Mwenyekiti wa TLP Mh. Augustine Lyatonga Mrema akishangiliwa na wana CCM kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho Kizota, Dodoma

Uzuri wa ndege manyoyaaaaa
Uzuri wa CCM seraaaaa
Huu ni ujumbe wa Khadija Kopa akimfagilia Mheshimiwa Lyatonga Mrema, mwenyekiti wa Chama Cha TLP alipofungua moyo wake akimmwagia sifa kede kede Mwenyekiti wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete.

Hapa sasa hivi Lyatonga Mrema anatoa salamu rasmi kutoka chama cha TLP na kuwasema wale wanaosingizia katumwa na wana CCM wakome.

Anashangiliwa na wana CCM kwa nyimbo na vigelegele, anasema kwamba CCM haikamatiki. CCM Chama Kubwa, amesalimu amri. Kwani mwaka 1995 alishindwa, mwaka 2000 aligaragazwa na Mh. Mkapa, na mwaka 2005 ndio kabisaa Kikwete akammaliza. Hivyo CCM ni chama imara, hakishikiki. "Kweli CCM inagaragaza upinzani".

Mheshimiwa Mrema aliongeza, "Kila mwaka wa uchaguzi inakula kwangu, sasa nimechoka" anasema Mrema kwa hamasa huku akiendelea kusifia CCM na uongozi wake.

Kwa maneno yake amesema, hana sababu ya kuacha kumsifia Rais Kikwete kwani ndiye Rais pekee anayemjua. Amefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka mitano hususan katika harakati za kupambana na ufisadi na mafisadi nchini.

Amekiri ya kuwa katika marais wengi waliopita , Kikwete ni mthubutu na mtekelezaji. Anaumia roho sana kusikia kuna watu wanaombeza ati hajafanya lolote hivyo wamtose.

Mrema amewasuta wote wanaobeza maendeleo ya serikali ya Rais Kikwete na amewaomba wana CCM waendelee kumsaidia ili afanye vizuri zaidi. Hapo Mrema alishangiliwa sana kwa nyimbo za CCM na kusindikizwa na bendi ya TOT.

Mrema amemaliza kwa kusema ya kwamba anafuata wosia wa baba wa Taifa na hivyo atagombea ubunge Vunjo kupitia chama chake cha TLP.

Mwenyekiti wa CCM amemshukuru kwa kuwa mkweli lakini amemuhakikishia ya kwamba hata wana CCM watakwenda huko VUNJO na watakutana tena.

Mambo moto moto hapa Kizota, salamu zinaendelea. Picha zinakuja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2010

    kusema ukweli kikwete amefanya mambo mno sema kuna watu hawataki kukubali tu kisa chuki binafsi,hebu tuweke mambo alofanya kikwete kwenye kipindi cha miaka mitano,kwanza barabara ni nyingimno,tukitaja huku hatutomaliza,na nyengine ambazo ziko katika matengenezo kama minjingu babati,arusha namanga,tanga horohoro,babati singinda.barabara za dar,kilwa,samnujoma,shekilango na nyengine kibao,shule ndo halina ubishi,nyumba za polisi za kisasa kabisa,nyumba za jeshi la wananchi,benki ya wanawake tanzania,ni benki ya kwanza africa mashariki na kati,chuo kikuu dodoma,na vyuo 2 vilivyokuwa hatua za mchakato,chuo kikuu cha utalii dar,na chuo kikuu cha wanyama pori arusha,machinga complex,mabilioni ya jk,muhimbili inazidi kubadilika na kutanuka.ameingia madarakani serikali inakusanya bilioni mia na tisini kwa mwezi leo bilioni mia 375 kwa mwezi.kama madafu kuanguka marais wote wamerangusha madafu,mwinyi kaondoka dola mia elfu 64,baada ya miaka 10 mkapa kaondoka dola mia laki na 19.piga kazi JK,anachukiwa obama itakuwa wewe

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2010

    unacheza na itikafu?!
    na bado yatakutoka kuliko hayo kama ulosomewa ya mbayana!

    ReplyDelete
  3. now i belieave that we dont have a genuine opposition party in tz, wote wababaishaji tu.
    we will never see any other party take over the country beside ccm for the next 50years mpaka hivi vizee vyote vya upinzani na vya ccm vife....
    nawakilisha Southeast USA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2010

    Njaa jamani ni mbaya. Si mchezo angalia Mrema alivyochoka. Sasa anamwaga sifa sizizokuwepo kwa CCM. Njaa inaadabisha, si mchezo. CCM Oyee!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 11, 2010

    Watanzania wajiulize, is my living standards better today than it was 5 years ago? Na kama jibu ni yes, basi mpeni Kikwete kura. Hayo ya kusifia ujenzi wa Machinga complex ambayo aliingia mamlakani akakuta karibu inamalizika, na barabara, ambazo nyingi planning yake ilianza kufanywa wakati wa Mkapa ni upotoshaji mtupu. Is life better today than it was 5 years ago? That should be the yardstick.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 11, 2010

    JANA NILISEMA SIASA ZA BONGO ZINABOA NDIO KAMA HIVI,VINYONGA KILA KONA HATA UMUONE WA BROWN, KIJANI LAZIMA ANAYO. NJAA TU INAWASUMBUA WANA SIASA. HAKUNA VYAMA VINGI ILA KUNA RANGI NYINGI.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 11, 2010

    Hizi ndio siasa tuzitakazo,kwa siasa sio hila na gilba bali kuwa pamoja pale panapostahili,kwa mfana kusifia mazuri na kukosoa mabaya.Mrema amafanya haki kabisa siasa sio chuki ,siye wote tuko kwenye boti moja,tukitoboa boti tutazama wote.Napenda pia nimsifu sana Vuai Nahodha kaw hotuba yake yenye bashasha tele haswa pale aliponuku semo mbali2 wa wanafalsa kama Mjomba Mpoto,hakika Karume umefanya sana kazi Zanzibar haswa kuondoa chuki ya kisiasa kati ya CCM na CUF kwa hili utakubukwa daima.kwani ilikuwa ni kero sana huko Znz.Hakika Vuai alipokuwa akikusifia chozi la mwanaume lilikuwa likimtoka jabari huyu,hiyo ndio siasa sifia panapastahili kosoa panapohusika.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 11, 2010

    Mrema ni CCM hiyo mbona najua tangia bado ni mtoto mchanga. alikuwa anakuja sana kwa marehemu babu yangu enzi hizo za nyerere na mwinyi..wakati babu yangu alikuwa mkuu wa mkoa wa Tanga nadhani..mrema, mama maria nyerere, mwl...n.k
    mdau,
    US

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 11, 2010

    Nyie mnashangaa leo? Mbona Mrema bado anapokea paycheck pale Makumbusho?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 11, 2010

    Hatukatai ni kweli kabisa kikwete amefanya kazi yake, lakini kwa Mrema wa chama pinzani TLP asifie CCM, it doesnt sound right. Kwanini aende kusifia chama pinzani kama na wao wanatafuta kura hizi hizo kwa wananchi..?? Hii inaonyesha kama kuna unafiki hivi,labda ye ni TLP kanyaboya, ni mwanacha wa CCM kisiriri ...aaaghghhh, wanawafanya watanzania mazuzu..hawaezi kuchambua...inasikitisha. Viongozi wa vyama pinzani they need to be genuinesi fake kama mrema.

    ReplyDelete
  11. Aliekuwa Mdhamini wa MremaJuly 11, 2010

    ni kweli CCM chama hatari hakuna kinachomfuatia kwa karibu.

    CCM ndio chama pekee kilichopunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito vinavyoongezeka kila kukicha.

    Ndio chama pekee kilichopunguza vifo vinavyosababishwa na ajali zinazoongezeka kila siku nchini.

    Ni chama pekee kilicho hakikisha mikataba hewa inasainiwa na mafisadi kuhakikisha tunapata umeme masaa ishirini na nne kila siku ya wiki.

    Ni chama pekee kilichohakikisha kuwa wachimbaji wamadini kutoka nchi za nje wanakamua dhahabu asilia na kuisafirisha nje ya nchi kwa kulipa ushuru mdogo ama kutolipa kabisa.

    Ni chama pekee kinachohakikisha vijana na wahitimu wote wa vyuo nchini wanapata ajira.

    Ni chama pekee kinachosimamia mfumuko wa bei kiasi kwamba mfumuko wa bei umekuwa mkubwa kupita nchi yoyote ile ya East Africa.

    Ni chama pekee kinachowajali wananchi wake kwa kuhakikisha maji safi yanapatikana kwa kila mtanzania

    Ni chama pekee kinachoweza kuchukua risk na kupuuza maoni ya watanzania kujiunga na soko huru la EA ingali kikijua kuwa halina manufaa kwa Tanzania.

    CCM ni chama kizuri kinachopambana na shida za mlala hoi wa kila siku hasa mijini kwa kuhakikisha foleni kwenye mabarabara yetu inaongezeka kila siku masaa 14 siku ieende.

    Ni Chama Pekee Duniani kilichohakikisha kinaboresha elimu ya vijana wa nchi hii kiasi kwamba zaidi ya asilimia 80 wanapata daraja la nne ama sifuri kwenye mitihani yao ya kidato cha 4.

    Ni chama pekee kinachoweza kuimarisha upinzani kutoka kwa vyama vingine kwa kuwanunua ama kuwahonga viongozi wa upinzani.

    Nina kubaliana na Mhe. Mrema kuwa CCM ni hatari tupu haishikiki, na itashinda kwa kishindo. Dawa ya hatari hii haiko kwenye kizazi hiki, hio itakuwa historia kama kunawanaoiandika

    Mr. Mrema niliisha kwambia kuwa nilifanya makosa kukudhamini 1995, kwani nafikiri akili yako iko pungufu na wala haustaili kuwa mbunge.

    Mungu inusuru Tanzania na majanga haya.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 11, 2010

    Ndio maana mda nlikuwa najua mpinzani ni Lipumba tu peke yake hawa wengine wakipewa ugali tu kila kitu wanaaachia,,,,@anony wa 2 jamaa kweli itikaf imempata kila kitu kitakuwa hadharani

    ReplyDelete
  13. safi sana Mh. Mrema kwa kumpa sifa Kikwete kwani amejitahidi sana na nivema watu wakiona jambo jema limetendeka walisifie sio mpaka uwe ccm, hata ukiwa chama kingine, sio kuka kimya na kuweka unafiki tuu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 11, 2010

    Upinzani wa kweli utatoka CCM. Baba wa Taifa aliwaambia hayo...lakini 15 Years sasa bado wapo watu hawaelewi alikuwa anamaanisha nini.

    Watanzania tunatia huruma.

    CCM itakuwa madarakani for another 100 Years. Watch this space...

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 11, 2010

    Msemaji wa kwanza anasema kuna watu hawampendi Kikwete sababu ya chuki binafsi. Hebu tuambie chuki binafsi ni nini hasa? Wangapi wanamja Kikwete kwa karibu mpaka wawe naye na chuki bibafsi. Kushindwa kuiongoza nchi kikamilifu na kukumbatia ufisadi ndio inaleta hawa watu kuuchukia utawala wa Kikwete na sio chuki binafsi. Tekeleza ipasavyo, nawe utalipwa ipasavyo!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 11, 2010

    HUYU anaesema ccm itatawala miaka 100 naona kalewa na siasa za nyerere, baba wako wa taifa katuachia ufisadi ule ule aliokuwa anauvumilia wakati wake na sasa jk anaendelea nao!!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 11, 2010

    MREMA PUMZIKA TU NYUMBANI SASA MAANA UTAFIA NJIA BURE UKIENDELEA NA SIASA. UBUNGE VUNJO NAKUHAKIKISHIA HAUTAPATA NG'OO. SASA KAMA CCM NI CHAMA KUBWA KWA NINI WATU WA VUNJO WACHAGUWE TLP BADALA YA CCM?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 11, 2010

    Siasa za Tanzania zinatia kichefuchefu

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 11, 2010

    Kweli Mangi ameishiwa sera ananitia aibu mzee huyu..Tanzania siasa chwe kabisa. Huyu anony wa kwanza anayesema JK kafanya mengi naye ZERO maana hata anachokisema hakijui. Vyote alivyotaja ni Initiatives za Mkapa kama hajui. Kuporomoka kwa shilingi hakuoni anaangalia vya kupita.Sisi tunataka kujitegemea sio kuombaomba kama Matonya..I have never come across a government badget with deficit on this world zaidi ya bajeti ya JK ya mwaka huu.
    Safari bado ni ndefu lol

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 11, 2010

    NJAA MBAYA SANA!!MWACHENI BABU WA WATU !! MIAKA YOTE KAKOMAA NA UPINZANI ANGALIA SASA KAVUNA NINI !! KACHOKA KULIKO WANANCHI WENYEWE WENYE HALI YA CHINI !! USICHEZE NA NJAA WEWE PLUS ANA FAMILIA YA KULISHA JAMANI !ONLY GOD KNOWS WHY !!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 11, 2010

    sijawahi kuona mpinzani wako unamumwagia sifa. hii jemba ni clown nini?

    ReplyDelete
  22. Advocate JashaJuly 11, 2010

    Kweli njaa inamsubua mrema kanunuliwa kwa kiasi gani hatujui kama CCM Chama kikubwa kimefanya mengi mazuri kwanini asirudi ccm ili kieleweke kwanini kiwepo TLP iwapo hakuna tofauti na CCM .Ukitaka kuiba ,kua fisadi, nakufanaya mabmbo yote bongo jiunge na CCM ni mwamvuli tosha kufanya kila ulitakalo.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 11, 2010

    watanzania always tunapenda kukandia sio kusifia,jkikwete kafanya mambo mengi sana na hasa ya ufisadi.tuangalie utawala uliopita ulivyokuwa wa ufujaji pesa mtu anakula ela za umma utadhani ni zake ila ktk utawala wa kikwete watu hao wameonekana na wengine bado wanakesi mahakamani ila tunaweza sema jk hana washirika wazuri walio na moyo wa utendaji kazi.MREMA OYEE SIFIA ULIPOPAONA PANAFAA SIFA.CCM JUU JUU JUU ZAIDI.na tukumbuke hii ni nchi sio nyumba ambayo unaweza kuiendesha upendavyo.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 11, 2010

    Mrema alichosema ni kwamba CCM na TLP ni vyama vya watanzania vyenye lengo la kuleta Uongozi bora.

    Haiwi sawia kwa yeye kumpinga JK eti kwa sababu tuu ni mpinzani> Asiwe mkweli hata kama kweli JK ni mzuri?

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 11, 2010

    acheni longolongo hapa,machinga complex ni plan ya jk,mkapa ameondoka barabara ya dodoma morogoro imelipwa na serikali ya jk,mkapa ndo chanzo cha ufisadi nchi hii,mikataba mibovu,na mambo mengi ya uozo,sema watu bado wanamuona mtu wa maana.ndo rais mbovu tz imewahi kupata,kawanyanganya wananchi mererani na kuwapa wa south africa.

    ReplyDelete
  26. Tumerogwa,na aliyeturoga ameshafariki.Hawa akina Mrema ni kiwakilishi tu cha hali hiyo.Nasema hivyo kwani hakuna namna tunavyoweza kueleza kwa uhakika kwanini licha ya ugumu wa maisha na umaskini unaowakabili Watanzania wengi,wahanga hao bado wana mapenzi ya hali ya juu kwa CCM- chama ambacho kwa vyovyote hakiwezi kukwepa lawama kuhusu umasikini wa nchi yetu.Hebu angalia hao wenzetu wanaopongeza takwimu na kupuuza hali halisi ya mtaani.Tukiendelea na mtindo huu basi ni dhahiri vizazi vijavyo vitavunjavunja makaburi yetu kwa hasira kuhusu nchi tutakayowaachia.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 12, 2010

    MREMA CHOKA MBAYAAA! AROSTO AMESHAZEEKA!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 12, 2010

    Uliyekuwa mdhamini wa mrema nimekukukubali, barabara machinga complex zote ni plan zilizokuwepo, tunatakiwa sasa kupima from the life starndard level, CCM todate nduio chama kilichotulostisha, kama anasema ni chama hakishikiki si anaruhusiwa kuchukuwa kadi, Kweli nimeamini maisha tight mzee mrema sikuhizi anatembea na gari bila kiyoyozi!!!!!!hata mimi nimemfunika.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 12, 2010

    This guy lacks depth and genuine conviction. Anapenda makofi tu, no character. Anatia kinyaa

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 12, 2010

    MIMI NAONA MREMA ANA MATATIZO YA AKILI NI BORA AKITOKA KIZOTA ASOGE MIREMBE AKAPATA MATIBABU KWANI HUYU MZEE NI MGONJWA ANGALIA USO WAKE ULIVYOBABUKA MUONEENI HURUMA HAJUI ATENDALO.

    RIP.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...