Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakichota mabaki ya mafuta kandokando ya bahari ya hindi katika eneo la Posta ya zamani yaliyomwagika toka kwenye meli ya mafuta leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2010

    kweli hali ngumu !! At all that mnaenda kuwapigia walewale kura !!hapo mi ndo siwaelewi watanzania !!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2010

    kaka angalia wasikucharaze vibao na kikamera chako!! watu wana njaa zao wewe una watoa toa kwenye kamera

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2010

    inasikitisha nadhani hawaelewi hatari iloyowopo hapo incase of fire

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2010

    Yale Yaleeeeee...halafu atatokea mvuta sigara hapo wote wanalipuka....jamani waonyeni hao watu....hicho ni kifo....vitu vya dezo vina madhara yake..

    ReplyDelete
  5. Nabii Yohana Mashaka Yoweli Kaguta MuseveniJuly 26, 2010

    HII NDO MAANA MIMI NATAKA KUHAMA BONGO KULUDI MALEKANI YA WOLSTRITI. WATU HAWANA AKILI VILE, SASA HUU NDIO UPUUZI GANI?? NDUGU ZANGU WASUBILI TU HAYO MAFUTA YALIPUKE NDO WATASHIKA ADABU. MIMI NITAANZA KUANDIKA MA NONDOZZ KALI KALI ILI HAWA WATU WAKOME. AISEE

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2010

    Jamani sasa hayo mafuta kwenye vikopo vya Uhai wanakwenda kuuza?? Ama kweli watu wanaishi chini ya dola moja kwa siku!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2010

    Jamani wanasafisha "Oil spill" hao, mbona wale wa Gulf Coast USA hamuwaandami?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2010

    KAKA MICHUZI HUYO COACH MPIYA WA TAIFA STARZ UPO WAPI?? AU NDO BILA BILA

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2010

    Meli inachafua mazingira hamna anayewajibishwa tunabakia kuwaandama wananchi masikini.Kampuni inayohusika na na hiyo spill iwajibike wakati wa kuchekeana umeisha!Tanzania wake up!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2010

    Yule jamaa mwenye kofia si askari wa security guard?? Na yeye anachota mafuta ya bure tena kwenye chupa ya uhai ya nusu litre?? Halafu atayauza kwa Tshs. 500/= kwa wenye daladala!! Kweli bongo tambarare. Kwa wewe anony hapo juu unaposema bado mnawachagua, kwa hiyo serikali ndiyo iliwaambia waende kuchota mafuta?? Hata kama wasipowachagua hao walio madarakani, matatizo yetu ya Africa ni mengi. Lakini pia watu hawafanyi kazi. Wanabaki kulalamika tu. Je serikali ifanye nini sasa?? Vijana wako mitaani tu wakati ardhi kibao huko vijijini. Uzalishaji umeshuka kwa asilimia kubwa sana kwa sababu watu hawafanyi kazi. Chukulia mfano Zambia, waliacha kuichagua serikali iliyokuwa madarakani hali ndiyo mabaya zaidi kuliko pale awali. Kenya waliinyima kura serikali iliyokuwa madarakani, je hali ikoje? Malawi?? na nchi nyingi tu za Africa. Mchawi sio serikali iliyo madarakani bali ni sisi wenyewe. Ni wavivu na tunabakia kulalamika tu!! Unalalamikia serikali wakati kila siku unazurura tu. Jamani tuzalisheni mali ili uchumi wetu uongezeke!!
    Mdau

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2010

    Nishati kweli nishai, afande kaacha lindo aisee!

    ReplyDelete
  12. Sitaki kura za WafanyakaziJuly 27, 2010

    Maisha Bora kwa kila mtanzania

    ReplyDelete
  13. Unajua viti kama hivyo vikionekana inashauriwa kuwaarifu wana usalama, na kweli ni wanausalama watahakikisha usalam unakuwepo

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2010

    HAKUNA BWANA NI SERIKALI YETU NZEMBE!! KWANI INASHINDWA KURUDISHA VIJANA WAKALIME? IPITISHE NGUVU KAZI, ASIYE NA KAZI HATAKIWI MJINI, AU HAPO HAPO MJINI SERIKALI IWAPE VIJANA KAZI, FUFUA VIWANDA, HATA UPANDAJI MITI NA MAUA, SIO MPAKA KUWE NA MIKUTANO YA KIMATAIFA NDIO KUONEKANE MITI JAMANI??? VIJANA WAPAMBE MJI, FUKIA MASHIMO, SAFISHA MITARO, PAKA RANGI MAJENGO YA WASIOJIWEZA, N.K, NA WAKILIPWA VIZURI WATAFANYA KAZI YOYOTE MJINI HAPO.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2010

    Uchafuzi kama huo ungetokea marekani, hiyo kampuni lazima ingefilisiwa, na waziri anayehusika na usalama wa vyombo vya majini kufukuzwa! Kwetu, issue ni kuchota mafuta kwa ajili ya kuwashia vibatari!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 27, 2010

    Tusidanganyane. Hata ukiita walinda usalama kwenye tukio kama hilo nao wanaweza wakachota mafuta baada ya kuzuia watu kusogea katika enelo la tukio. Kuishi chini ya dola 1 sio mchezo. Kikwetu tunasema hata ukilala still "kutakucha na kuchwa"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...