mafundi wakipaka rangi kivuko-pundamilia barabara ya azikiwe avenue jijini dar katika sehemu ambayo tuta lake limekatwa bila shaka kuwezesha wapitao kwa miguu wapite kwa usalama na magari yakatishe badala ya kuzunguka hadi picha ya bismini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2010

    Akili si hiyo, palikuwa panaboa sana hapa

    ReplyDelete
  2. Kaka,

    Kama una kumbukumbu nzuri utakumbuka hapa zamani miaka ya 1970s na 1980s palikuwa na PENGO hapo na magari yalikuwa yanakatiza hapo, baadae pakaja kuzibwa kwa maelezo ya kwamba palikuwa panasababisha ajali.

    Sasa tumerudi tena nyuma na kupazibua tena. Sijui zile ajali zilizokuwa zinaepukwa itakuwaje sasa!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2010

    Hapo sawa ila utiaji huo wa rangi ya pundamilia si sawa kwani baada ya siku 2 rangi inafitika na sisi wajaji wa waja leo kuondoka leo tujapo tena wakati rangi ishafutika itakuaje jamani?
    Afu hapo ni bora mkaweka traffic light hapo baadae.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2010

    yaani mi sijaelewa ndo leo wanajua kwamba ukiweka pundamilia inasaidia watu kuvuka bila kugongwa.Pundamilia zimekuwepo toka lini jamani!!its such big shame for this country!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2010

    watu wa mipango miji wako wapi miaka yote, utafikiri hamna watendaji kazi(lazima tunao wasomi wengi) kushughulikia mambo haya na mengine ambayo ni kero, au ni sababu afisa mifugo anaweza pewa uwaziri au ukuu fulani kwenye mambo ya masoko, na engineer akawa kwenye elimu au nyingine nyingine, lah

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2010

    hapa wamecheza step ya maana sasa watatue na foleni maeneo mengine jijini

    ReplyDelete
  7. Mmmh, wazo zuri, akili zaidi ni KUKIONDOA kituo cha Daladala hapo Posta Mpya kabisa(na zile Taxi ubavu&mbele ya NSSF HQ)! Sijui waombe nafasi Gymkhana kuwe na main stand ya mjini?
    Ngoja nikajaribishe kuingia kulia hapo kutoka Imalaseko! Duh!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 26, 2010

    Ni kweli.nadhani haya ni miongoni mwa maamuzi ya maana kidogo,lazima vitu vingine viendane na hali halisi na wakati uliopo kwa sasa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2010

    Nukuu "tuta lake limekatwa bila shaka kuwezesha wapitao kwa miguu wapite kwa usalama"
    Hio si sahihi

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 26, 2010

    Hapo panahitajika round-about ili kupunguza ajali. Kwa mtaji huu wa kukurupuka na kukata tuu, subiri tuone hao jamaa wanaotokea Imalaseko kuingia kulia wanayogongwa na madaladala..

    mzozaji.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 26, 2010

    sasa haya si ndio mawazo yaliyotolewa na MZALENDO wiki iliyopita?

    namuunga mkono kuwa ile round about iondolewe wahamishe ile sanamu then waweke taa pale

    ReplyDelete
  12. hakuna lolote ajali zitaendelea kutokea sababu waendesha magari aka madereva wetu hawafuatilii sheria/kanuni za barabarani.Pundamilia walikuwepo tangu "KAMATA na UDA" na bado ajali zilikuwepo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...