba na nusu mchana!!!!!hio foleni balaa....mimi nilifikiri foleni ni asubuhi na jioni[rush hrs].wabongo na nyie mmezidi kaeni makazini sio kuzurula hovyo siku nzima

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2010

    mheshimiwa BUMBER TO BUMBER ndio wapi mpaka wapi ??ausp

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2010

    hivi ukingongwa na kikamera chako utamlaumu nani!! nchi yenyewe ya walevi !!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2010

    naona wa bongo mnajitaidi usafi kidogo sikama nairobi adi wanyama wanashindana na magari

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2010

    Nani angeweza kuwaza kwamba Dar itakuwa hivi leo?

    Wakati wa Nyerere kuingiza gari nchini ilikuwa kwa kibali, na kuendesha gari siku ya jumapili ilikuwa mwisho saa nane mchana ili kusave mafuta.

    Sijui kama ni wakati ule au hivi sasa ndio bora!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2010

    Ni Bumper-to-bumper, sio bumber-to-bumber.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2010

    Mr Michuzi, siku zingine uwe unauliza kabla ya kuandika utumbo hapa...bumber ndo nini tena??, I guess you meant to write bumper to bumper...hata kama hujui kiingereza lakini una internet kaka, to verify the words u are not sure of. Au nadhani ni vijana wako ulowaajiri ndo wanafanya kazi za kukurupuka hivi...nimekuwa nikishangazwa sana na lugha mbovu inayotumika humu bloguni. Try to be professional, u have a very big audience Michuzi. Am just saying.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2010

    mnashangaa nini? Mnazi Mmoja leo viongozi karibu wote wlishiriki ktk maadhimisho ya siku ya Mashujaa! Hivyo kupelekea barabara muhimu za kati ya mji kufungwa.

    Foleni hii hata wakati wa Nyerere miaka ya 1980 ilikuwepo, sema wengi mlikuwa hamjafika Dar, ndiyo maana Samora na Sokoine zikawa barabara za 'one-way', daraja la Salander jipya likajengwa la zamani sasa ni la wapita kwa miguu na baiskeli, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi ikawa up-graded, yaani sisi watoto wa mjini tunajua historia ya jiji la Dar(Diziam)
    Hakuna Kushangaa, mjini hapa.
    Mdau
    Townie.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2010

    Michuzi, unalalamika nini wakati Rais wenu amesema ya kuwa hiyo ni sign ya maendeleo. Subiri mtajengewa flyover kila kona ya huo mji. Watanzania lazima tujue ya kuwa elections have consquences......

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2010

    Alieandika "bumber to bumber" lazima atakua anatoka mitaa ya Iringa-Iringa ivi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 25, 2010

    BUMBER TO BUMBER....lol

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 25, 2010

    INAKUWAJE KWENYE CROSS ROADS HAKUNA STOP SIGN?WHO WILL GO FIRST?NDO MAANA MAFOLENI YA KIJINGA HAYATAKWISHA HUKO BONGO

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2010

    thanx mithupu!
    lkn ni bumper to bumper..........sio bumber!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2010

    Public transport wakati wa Nyerere ilikuwa superb. UDA walikuwa na ratiba za uhakika, ratiba ikisema basi litapita saa 5:15 asubuhi kweli litapita ktk kituo saa hiyo.

    Wasafiri wa UDA walikuwa na Travel- card wanalipia mwezi mzima kama London vile. Lakini mkaharibu usafiri wa umma, hamkuweza kuuboresha ulipokuwa umefikia.

    Matokeo kila mtu anataka usafiri wake binafsi, kitu ambacho hata London, New York, Tokyo, Paris n.k watu wana-prefer usafiri wa reli/basi ingawaje wana magari wamepaki nyumbani.

    Usafiri wa umma bora ndio kipimo halisi cha maendeleo na siyo vurugu za magari binafsi na daladala ndiyo kipimo cha mafanikio.

    Kwa kweli badala ya kupiga hatua kiusafiri kuwahi tunakokwenda kwa muda mfupi, sisi ndiyo tumerudi nyuma kwa 'kudamka alfajiri na kuchukua masaa mengi kufika ktk shughuli zetu mbalimbali jijini DSM.
    Mdau1

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 25, 2010

    MTU HAPOA MMOJA ANASEMA KUINGIZA GARI WAKATI WA NYERERE ILIKUWA HADI KIBARI ACHA KUMCHUKIA NYERERE KWA SABABU ZAKO BINAFSI EBU KUWA MKWELI MTANZANIA MWENZANGU, HIVI MIAKA YA 60 HADI YA 70 HADI YA 80 NI WATANZANIA WANGAPI WALIKUWA NA UWEZO WA KUNUNUWA GARI JAMANI ACHA KUPOTOSHA UKWELI MTANZANIA MWENZANGU! WATU HAWAKUWA NA UWEZO WA KUNUNUWA GARI KI-OVYO KAMA ILIVYOKUWA SASA NA HATA NCHI PIA HAIKUWA NA PESA ZA KIGENI ZA KUTOSHA KUKIDHI HAJA HIYO, IVI UNAJUWA GARI HAINUNULIWI KWA MADAFU INANUNULIWA NA DOLLAR, USIONE UNANUNUWA GARI KUOPITIA BANK UNATOWA MADAFU UJUWE HIYO PESA INABADILISHWA KUWA DOLLAR NA KUPUNGUZA DOLLAR ZA NCHI KATIKA MFUKO WA SERIKALI KUPIRIA BOT AMBAZI ZINGENUNUWA KITU KINGINE CHA MUHIMU KWA WAKATI ULE, ANYWAY THAT IS ANOTHER SCHOOL KWA HAPA SOTOWEZA KUKUFAHAMISHA KIUNDANI INAKUWAJE UNAPONUNUWA GARI KUTOKA NJE NA MADAFU YAKO. KIUFUPI NI KWAMBA ENZI ZA NYERERE NI WATU WACHACHE SANA WALIKUWA NA UWEZO WA KUNUNUWA GARI NA WALINUNUWA JAPO KWA VIBALI NA NCHI HAIKUWA NA PESA YA KUTOSHA YA KIGENI, MBONA MABAHARIA WENGI TU WALIKUWA WANARUDI NA MAGARI NI KWA SABABU PESA YA NCHI ILIKUWA HAIHUSIKI WALIKUWA WANANUNUWA GARI KUTOKA NA PESA WALIZOCHUMA WAKIWA NJE KWENYE KAZI ZAO ZA KIBAHARIA NA NDIO WATU WALIOKUWA NA UWEZO WAKATI ULE WA KULETA GARI NCHINI

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 25, 2010

    HAKUNA HAJA KUJA NA GARI MJINI NI VERY EXPENSIVE IN TERMS OF FUEL AND TIME.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 25, 2010

    ANOMY WA KWANZA UKO SAHIHI KWANI FOLENI GANI IANZE ASUBUHI HADI USIKU?
    ASUBUHI INAELEWEKA KWA AJILI YA KUWAHI KAZINI, SASA MCHANA IWEJE FULENI WAKATI WATU WAKO MAKAZINI? NA BONGO HAKUNA SHIFT ZA KAZI KWANI SEHEMU NYINGI NI SHIFT MOJA TU.

    NAHISI UZURURAJI NAO UNACHANGIA KWANI KAMA WATU WANATULIA MAKAZINI FOLENI ZA MAGARI INGEPUNGUA MCHANA HADI SAA TISA WATU WANAPOANZA RUDI NYUMBANI TOKA MAKAZINI

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 25, 2010

    Kulinganisha bongo wakati wa nyerere na sasa ni sehemu ya kuwa nyuma kimawazo, utrudu nyuma kiasi gani? Ama utalinganishia nchi yetu wkati wa ukoloni na sasa, nani angetegemea ungekuwa unabofya online kama hivi ???

    Linganisha Bongo na nchi zingine zinazoendelea leo .

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 25, 2010

    nyerere ndo chanzo cha amtatizo ya watanzania,nawashangaa bado kunawaomtukuza,nchi za eastern europe wamestuka now,wale viongozi wa ujamaa wote wametolewa kwenye history za nchi,na masanamu yao kuvunja,ujamaa umechangia ujinga wa watanzania,ulozaa mafisadi.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 26, 2010

    HAVE YOU PEOPLE NOTICED THAT ALL OF THE CARS IN THE CLIP ARE TOYOTA BRANDED, I THINK WITH AN EXCEPTION OF ONE OR TWO WHICH ARE EITHER NISSAN OR HONDA!!! HAVE JAPANESE GOT AN AGENDA WITH TZ?!!! BRIIIILIANT

    ReplyDelete
  21. Aaarghhh! Embu ishieni na upuuzi wenu wa kila siku. Kila kukicha habari ni foleni tuuu, foleni, sijui misururu!! Hivi hakuna kitu kingine cha kuongelea huko bongo kwetu zaidi ya hilo?

    Hata mkiliongelea kila siku wenzenu wameweka gundi kwenye masikio. Hawawasikilizi. Mnapoteza muda wenu bureee!

    Wenzetu kule kwa bwana Paul Kamau wameshaanza kujenga barabara za uhakika badala ya sijui mafulaiova sijui nini! Nakwambia wataanzisha kafulaiova kamoja na kuhakikisha kuwa wakati wa uchaguzi zege zilapigwa, yaani kama sempo vile ya kusemea kuwa 'tuko kaziin'. Wataweza hata kumalizia, afu uchaguzi ukishapita, sahau. Kafulaiova katabaki aisoletedi kama kale kadaraja ka waenda kwa miguu pale Manzese. Itapita miaka mitano bila kuongeza kengine. Suluhisho la taabu ya kusafiri itabaki palepale.

    Kilichobaki ndugu zangu, kama unahitaji kuishi kwa nafasi yako - hama nchi ndugu. Vinginevyo, baki ukisali na kusubiri siku ambayo barabara zote za Bongo zitakuwa zimeblok! Yaani hakuna gari kwenda mbere wara kuludi nyuma.

    Labda zianzishwe DART (ule mradi wetu wa mabasi yaendayo kwa kasi ya ajabu) itumiayo endikopta bandala ya mangari (mambasi).

    Dayasipora Damu

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 26, 2010

    jamani madereva wa kibongo acheni kupiga hivyo vi horn kila dakika,kuna foleni unampigia horn aliyembele yako unataka afanye nini?

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 26, 2010

    bandugu mmeamua kuishi dar basi endeleen na matatizo yenu ya mifoleeni kwan kuishi dar lazima mbona kuna mikoa kibao tu ya kula bata!!!acheni ulimbukeni!!!na huo ulimbukeni ndo unaopelekea mnakuwa mandhan labda kununu kijigari ndo maendeleo mpaka mnapelekea mifolen mjini huo ni ushamba!!!

    halafu na nyie wanasiasa kuwepo hapo sio ndo kwamba mnajua sana anytym mnaweza kutoka!!!jana mlituambia tunaleta magari yaendayo kasi!!hilo halijaisha mnakuja na maflyover!!!cjui kesho ndo mtatuambia mnaleta helkpter??? acheni kuwafanya wananchi matahira!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 26, 2010

    KWA SABABU TUMEAMUA KUACHA KUFIKIRI, FOLENI HAZITAISHA.. HIVI NI KWA NINI HADI LEO (NA MATATIZO KIBAO YA MIUNDO MBINU TULIYONAYO) TUNAENDELEA KUTOA VIBALI VYA KUJENGA MAJENGO MAREFU KATIKATI YA MJI?? KWA NINI YASIJENGWE NJE YA MJI?? TUSIKILIZE WATAALAMU JAMANI NA TUACHE BLAAH BLAAH..!!!

    Mdau chiggs, deslam

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 26, 2010

    Wakati wa Mwalimu, ukiwa mfanyakazi unakopeshwa gari maana mshahara na thamani ya fedha ilikuwa juu, unajaza fomu unaenda Riddoch Motors, MTAVA n.k unapewa mchuma unakatwa kila mwezi toka mshahara wako.

    Hivyo namuunga mkono mdau Townie kuwa watu wengi humu walikuwa hawajawahi kukaa mijini wakati wa Mwalimu na kujua enzi hizo watu waliishi vipi mjini au labda walikuwa hawajazaliwa.

    Tuchukulie suala la Drive-In cinema, majumba ya sinema, mikopo kwa ajili ya nyumba, magari na vifaa vya nyumbani, mali-kwa-mali, ukienda jalalani unakuta makombo ya vyakula yametupwa hata uswahilini, hii leo sidhani kama kuna mtu anatupa makombo ya chakula, enzi za Mwalimu hii yote iliwezekana kwa wa vipato vya juu na chini, tazama picha za watanzania wa miaka ya 1960, 1970 na mwanzoni 1980 walikuwa wamenawiri kwa kula chakula bora.

    Mdau
    Born Town.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 26, 2010

    Acheni majungu badala yake mtoe ushauli na mawazo nini kifanyike ili tatizo la traffic lipate solution kwa sababu ni tatizo sugu kwa watanzania na linaitaji litatuliwe.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 26, 2010

    Tatizo watu wengi wanapenda kupotosha sana kuhusu Nyerere na utawala wake. Hayo mnayoyasema ya kutembea wikiendi kwa kibali ilikua ni nyakati baada ya vita ya Uganda kipindi hali ya Uchumi iliyumba sana kutokana na gharama ya vita ile, lakini kabla ya hapo gari ilikua unaweza kumiliki. Reserve ya fedha ya kigeni ilikua ya kutosha kutokana na mauzo makubwa ya bidhaa za kilimo kabla ya vita ya Uganda

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 27, 2010

    MAGARI MENGI NI STJ STK HAPA YATOKEEE TUUU YANAFANYA NINI SI YAENDEE DODOMA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...