Na Woinde Shizza,Arusha
Ikiwa mashindano yajulikanayo kama Safari Pool national champion ship yanatarajiwa kuanza kutimiua vumbi hivi karibuni na fainali zake zinatarajiwa kufanyika mkoani Arusha kampuni ya bia ya TBL imeanza maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo
Kampuni hii imeanza kutoa hamasa katika sehemu mbalimbali za mjini hapa ikiwemo katika bar ambazo zina washiriki wengi ambao wanapenda mchezo huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya mmoja wa wahamasishaji wa mashindano hayo alipoojiwa na blog ya jamii kuhusiana na hamasa hiyo alisema kuwa wameanza kutoa hamasa kwa kufanya promosheni kido kidogo ya kuwataharifu wakazi w amkoa huu kuwa mashindano haya yanafanyika mkoani hapa.
Alisema kuwa kuna baadhi ya zawadi ambazo wanazitoa kwa ajili ya kuhamasisha watu na pia alibainisha kuwa pamoja na kuwahamasisha watu pia wameandaa mashindano.
Alisema kuwa mashindano wanayafanya kwa sasa ni yanajulikana kama speed pool ambayo yanachezwa kwa kutega sekunde na mshindi anayepatika anagaiwa zawadi.
Hiyo ship ya Champion inaingia lini bandarini? duuh leo mnenichekesha.
ReplyDelete