Na Woinde Shizza,Arusha.
WANACHAMA 12 wa Chama Cha Mapinduzi, wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania ubunge katika majimbo ya Arusha mjini, Arumeru Magharibi na Arumeru Mashariki.
Walichukua fomu hizo kwa nyakati tofauti katika ofisi za wilaya za Chama Cha Mapinduzi na wanatakiwa kuzirejesha kesho zikiwa zimekwishajazwa kikamilifu.
Katika jimbo la Arusha mjini, waliochukua fomu ni Dk Batilda Burian ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Khamis Kibola, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Umoja, Deo Mtui, Michael Sekajimbo na mbunge aliyemaliza muda wake, Mh. Felix Mrema.
Mapema baada ya Dk Batilda kuchukua fomu zake na kutoka nje ya ofisi baadhi ya wanawake waliokuwa wamefika ofisini hapo walianza kushangilia na kumpongeza suala ambalo lilimlazimu Katibu wa Wilaya wa CCM, Salum Mpamba kutoka nje na kuwaonya.
Aliwakumbusha kuhusu kanuni ya kutofanya sherehe kwa mgombea ye yote aliyejikeza kuwania nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea.
Kwa upande wake, Dk Batilda aliwashukuru akina mama hao kwa kumwezesha ambapo walichanga jumla ya sh. 168, 000 za kuchukulia fomu.
Katika Jimbo la Arumeru Magharibi, waliojitokeza kuchukua fomu ni Goodluck Ole Medeye, mbunge wa zamani Elisa Mollel na Edward Ngoseki ambaye ni afisa elimu wa wilya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wa Jimbo la Arumeru Mashariki, waliochukua fomu zao ni Jeremiah Sumari ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Elirehema Kaaya ambaye ni Ofisa Mifugo wa Mkoa wa Mwanza na Anthony Musani ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Leuguriki.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arumeru, Anna Mwiteni ndiye aliyewakabidhi fomu hizo wanachama wanaomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi za ubunge.
Baada ya kuchukua fomu, Medeye alisema amechukua fomu ili kutimiza azma yake ya kuwania ubunge.

batilda unayo kila sababu ya kuchukua jimbo la arusha mjini,watu wamemchoka felix mrema,mbuge gani anayekaaa marekani zaidi ya tz,hajawahi kuchangia bajeti haa moja,mbungeni yuko kimya,na akirudi arusha yuko busy na mashamba yake ya maua.utapita kirahisi sana,mayb hamisi kibola ndo atakuwa mshindani wako na sio mrema.
ReplyDeleteDR. Batilda Buriani is the best candidate without a doubt for Arusha mjini, all the best!!!
ReplyDelete(US Blogger)
Kaka yangu mpendwa Dr Hamisi Kibola chonde chonde muachie dada yetu usimwekee kiwingu kaka. Tuna imani na Dr. batilda kwani ni dada yetu amekulia hapahapa. Dr. Kibola mpe tafu dada aweze kupeperusha bendera ya arusha bungeni. Tutakupa 2015 kama hutajali kwani nawe ni wahapahapa. Kwako Dr. Batilda nasema HATS OFF..kipenga kimeanza, Rabbi akuongoze katika mafanikio katika kinyang'anyiro hiki na kila mpinzani Rabbi amfunike macho yake upite salama.
ReplyDeleteDr. Kibola ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania ambayo inaanzisha na kuendesha mifuko mbalimbali ya Uwekezaji wa pamoja ukiwapo UMOJA FUND,WEKEZA MAISHA,WATOTO FUND NA JIKIMU FUND.
ReplyDeleteAmekulia Arusha,ana maono ya kutusaidia wanaarusha.He is the best candidate.