Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Balozi Augustine Mahiga akiwa mwenye furaha akipungua mikono kuwakaribisha mabalozi wenzie katika hafla aliyoiandaa kuwaanga.
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,( Somalia) na aliyekuwa Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Augustine Mahiga akizungumza na Mabalozi wenzie.Sehemu ya Mabalozi na wageni waalikiwa wakimsikiliza Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Balozi Augustine Mahiga aliyekuwa akiwaaga.
Balozi Augustine Mahiga akiwa na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, mara baada ya hafla ya kuwaaga mabalozi wenzie.


Na Mwandishi Maalum

NEW YORK-Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Somalia, Balozi Augustine Mahiga, amesema atafanya kila lililo ndani ya uwezo wake katika kuisadia Somalia kuwa nchi ya amani, usalama na inayotawalika.

“Natambua vema kazi kubwa iliyombele yangu, nina jukumu kubwa, ni kazi ngumu na zito. Lakini ni lazima atokee mtu wa kuifanya kazi hiyo, nami nipo tayari ninachokiomba kutoka kwenu ni ushirikiano, na msaada wa kila aina mtakaoona utasaidia kufanikisha kazi hiyo na hasa nia ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kuifanya Somalia kuwa mahali salama“.

Mahiga ameyasema hayo wakati wa hafla aliyoiandaa ya kuagana na Mabalozi wenzake ambao amefanya nao kazi wakati alipokuwa Mwakilikilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, kabla ya Katibu Mkuu kumpatia wadhafa huo mpya.Hafla hiyo ilifanyika Umoja wa Mataifa.

Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu, akawaeleza mabalozi wenzie kuwa kwa namna hali ilivyotete huko Somalia, Jumuia ya Kimataifa haiwezi kuikwepa na kuitenga bali ni kuisaidia.

“ Nina kwenda kuifanya kazi, na moja ya jukumu langu kubwa ni kuifanya Somalia kuwa moja ya ajenda kuu katika Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, hakuna namna wala jinsi na ni ukweli uliowazi na sote tunajua tutake tusitake hatuwezi kuiacha Somali ibaki kama ilivyo” akasisitiza.

Akaongeza kwa kusema kuwa kwa miongo mingi Somalia imekuwa haina serikali kuu pamoja na kwamba kumekuwako na juhudi za kila aina za kuidia nchi hiyo, lakini mara zote na baada ya juhudi hizo ambazo anasema zimefanyika kwa mara 19 kukamilika, Somalia imejikuta ikirejea tena katika hali ya mchafuko na vita.

Akielezea zaidi hali ya Somalia, Mahiga anasema, sura ya nchi hiyo katika jumuia ya kimataifa ni sura ya nchi iliyojaa uhalifu wa kila aina, mauaji, ugaidi na utekaji nyara na kwamba hiyo si sura halisi ya Somali, kwani ni nchi nzuri yenye raia wema na yenye kila sifa ya kama ilivyo nchi nyingine katika umoja wa mataifa, kinachotakiwa ni kuisaidia.

Akatumia nafasi hiyo kuwashukuru mabalozi hao kwa namna walivyoshirikiana naye katika kipindi cha miaka saba aliyoiwakilisha Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Kipindi anachosema Tanzania kwa kushirikina na Mabalozi hao, iliweza kusukuma mbele mambo mengi ya msingi. Baadhi yakiwa ni mchakao wa Muundo mmoja wa Umoja wa Mataifa, kuanzishwa kwa Kamisheni ya ujenzi wa amani, kuratibu dhana ya ulinzi wa raia kwenye maeneo yenye vita na wajibu wa kuwalinda raia.

Kwa upande wao na wakizungumza kwa nyakati tofauti kila balozi aliyepata nafasi ya kusema, hakusita kuonyesha hisia zake, licha ya kumpa hongera wapo pia waliompa pole na kumtakia kila la kheri kwa kujua fika uzito na ukubwa wa jukumu analokwenda kufanya.

walitabua mchango wake wakati wa uwakilishi wake, wakimuelezea kama mmoja ya mabalozi wenywe uwezo mkubwa mahiri na hodari katika kujenga hoja, kuziwasilisha, kuzisisima na hata kuzitetea, na aliyeiwakilisha vema Tanzania na Afrika kwa umahiri mkubwa, huku wakisisitiza kuwa Jumuia ya Mabalozi imepungukiwa kwa kuondoka kwake.

Wakamuahidi ushirikiano wa kutosha, kwa kuwa wote wanatambua umuhimu wa Somalia si kwa Somalia yeny ewe bali kwa Usamala na amani wa Jumuia ya Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2010

    Africa wakipatikana watu 50 kama hawa wanaongea na kutaka matendo yafanyike basi kweli nchi za Africa zenye vita si Somalia tu zinaweza kusawazisha kwani matatizo ya Africa lazima yakazaniwe na wa AFRICA. Hongera Mjomba fanya kweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2010

    Nukuu katoka katika Paragraph ya 6 "Akaongeza kwa kusema kuwa kwa miongo ishirini, Somalia imekuwa haina serikali kuu"

    Ni miongo miwili (2) ambayo ni sawa na miaka ishirini na sio MIONGO ishirini (20), ambayo ni sawa na miaka 200 jambo ambalo si kweli.

    Naomba Mwandishi Maalum arekebishe upotoshaji huu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2010

    Mzee kila la kheri lakini ukiona wanataka kukudhuru wewe rudi haraka Bongo

    Observer

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2010

    Nakumbuka ni juzi tu hapa Waziri wetu wa mambo ya nchi za nje Bw. Membe alitoa kauli yenye kutia huzuni kwamba " Somalia ni nchi iliyolaaniwa"

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 19, 2010

    ni kwamba ni mchapakazi hodari,ndo maana kahamishiwa somalia???

    sielewi mnieleweshe!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 19, 2010

    Huyu mzee anafaa kuwa president. Kwanza yuko very presentable. Halafu ata ukimuona unajua nchi iko kweny good hands. 2015 itabidi tumuombe achukue fomu.

    Alafu ametulia sana. Hana makeke wala majivuno au kujionyesha kwenye michuzi kila siku kama mabalozi wengine!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 20, 2010

    This is an asset of the United Nations. Huyu jamaa iko kichwa safi kabisa. Naunga Mkono agombee Urais 2015. Na iko na experience nzuri sana katika mambo ya multilaterals. Hatanii.Is a serious man. Hongera Dkt. Mahiga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...