MAONI YANGU KUHUSU HOJA
BINAFSI JUU YA KERO YA FOLENI DAR ES SALAAM

Kwanza kabisa naomba kuunga mkono na kumpongeza mtoa hoja, baada ya kusema haya naomba nitoe maoni yangu kama ifuatavyo;

Kwa maoni yangu ni kuwa msongamano wa magari Dar Es Salaam unasababishwa haswa na mipango miji mibaya ya wanaohusika na mipango miji, hayo mengine yanayosemwa ni dalili tu za ugonjwa au ni magonjwa yanayosababishwa na tatizo kuu la kutokuwa na mipango miji endelevu, kwa kuzingatia mifano ifuatayo utaweza kuelewa nini nachokiongelea.

1. Dar Es Salaam hatujawa na magari mengi kiasi cha kuwa na msongamano tunao uzungumzia, tatizo hili linasababishwa na mipango miji mibaya ya kulundika shughuli na huduma za kijamii mahala pamoja, fikiria magari yanatoka bunju yanaingia bagamoyo Road, yanakutana nay a tegeta, boko, mbezi mwenge , kijitonyama, yoote hayo uelekeo ni mmoja mitaa ya posta, kwa hali hii huwezi kukosa kuwa na foleni!!! Katika nchi zenye mipango miji mizuri mtu anaweza kupata huduma zote muhimu bila kulazimika kwenda katikati ya mji

2. Mwananchi anatoka Mbweni anaenda uwanja wa ndege, analazimika kuja hadi mwenge ili apate uelekeo wa kuenda anapotaka kwa kuwa hakuna njia mbadala itakayomfikisha anakoenda, hali hii pia ni kwa wale wanaokwenda kimara, mbezi, kibamba na maeneo mengine ya morogoro road, tatizo hili pia wanalo wakazi wa tabata na segerea wanapotaka kwenda airport kulazimika kwenda hadi Mandela road, buguruni kasha nyerere road wakati uwanja wa ndege upo karibu nao

3. Barabara za Dar zilikadiriwa kuhudumia idadi Fulani ya wakazi, kwa wakati huo hawakuzidi milioni moja, sasa jiji lina wakazi zaidi ya milioni nne ambao wanaongeza mahitaji ya usafiri wa umma na ule wa binafsi lakini miundo mbinu haikuwi kwa kasi ile ile ya ongezeko la watu


4. Kwa ruhusa za malaka zinazohusika unakuta inavunjwa nyumba iliyokuwa na ofisi tatu na wafanyakazi 20 linajengwa jengo la ghorofa 25 lenye ofisi zaidi ya mia na wafanyakazi karibu ya mia sita kwa miundo mbinu ile ile ya nyumba ya ofisi tatu

5. wahusika wa mipango miji bado hawajatoa kipaumbele kwa barabara za ndani yaani feeder roads , magari mengi yanapita barabara kuu sio kwa kuwa ni lazima yapite huko bali ni kwa sababu za kukwepa mashimo makubwa kwenye barabara za ndani


6. Huduma ya usafiri wa umma ni duni sana kiasi cha kuchochea haja ya wananchi wengi kumiliki magari binafsi na hivyo kuongeza idadi ya magari barabarani
7. Barabara tulizonazo hazina utengani wapi mwenye baiskeli,au pikipiki apite au mwenda kwa miguu, woote hawa wanapita sehemu moja bila kujali tofauti za mwendo kasi baina yao

8. Kwa mipango miji yetu kama ilivyo sasa hakuna vipimo vya uzito au urefu wa gari, kama lipo basi ni kwenye barabara chache ambazo mimi sikubahatika kuziona, kwa hali hii huwezi kushangaa ukakuta lori kubwa katikati ya mji tena saa za kazi au ukakuta lori limekata nyaya za umeme au simu kutokana na urefu wake wa juu.


SULUHISHO

Kwa maoni yangu suluhisho la tatizo hili la msongamano wa magari litaondoka tu
Pale ambapo tutaweza kuwa na mipango miji sahihi na endelevu ambayo itazingatia hali ya sasa na matarajio ya baadae kutokana na kukuwa kwa shughuli za kiuchumi na kijamii za nchi.

Pamoja na mipango hii kutayarishwa utekelezwaji wake uwe kwenye eneo lingine la wazi ambapo pataundwa mji mpya wenye miundo mbinu ya kisasa na yenye kukidhi ukuwaji wa shughuli na idadi za watu.

Mradi huu wa ujenzi wa mji mpya katika eneo la wazi utatekelezwa kwa gharama nafuu kuliko kufanywa ndani ya Dar Es salaam ya Sasa ambako kutakuwa na suala la kulipa fidia kwa wale watakaovunjiwa kupisha ujenzi wa miundo mbinu mipya jambo ambalo litasabisha migongano ya kijamii baina ya wananchi na wenye mamlaka.

Jambo kama hili la ujenzi wa mji mpya si geni nchi nyingi zimefanya na ndio maana hata ukienda Italy leo hii kuna Roma mpya na ya zamani, kadhalika Amman Jordan na nchi nyingine nyingi kuna mji mpya na wa zamani, mji wa zamani ukiwa ndipo palipoanzia mji.

Kuendelea kung’ang’ania Dar na kuruhusu ujenzi wa magorofa makubwa Maeneo ya posta na kariakoo ni kuzidisha tatizo la msongamano wa magari na siku si nyingi itakuwa msongamano wa maji taka , uchafu nk.

JAMANI WADAU WOTE KATIKA MIPANGO MIJI NA MAENDELEO YA MIJI IKIWA NI MADIWANI, WABUNGE, WATENDAJI NA WANANCHI KWA UJUMLA TUAMKE NA KUACHANA NA MAWAZO YA KALE KUWA KILA KITU NI MITAA YA SAMORA NA KARIAKOO TUAMUE KUUNDA DAR MPYA NA YA KISASA KATIKA ENEO JIPYA LA WAZI AMBAKO TUTAWEKA KILA AINA ZA BARABARA ZA JUU NA CHINE, MBILI, TATU ,AU NNE KWA KADRI YA MAHITAJI YETU, HILI NDIO SULUHISHO LA KUDUMU.
KUWEKA NJIA TATU, KUWEKA ASKARI POLISI WENGI BARABARANI, KUHAKIKI LESENI ZA UENDESHAJI HIZI NI HUDUMA ZA KWANZA TU AMBAZO HAZITIBU UGONJWA SANA ZINAULEA NA KUZIDI KUUPAUWEZO WA KUJIJENGA.

NAOMBA KUTOA HOJA

ASMAH YAHYA
KIGAMBONI
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2010

    WADAU WANGU NAOMBA KUUNGA MKONO HOJA!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2010

    matatizo haya yote yanajulikana hadi serikali kuu, kikwazo ni kwamba viongozi wetu hawana uthubutu wa kufanya maamuzi muafaka na kupata suluhisho la kudumu. kila kiongozi anayeingia madarakani anafanya maamuzi yenye impact kwa muda huo tu atakaokuwepo madarakani yaani hawafikiri TZ in 50yrs to come inatakiwa iweje, ndo maana hata bara2 zilizojengwa awamu ilopita sasa hivi zinafanyiwa marekebisho kutokana na kuwa chini ya kiwango, na zinazojengwa sasa nazo zipo chini ya kiwango.
    NAMUOMBA JK KAMA KIONGOZI WA NCHI ATOE KIPAUMBELE JAPO KWA SEKTA MOJAWAPO YAANI SISI WANANCHI TUONE DIRECT IMPACT YA HIYO SEKTA, MFANO JIRANI ZETU WANA KENYA AIRWAYS INAFAHAMIKA ULIMWENGUNI , NA SISI BASI TUCHAGUE KITU KIMOJA TUKIFANYE KWA UFANISI N FEEL PROUD OF IT. mfano tunaweza chagua barabara au umeme au hata kilimo iwe hata mgeni anapokuja Tz aseme TZ kuna umeme wa uhakika wanauza hadi EA nzima au tz kuna bara2 safi nchi nzima au aone tz yenye wakulima walioendelea. but hii gusagusa ndo tunaishia kuwa na viraka katika kila sekta.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2010

    Hoja nzuri sana pendekezo langu wakati tunasubiri kujenga new DAR serikali na taasisi zake zote hamieni DODOMA tafadhali hivi kwanini hamtaki kwenda??!!! mnatubana sana maana barabarani STK,SU,ST NA JW zitapungua so msongamano nao utapungua

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2010

    Mimi tatizo langu naliona hasa pia kwa parking. gari zinapaki barabarani pia, mfano mzuri ni barabara ya samora pale JMMall. Watu wa mi[pango miji wachovu kabisa kwani hizi nyumba zinazovunjwa/maghorofa kwanini wasipewe condition ya kujenga floor moja ya parkings kwa maghorofa mapya? Nenda karia koo hali ni ile ile wanavunja mapagale wanajenga makwangua anga ya rosheni 7 au 8 bila ya kua na parking wakati humo wanapangisha maofisi wakati hapo mwanzo pagale lile lilikua na familia ya watu 6.Ofisi hizi watu wanamagari wanapaki barabarani upande mmoja njia inafinywa badala ya kupishana kwa raha inabidi upunuze kasi ili msikwanguane na wakati huo huo unaleta foleni kwa vile spidi inakua ndogo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2010

    JAMAA ANA HOJA NZURI,INAONEKANA NI MSOMI.

    MHESHIMIWA MICHUZI,NAUNGA MKONO HOJA KWA ASILIMIA 99.99

    Nicholaus,
    Netherlands

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2010

    Mkuu Yahya,

    Nikupe hongera kwa hoja zenye busara.

    Ningependa kukusahihisha kidogo kwenye hoja yako nambari 2 kama hivi:
    Wasafiri wanao kwenda kimara, mbezi, kibamba na maeneo mengine ya morogoro road kutokea Mbweni kwa sasa wanaweza kupitia Goba ambako mpaka Novemba 2009 barabara ile ilikuwa inabitika vizuri kabisa mpaka kutokea Mbezi. Sio lazima waje Mwenge ndio waweze kwenda Mbezi kupitia Ubungo.

    Vivyo hivyo wale wanaotaka kwenda Uwanja wa Ndege kutokea Segerea na Tabata, wao nao wana hiari ya kupitia Segerea Seminari na kutoka Stakishari kisha Uwanja wa Ndege. Hiyo barabara nayo ni ya kiwango cha lami. Wanaotaka kupitia barabara ya Mandela wanafanya hivyo kwa mapenzi yao.

    Ni hilo tu, mchango wako mzuri sana hasa hoya namba 4. Michuzi huwa anapenda kufurahia kuwa vikwangua anga vinazidi kuongezeka. Ni aibu tu kuwa vinaongezeka sehemu kinyume kabisa. Laiti kama makampuni mengine yangeiga mfano wa Vodacom wa kujenga HQ zao Goba, au Wizara ya Kilimo kuhamia Tazara na Zain kujiweka Kijitonyama.

    Huko katikati ya Jiji zibaki ofisi za balozi na Ikulu tu.

    Mdau Nawakilisha.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2010

    Hivi raisi anasemaje kuusu swala hili ??kwani asiseme kwamba halioni !! kwa sababu wahusika amelifungia swalahili macho !!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2010

    HUU MTAA WETU UNA NYUMBA 13. MIAKA 7 ILIYOPITA NI BABA MATATA NA MZEE MASSAWE NDIYO WALIKUWA NA MAGARI. SASA HIVI NYUMBA ZOTE 13 ZINAMILIKI MAGARI ZAIDI YA MANNE KWA KILA NYUMBA. PALE KWA MZEE MAGANGA YEYE, MKEWE, MABINTI ZA WOTE 3 NA MTOTO WA DADA KILA MMOJA ANAMILIKI GARI LAKE. UKIJA HAPA KWA HUYU MWARABU NDIYO USISEME MAGARI YAMEJAZANA KAMA YADI YA KUUZIA MAGARI. HUYU JIRANI WA KARIBU YETU FAMILIA YA WATU 6 ASIYE NA GARI YULE MDOGO AMBAE HAJAFIKISHA UMRI NADHANI ANASUBIRI UMRI UTIMIE. HAPA KWANGU NIKO MIMI NA MKE WANGU LAKINI WADOGO ZANGU NA SHEMEJI ZANGU JUMLA 5 KILA MMOJA ANA USAFIRI WAKE. KIKUBWA ZAIDI WAKAZI WOTE WA MTAA HUU HUTOKA ASUBUHI NA KURUDI JIONI. MIAKA YA ZAMANI PALE TANASCO DRIVE IN AU NYUMBA ZA TPDC MIKOCHENI ILIKUWA LINAKUJA BASI MOJA LA KAMPUNI WANAPANDA WATU WOTE WAKE AU WAUME ZA WAFANYAKAZI NA WATOTO WAO.
    SIKU HIZI ATI TUNATAFUTA MCHAWI WA FOLENI DAR.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2010

    Tuna hoja nyingi nzuri sana lakini ufumbuzi wake uaweza ukawa ni ndoto.Kwa mfano mimi nimeendesha gari Dar(nimejifunzia pia Dar)miaka ya 75-76, wakati ule hapakuwa na traffic lights, barabara ni ndogo zaidi na pia magari yalikuwa kidogo zaidi na watu pia.Lakini pamoja na hayo, tangu wakati ule hadi sasa ni barabara chache sana zimefanyiwa ama upanuzi au maboresho na zote ni zile zinazoanzia nje kidogo ya jiji, kwa mfano Morogoro road, na Ali hassan Mwinyi.
    Kwa mtazamo wangu, naona Watanzania wenzangu tumekosa nidhamu ya utumiaji wa barabara.Wote kwa ujumla wetu,ama hatujui au kwa makusudi hatufuati sheria zinazoongoza watumia barabara mwishowe tunafikia hapa tulipo, si kwa foleni, kwa ajali na hata uharibifu wa vyombo na mali.Nimetembelea nchi fulani ya ulaya nikakuta wanafuata sheria vizuri na hakuna matatizo kwenye barabara ingawa magari ni mengi mno mno-hakuna hata mfano wa kulinganisha na haya ya Dar- na yanakwenda tu hata wakati wa rush hour, hata honi husikii!!
    Cha kwanza tujijengee hiyo heshima ya matumizi ya barabara zenyewe ndiyo tumtafute mchawi alipo. Mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2010

    MHH wanadau naunga hoja!!!ninachoshangaa kuhusu swala la mipango miji ni kuwa pamoja na kwamba Posta ni vurugu bado kuna majengo mapya yanajenga tena yenye ghorofa za kutosha sasa sijui serikali yetu inatupeleka wapi.Kwa kweli namuomba RAIS JK aliangalie swala kwa jicho la pili.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2010

    Hawa wahusika waende wakatembelee mji wa Cairo (Egypt) waone wenzetu wanavyo "plan" mji na barabara zao.

    kwa mfano umbali wa kutoka mjini mpaka bunju ni miji tofauti ambayo huwezi kujua mji huu unaanzia wapi na kuishia wapi. Barabara (including flying overs) ni nzuri na nyingi na magari ni mengi sana lakini hakuna foleni kabisa. Mji mpya ukiwa unajengwa nafassi kubwa ya barabara inaachwa. Kuna haja ya hawa wahusika kutembelea na kujifunza wenzetu wanavyotengeneza miji yao

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2010

    Brilliant ideas Tatizo ni kwamba hatuna Brilliant leaders. Wengi wanaona mwisho wa viganja vyao tu na kwampango huu kama Tanzania hatutaamka na kusimamia hivi vitu tutaendelea kuzungumza tu. Tunaandamana kwa vitu visivyo vya lazima lakini vitu kama hivi hatuandamani. Hebu siku moja tuamue tuzibe njia zote wanazopita viongozi wakuu wa serikali hasa wahusika tunaendesha magari unaenda kuacha hapo wanapopita tukiacha magari kama 50 au zaidi kwenye barabara wanazopita hao viongozi, na mabango yanayoainisha vitu tunavyovitaka/mapendekezo yetu watalazimika kutusikiliza. We can protest without violence people! Hivi ndio viongozi wetu wataamka usingizini.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2010

    TATIZO KUBWA NI MIPANGO YETU MIBAYA NASHANGAA TANZANIA,WAKATI JIRANI ZETU UGANDA WAMESHAJENGA "BY PASS" NA KENYA HIVI SASA TAYARI WAMEANZA KUJENGA,HII INAPUNGUZA SANA FOLENIMTU ALIYE MWENGE,MBEZI BEACH,TEGETA BAGAMOYO ANAENDA MOROGORO AU AIRPORT ETI MPAKA AJE UBUNGO ANAYETOKA AIRPORT ,KURASINI,MGAGALA,GONGO LA MBOTO ANAENDA MOROGORO AU BAGAMOYO AU MBEZI BEACH LAZIMA AJE UBUNGO AU KATIKATI YA JIJI INATAKIWA KUWE NA BARABARA KUBWA KUTOKA KIGAMBONI HADI PUGU HADI MBEZI LUIS HADI MBEZI BEACH AU TEGETA HII ITAPUNGUZA MSONGAMANO KWA KIASI KIKUBWA SANA.NASHANGA WANASIASA WANAONGLEA BARABARA ZA JUU WAKATI DAWA IPO HII KWANZA YA KUWA NA BARABARA YA KUZUNGUKA

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2010

    Mdau ametoa hoja nzuri na uvumbuzi wake. Hapa tunatoa maoni ya kujenga sio kubomoa, je haya maoni yanawafikia VIONGOZI wanaohusika? Je Hatuoni kwamba wakati mzuri ndio huu wa UCHAGUZI ndio tuutumie kuwabana, sio wanataka kura za wananchi, wakizipata na kushinda Uchaguzi wanachokijua kila kukicha kwenda ULAYA, na Kufisadi Mali za Walalahoi. Wengine wapo Madarakani Tangu enzi za TANU hawana wanachokifanya, wanahamishwa Wizara. Kwakuwa Uchaguzi ndio umekaribia jamanii, hawa watu wapewe KITI MOTO (MDAHALO) waulizwe watatufanyia nini, ikiwa moja ya KERO kubwa ni Msongamano wa Magari Dar es salaam. Kama hujatekeleza ulichokiahidi, automatic next Uchaguzi hupewi nafasi yoyote ya kugombea. Hapo Dar Jamani Suluhisho ni KUINTRODUCE CONGESTION CHARGE KUINGIA MJINI AU FLYOVERS. Kwakuwa Makosa yalishatendeka ya Planning hapo kabla, haya bado yanawezekana kabisa. ZIADA JAMANIII TUFIKIRIE KUJENGA UNDERGROUND TRAIN kama ilivyo miji mingine kama London na kwingineko.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2010

    haya maoni ni mazuri.lakini mboni sulusheni ipo nayo ni kuhamia dodoma? hivi kwa nini raisi , waziri mkuu na wizara zote na mengineyo wasihamie dodoma.kila siku wanajenga mawizara hapo dar tu na majengo ya serikali kule magogoni yanajengwa kwa nini wasiende dodoma.kila siku tutahamia tutahamia hadi YESU arudi ndio mtahamia.amia dodoma afu dar uone kama kuna foleni.viari venyewe havifiki hata milioni moja.bado kabisa hatuna magari.yaani nchi nzima magari hayazidi milioni moja nchi ya watu 45milioni.dar hapo mmpo si zaidi ya 4milioni. peleka serikali kule dodoma waache wafanyabiashara hapo dar kwani serikali haihitaji wateja kwani inatoa huduma.
    mipango miiiiingi hamna kitu.

    kijijini mexico boarder

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 24, 2010

    Mkiweza kujibu swali la kwa nini tunang'ang'ania kubanana Dar es Salaam mtaweza kuondoa tatizo la foleni Dar na nchini kwa ujumla.
    Vinginevyo mtajenga miflaiova wee na bado mtakuwa na foleni kuzidi hata miji mikubwa ya Marekani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...