Mheshimiwa Balozi Mwanaidi S. Maajar, akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Balozi, Bwana Chabaka Kilumanga kwa niaba ya Maofisa na Wafanyakazi wote wa Ubalozi - London.
Mheshimiwa Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akiongoza kikao chake cha mwisho na Maafisa Ubalozi London kabla ya kuanza safari ya kuelekea Washngton DC alikohamishiwa kikazi. Vikao hivi vya kikazi kati ya Balozi na Maafisa wake vimekuwa vikifanyika kila wiki toka Mheshimiwa Balozi alipowasili kituoni hapo mwezi Septemba 2006. Agenda ya vikao hivi kupeana taarifa za maendeleo ya majukumu ya kila siku Ubalozini hapo. Hii imesaidia sana kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa umoja kama mabaharia wawapo chomboni. Tunamtakia kila la heri Balozi Maajar katika majukumu yake mapya huko Marekani.
Maofisa ubalozi katika mkutano huo
Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania – London kwenye picha ya pamoja na Mheshimiwa Balozi Mwanaidi S. Maajar. Kutoka kulia ni Kanali Penegreen Mrope, Bwana Clement Kiondo, Bwana David Nginila, Mheshimiwa Naibu Balozi, Bwana Chabaka Kilumanga, Mheshimiwa Balozi Maajar, Dada Caroline Chipeta, Bwana Sylvester Ambokile, na Bwana Allen Kuzilwa.
Mheshimiwa Balozi Mwanaidi S. Maajar akijumuika na wadau kwenye mnuso wa kumuaga rasmi
Afisa ubalozi Bw. Amos Msanjila akiwa na wadau katika mnuso wa kumuaga rasmi Mheshimiwa Balozi Maajar
Wadau wakijumuika pamoja kwenye mnuso wa kumuaga Mheshimiwa Balozi Maajar
Wadau katika mnuso wa kumuaga rasmi Mheshimiwa Balozi Maajar








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2010

    Tukitoa Maoni Hamyaandiki. Mnataka wote tuwe tunatoa hongera tu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2010

    ivi huyu mama mbona anaagwa mwezi mzima jaamani si aende uko akaendeleze kuiuza nchi tunajua kwanini anapewa hizi nafasi..na ankali kubania ni jadi yako unaogopa maskadi ya wanasiasa

    ReplyDelete
  3. msemakweliJuly 02, 2010

    Wala sisemi chochote mana juzi nilicomment hukutoa kwa hiyo habari za huyu mama usiziweka mana tukitoa maoni ya kweli huyatoi. nikweli ni mwezi wa tatu huu anaagwa sijui anahisi Matawi aliyofungua hayajatosha????????? nafikiri mmenielewa. Mana nikitaja hapa hamtaiona hii comment.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2010

    Mheshimiwa kama utapata ujumbe huu naomba mara moja utulie kwenye nji ya Obama, kama bado unapapenda ukerewe bora si ungeomba ubakizwe huko.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2010

    Huyu Nae kazidi kuagwa Jamani..hebu akafanye Kazi eti...ebo...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...