Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Dar es salaam na Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, kwa ajili ya kumtambulisha mgombea huyo pamoja na Mgombea Urais wa Zanziabar kwa Tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanziba kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakiagana na wananchi wa Kisiwa cha Pemba katika Uwanja wa Ndege wa Karume leo, baada ya kukamilisha ziara yao ya siku mbili kisiwani humo ambapo jana Rais wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume aliwatambulisha Wagombea hao kwa Wananchi wa Kisiwa hicho katika uwanja wa Gombani ya kale Chakechake Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2010

    Ivi kwani campeni zimeshaanza rasmi au ccm tu ndio wanaruhusiwa kufanya kampeni kabla ya tarehe ya uzinduzi? Ni swali tu michuzi usiibanie

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2010

    Anon wa Mon Jul 19, 03:01:00 AM

    Kama ulikuwa kichwani kwangu. nafikiri hii si haki ninavyojua mimi huko nyuma wagombea walikuwa wanatambulishwa Jangwani siku ya ufunguzi wa Kampeni.

    CCM ukiwaambia katika hili watakwambia wanambulishwa katika mikutano yao ya ndani lakini mbona hata sisi wa nje tunona wanachofanya?. Kweli kama nchi umeishika none can stop you haya, wanedelee kutambulishana tu maana ndiyo demokrasia hiyo wanayoijua wao, huku Tume ya uchaguzi imekaa kimyaaa kama saa nane usiku vile na kamvua kananyesha kwa mbaali huku ukiwa umezunguukwa na walinzi wanaokufanya usihofu kukurupushwa na majambazi au vibaka. Tendwa naye kimyaa kama yupo mtungini vile.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2010

    hawa jamaa hiyo nchi mnaosema wamepewa na baba mtakatifu nyerere, hakuna demokrasia hapa, isipokuwa mtapata amani na ufisadi tu, swali nyie ccm bendera zenu za ccm zilikuwa zinanunuliwa sweden wakati wa nyerere, haya mashati mnatoa wapi? kama haujakufa utaona mambo!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...