Hi mwana libeneke pole na majukumu ya kutuandalia miseto mbali mbali mimi ninaombi moja uiwafikishie wadau kwa sisi wa kazi wa mbagala chalambe na majimatitu. Sisi tunapata shida sana na ndugu zetu TANESCO wamekuwa wakitusumbua sana kwa kutukatia umeme mara kwa mara kila ifikapo saa 1:00 asubuhi mpaka saa 12:00 kamili za jioni na kukata tena saa mbili mpaka saa 4:00 usiku au unaweza usirudi kabisa
Sasa kiukweli wamekuwa wakituongezea gharama kwa kushindwa kuhifadhi vitu kwenye majokofu kwani mara nyingi hupata hasara na hufanya hivyo bila hata kutoa taarifa hii inakera sana sasa kwa mujibu kwa wa kutaka kupata manufaa na kuongeza pato la serikali tutafika kweli hii haina tija kabisa wako mdau katika kufanikisha maendeleo ya taifa letu.
Mdau Mbagala Charambe
Tumia kura yako vizuri uchaguzi huu.
ReplyDeleteFUATA HAYA MAMBO MATATU (3)
ReplyDelete1 - ACHANA NA UMEME WA TANESCO
2- KAKATE NYAYA ZOTE ZA TANESCO NA MUWARUDISHIE MAANA HAZINA FAIDA KWENU ( sana sana zitawaletea hasara ya kuunguliwa na vitu mkapata maumivu zaidi)
3- MCHANGISHINE MKANUNUE SOLAR NDO KILICHOBAKIA MIMI NITAWAFUNGIA MTAPATA UMEME BORA BILA YA KULIPA BILI TENA KWA MIAKA 20 KWA NYUMBA 100 NA KUTUMIA PASI KASORO JIKO NA AC-[KIYOYOZI]
Mbagala ndio mnaongoza kwa kuibeba CCM na hayo ndo malipo yake naTANESCO wanampango wa kuwaongezeni muda wa mgao kwa siku badala ya masaa 4 sasa itakuwa masaa 14 ili sisi wa osterbay tusipate shida.Hivi huko mbagala kuna nini cha muhimu?.....CCM Oyeeee..Mdau Masaki.
ReplyDelete