AMINA SALEH MOLLEL (SHOTO) AMBAYE ANAWANIA UBUNGE VITI MAALUM ,UPANDE WA WATU WENYE ULEMAVU AKICHUKUA FOMU TAYARI KWA KUANZA MCHAKATO HUO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mume Wangu, Mikanjuni TangaJuly 23, 2010

    Ni yupi kati ya hawa wanaopeana hiyo karatasi ndio mgombea huo ubunge??? Wa upande wa kulia au upande wa kushoto??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2010

    mboma naona wanaochukua form wa ccm tu wa vyama vingine hawachukui?au hampati habari zao za kuchukua form?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2010

    NILIKUWA SIJUI KAMA AMINA MOLLEL ANA ULEMAVU NAMSIKIAGA KWENYE RADIO KICHEKO KIIINGI TU. ANA ULEMAVU WA NINI? SAMAHANI KAMA NITAKUWA NAULIZA SWALI BAYA. HALAFU VITU MAALUM HAVINA MKOA MAALUM AU NI KWA TANZANIA NZIMA?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2010

    Mimi nimemfundishs Amina Molel akiwa Sekondari, namtakia heri kwani amethubutu kujitokeza na kutoa mchango wake. Hongera Amina na Kila la Kheri.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2010

    Samahani kuuliza sio ujinga, kwani dada Amina Mollel ana ulemavu? au mtu yeyote yule anaweza kuwakilisha nafasi hiyo hata kama si mlemavu. Tafadhalini naomba mnielimishe.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2010

    Lazima kuna pesa zinazotolewa kwa hawa wanaochukuwa hizi fomu za kutaka kuteuliwa kugombea ubunge ndani ya "shiishiiemu".Mwanzoni nilidhani ni "unazi" wa Michuzi sasa napatwa na mawazo tofauti.Itakuwa ni zile "loop-holes" ambazo wenye akili wanazitumia kikamilifu kupata ulaji wa siku mbili tatu baada ya hapo wanatulia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2010

    Jamani hivi viti maalum karne ya 21 ni vya nini? Kwanini wanawake wasigombanie kama watu wengine? Mbona kuna wanawake wanagombania nafasi mbalimbali kwa kura kwanini tusitumie mfumo huo moja kwa moja? Let us fight the hard fight ndio tutapata changa moto hivi vitu vyakutafuniwa sipendi kabisa ndio tunajikuta na viongozi vilaza.Tutajivunia zaidi ukombozi wetu kama tukifight for ourselves sio kubebwa kwenye viti maalum ladies.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2010

    Jamani waliouliza ni vyema wakajibiwa. Dada Amina ana ulemavu wa mguu, ndio maana anagombea nafasi hiyo. Kwa maoni yangu naona atakuwa wakili mzuri sana kwa haki za walemavu katika huo mjengo wa kutunga sheria. Sifa yake kubwa ni kutokukubali ulemavu wake kumuweka nyumbani, amekuwa na bidii mno katika kazi yake. Amerejea juzi tu kutoka Nepal, mashariki ya mbali alikokuwa anasaka ujuzi na uzoefu zaidi wa kikazi. Amina ana upeo wa ziada, Mchamungu, mpole, msikivu na mwenye kupenda kujifunza. Kwa umri wake atatufaa sana katika nafasi hiyo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2010

    KWELI SIASA YA TZ IMENOGAAAA...HIVI KWELI WATAWEZA KUFACE CHALLENGES ZIKIUCHUMI ZILIZOPO DUNIANI....KWELI KIKWETE ATAKUWA NA KAZI....

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 26, 2010

    Hivi jamani viti maalum viti mpaka lini. Hata JK alisema wanawake wengi ni watendaji wakipewa fursa. Mimi nasema achaneni na woga wa kijinga. Mbona wanawake wa Rwanda ndio wanaoongoza kwa asilimia bungeni kuliko nchi yeyote duniani(56%) ikifuatiwa na Sweden(42%)?. Tena wengin ni wamajimbo. Shauri zenu endeleeni kulelewa na vya bure. Nendeni Rwanda mjifunze.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...