Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, imesema nusu ya watu waliokwenda kupima vinasaba (DNA) kutokana na kuwa na mashaka haya na yale, vipimo vimeonyesha kuwa si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Vifaa na Matengenezo wa ofisi hiyo, Emmanuel Gwae, wakati akizungumza katika maonyesho ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema tangu huduma hiyo ianze kutolewa na taasisi hiyo mwaka 2005, watu zaidi ya 2,000 walifika kupata vipimo kujua uhalisia wa watoto wao.
Alisema karibu nusu ya watu hao waliofika na kupimwa ilibainika kuwa watoto waliokuwa nao hawakuwa wa kwao.

Alisema idadi ya watu wanaokwenda kupata vipimo imekuwa ikiongezeka kuliko miaka iliyopita.

“Huduma hii ni kama imechelewa maana watu wanakuja kwa wingi sana kupima uhalisia wa watoto wao na wengi wanaopimwa wanakuta watoto si wao,” alisema.

Alisema kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha matokeo hayo ikiwemo kubadilishana watoto wakati wa kujifungua.

Alisema katika hospitali zenye mlundikano mkubwa wa wanawake wanaojifungua, baadhi ya wanawake kwa makusudi wanaweza kuwabadilishia wenzao watoto.

Alisema hali hiyo pia inaweza kutokea hata bila kukusudia kutokana na mazingira ya hospitali.

Alisema vipimo vya DNA hugharimu shilingi 300,000 na mhusika anaweza kupata majibu ndani ya wiki moja.

Alisema kabla ya mhusika kwenda kupata vipimo lazima apeleke kwa mkemia barua kutoka mahakamani, kwa wakili au ofisi ya ustawi wa jamii na kueleza sababu ya kutaka kupima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2010

    Michuzi acha kubania maoni bwanaaa! Ah! hadi inaudh. na hii basi bania ufurahi wewe...

    Unajua huyu JK ni memba wa saigoni. Na wana saigoni wote watoto wa mjini. Alipoingia madarakani watu wa kuja kibao walijishebedua kumsaidia aingie madarakani, wao wakijua akiingia Ikulu, mambo yao yatakuwa swafi. Maskini wakuja hao. JK alipoingia Ikulu tu akawapiga stop maswahiba wote. Akawaambia jamani eee nchi sasa ni yetu, na tuijenge. Wakaona he, huyu mkwere vipi tena. Sie tumemsaidia kuchukua nchi ili tuile yeye analeta za kuleta, chuki zikaanza. Wakaanza kumpakazia oooh hafai, simply kwa kuwa hakutaka kula nchi kama walivyotaka wao.

    Hii ndio sababu ya yote haya. wakuja wanafanya kampeni JK aonekane hafai simply kwa kuwa kawatolea nje. kazi zimekuwa haziendi ili aonekane zoba. Mkwere naye kagangamara. hasikii la nani wala nani.

    Kwa taarifa yao ni kwamba JK ni raisi pekee ambaye hana skendo hata ya kusingiziwa. mkwere wa watu hajachota thumni ya mtu wala nini. anapeta tu. na kila wanavyompakazia yeye ndio anazidi kupanda chati. wananchi wanampenda na safari hii watampa kura zaidi ya asiimia 80 ashinde kwa kishindo.

    Haya, mzee wa kiraracha mrema nayekaingia kichwa kichwa na kuwaumbu wapinzani kwa kuweka hadharani mamabo ambayo wapinzani wanashadidia. mwenye macho asikie na mwenye masikio aone. Hakuna kama JK nji hii. Mrema oyeeeeee! ila huko Vunjo nadhani kanoa stepu, angeikngia kwa gia ya CCM angepeta tu.

    yetu macho
    Mdau Kigambonino...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2010

    Hii mbona inajulikana Tanzania. Wanawake sio waaminifu hata kidogo. Hasa vigogo wanalea watoto wa watu wengine tu, na vigogo wengine watoto wao kibao Uswazi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2010

    Yaani professional persona mzima anasubutu kusema hadharani kuwa either takwimu ni kubwa hivyo kwa vile watotot wanaweza kubadilishwa hospitalini??? That is very low!!! Atawafanya wanawake wafie nyumbani kwa kujifungua kwa kuogopa kuzalia hospital wakijua kuwa kuna chance ya watoto wao kubadilishwa... kwanza ana uhakika gani mapaka aseme watoto wanabadilishwa hospitalin?? Angekua nchi za wenzetu huyu mtu wangemsue kishenzi kwa kupotosha reputation ya hospital zao.....Ahhhh

    Kama ni rahisi kubadilishiwa mtoto kama anavyosema basi itakua rahisi hivyo hivyo kwa hayo maabara kutoa matokeo ya uwongo...Inawezekana 50% ya hao walioambiwa watoto sio wao ni wakwao kabisa bali majibu yamechangwanywa changanywa tu...

    2 Kama ametambua kuwa mtoto anaweza kuwa switched at birth akishaona kuwa mtoto sio wa huyo mwanaume je wanampima na mama mwenye mtiootot kuona kuwa ni mtoto wake...kama ndio je wameona ni mwangapi amabao sio watoto wao? kama hawafanyi hivyo basi asije na habari zake za kusema kuwa inawezekana kuwa watoto wanabadilishwa wakizaliwa.... wowote,

    Mimi naona kuliko kuwa na barua tu ya mahakamani pia wangetakiwa kuwa na professional counselors. Wanaweza kuharibu maisha ya watu kwa DNA ambazo hata kwa wenzetu saa nyingine huwa wanafanya mara mbili mbili na kutumia sehemu tofauti kabla hujafikia conclusion. .

    Hapa na hii kitu either wanaweza kuharibu maisha na familia za watu. Na kufanya wababa wakimbie watoto wao na vipimo visivyo na uhahikia au kama ni kweli 50% ya waliopimwa watoto wamekutwa sio wao basi ndio maana ukimwi umetumaliza Africa....

    Mama wa nyika

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2010

    NANI KA KUAMBIA KIKWETE AJALA NCHI, KALAGABAO.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 11, 2010

    huyu mtaalamu wa dna hivi ana akili nzuri hayo ndo mafunzo aliyopewa kutowa siri za wateja?????????? hovyoooooooooo, aondolewe kwenye kitengo hicho hafai.

    ReplyDelete
  6. Mdau hapo umezungumza point kweli , @ Anonymous said... Mimi naomba Mungu apite tena awamu hii ili awamalize mafisadi wote,.

    ReplyDelete
  7. Hii inawastua wasiojua takwimu tu. Hizi ni kesi ambazo zilikuwa na utata tayari. Si kweli kuwa 50% ya watoto wote Tanzania hawana baba wa kweli. Kitakwimu tunasema hii sample si "representative of the Tanzanian kid population"

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 11, 2010

    finaly.safi saana,wababa wanayo haki ya kujua kama watoto na wao kweli hasa unapotia mashaka mana mhh,awmama naowamezidi kusingizia hasa wakiona jamaa anavijihela na mengineyo.amkeni kinababa mjue haki yenu.ha!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 11, 2010

    swala zima la kusaidia kinamama hasa sekta ya uzazi LILMEDORORA mno sijui serikali inafikiria nini kila siku ni hadisi kusaidia kina mama na watoto afu hawatimizi.
    Hayo maelezo ya DNA ndo yanaprove km serikali imelala bora mama awe kicheche kwa kuzaa na 2m mwingine apart frm mumewe kuliko kubadilishana watoto huu ni uzembe mkubwa sn sn sn na nikwasababu hospitali eti imejaa Serikali iko wapi jamani??????????

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 11, 2010

    Sasa michu hiyo comment ya kwanza hapo inauhusiano gani na habari za DNA?
    Any way,hapo ndio mjue mtoto kwa aslimia kubwa huwa ni wa mama,wengi wanabambikiwa tu hasa kwa wale wenye mademu vicheche(Mabwana lukuki).

    ReplyDelete
  11. Hakuna chochote hapo jamaa wana njaa tu ya pesa wanatafuta pesa tu.Eti wanadai waliopima wote wamegundulika watoto sio wao wewe ukisikia hivyo si mzee unahamasikia maramoja kwenda kupima then unawalipa kilo tatu zao alafu baada ya hapa wanakuita mlango wa nyuma usema kuwa mtoto sio wako kutokana na vipimo ili waeendelee na unyojaji wao[watanzania tusisahau wahenga walisema KITANDA HAKIZAI HARAMU].Mimi napiga hili zoezi na wale wote walioenda kupima au wanaotaka kupima [najua wengi watukuwa ni wa baba] wanajidhihirisha hadhari kuwa hawajiamini.Kaka michuzi watu nje wanatumia DNA kufanya research za maana sisi huku na serikali yetu ilivyo ya kiipuuzi inatumia DNA kuvunja ndoa za watu--jamani kweli tutafika.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 12, 2010

    Jamani ninavyojuwa nchi yetu Tanzania imepiga hatuwa sana kwenye mambo ya uzazi, ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika karibu na sisi, Ndiyo maana nyerere alianzisha dispendary kila mahali, sasa kama kijiji chako hakina hata dispensary nadhani ni kazi yetu wananchi kuangalia ni jinsi gani ya kusaidia serikali ituangalie. Hili suala la watoto wasio na baba halikuanza leo angalieni nyie wakina baba mliopo kwenye mtanda angalia wewe mwenyewe tabia yako, tabia ya baba yako, tabia ya babu yako. Mila na desturi zetu tumezitupa wapi? wanwake kila siku wanonekama victim katika kila jambo, huyo baba aliyekuwa namyemelea huyo mama yeye hana hatia? Kwa mfano ni familia gani ambayo haina wajomba ambao baba zao hawajulikani, na inabidi uzaidie hao wajomba kwa kila kitu, lakini watu wanajisahau kwamba wanmajukumu lakini utwawakuta wankwenda kuendela na tabia nje ya ndowa zao. Kwa hivyo mzunguko unaendela.Tunamshukuru sana Mwal nyerere kwa kuanzisha shule nyingi za akina mama, wakina mam wengi Tanzania wameelimika sana siku hizi. Familia zetu siku hizi zimesambaratika na kama familia haipo pamoja, hata taifa linayumba pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...