Skauti kutoka nchi mbalimbali duniani wanakutana Nairobi Kenya katika kambi maalum ijulikanayo kwa jina la Rover Moot au Jamboree ya Rova.

Rova Skauti ni kundi la maskauti wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, na hii Jamboree ya 13 ya Rova ya Dunia, na pia ni Jamboree ya kwanza ya kimataifa kufanyika katika bara la Afrika,

Nchi wanachama zipatazo 160 zimepeleka wawakilishi wake katika Jamboree hiyo na Tanzania ikiwemo.

Tanzania imepeleka Rova Skauti wapatao 7 kushiriki katika Jamboree hiyo.

Majina ya Rova Skauti hao pamoja na sehemu wanazotoka ni kama ifuatavyo:-

1. Bahati Japheti Uwino – Mbeya
2. Stanford F. Kazingo – Mwanza
3. Julius Kamili – Arusha
4. Aristeric Herman – Arusha
5. Wakasyuba Deogratias Katundu – Dsm
6. Amina Maulidi – Dsm
7. Mercy Mtei – Dsm
8. Fredrick Peter Nguma – Dsm ambaye pia ni Mkuu wa Msafara huo.



Kambi hiyo ya siku 10 inaanza rasmi leo tarehe 27 Julai 2010 na itamaliza tarehe 7 Agosti 2010.

Wakiwa nchini Kenya washiriki wote watapata nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali na kufanya kazi za ujenzi za kujitolea katika miji mbalimbali ya Kenya.

Washiriki wote watashiriki pia katika midahalo, semina na kongamano zitakazo jadili masuala mbalimbali yanayohusu vijana na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya Rova Skauti kutoka nchi za Brazil, Hungary, Slovakia na Australia wameomba kutembelea Tanzania baada ya Jamboree hiyo kwa madhumuni ya kupanda mlima wa Kilimanjaro na kutembelea mbuga zetu za wanyama. Shughuli ambayo itaratibiwa na Chama cha Skauti Tanzania.

Imetolewa na:

Laurence H. Mhomwa.
KAMISHNA MKUU.
Simu: 0715019288 / 0784737230
Email: tscouts2002@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2010

    Mimi nina swali, hivi siku hizi vyama vya Msalaba Mwekundu na Scout vimekuwa ni vyama vya dini zote? Manake mimi ninavyoelewa vyama hivi vilikuwa ni vya ki kristu. Siku hizi naona hata viongozi wake ni wa dini mbali mbali. Anayefahamu naomba anieleweshe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...