NA MAGRETH KINABO
NA BENJAMIN SAWE
MAELEZO, DODOMA
1/07/2010

WAZIRI Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema kwamba Watanzania watakaouza ardhi kwa wageni kutoka nje ya nchi mauzo hayo yatafutwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana Bungeni na Waziri Mkuu Pinda, wakati akijibu maswali ya hapokwapapo Bungeni kuhusu swali la Mbunge wa Gando(CUF) Khalifa Suleman Khalifa lilioulizwa je Serikali inatoa tamko gani kuhusu Watanzania watakaouza ardhi kinyemela wakati wa utekelezaji wa Soko la Pamoja?

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Pinda alisema chini ya mkubaliano ya soko hilo , yapo maeneo mengi ya kufuata sheria ya nchi, hivyo bado sheria ya nchi inatawala. Masuala la ardhi ya Tanzania yatakuwa ni masuala ya sheria kama ilivyo katika hati ya kusafiria(passport).

“Ninatoa wito kwa Watanzania kwa kutambua Sheria ya Ardhi bado ipo si busara wale watakaokiuka kisheria mtu kuuza ... ikigundulika mauzo haya yatafutwa,” alisema Pinda.

Alisisitiza kuwa mtu kutoka nje ya nchi
hawezi kumiliki ardhi labda kama ni kwa ajili ya uwekezaji.

Katika swali lingine la nyongeza la Khalifa lililouliza kuwa Serikali inatoa kuli gani kuhusu waajiri binafsi watakowafukuza Watanzania kufuatia soko hilo kuanza na kuwaajiri watu kutoka nje ya nchi.

Waziri Mkuu, Pinda akijibu swali hilo , alisema suala la ajira halitakuwa la kiholela, hivyo aliwasisitiza waajiri kutoa kipaumbele cha ajira kwa Watanzania na ajira za watu wa nje ya nchi ziwe kwa wale wataalaamu ambao Tanzania hawapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2010

    Hamna jipya hapo ni politics tu, tumeshaliwa tutulie tu, we are the victims of political fashions. Eti sababu Ulaya wanaungana basi na si tuungane. Ama kwa hakika hakuna kitu nachokichukia dunia hii kama siasa. Mh. Waziri wa Africa Mashariki sitokusamehe maishani kwa kutuletea sebuleni wale waliotutukana enzi ile na kutuulia baba zetu kwa chuki zao. Michu ipotezee ukipenda

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2010

    Iwapo mie nilijivunja kiuongo na kuchikua mkoba wa kigeni, sasa ndugu na jamaa wakikitaka kibanda changu si watanilipua kwa crown wapate mali zangu? Lakini wakati wa biashara, muuzaji haulizi pasi kwani tulisoma wote primary na anajua mie mbongo ila viwanja vingi tu. Kazi hapo
    BM

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2010

    Kwa nini Watanzania wanaogopa ardhi yao kutumiwa na wageni? Asilimia 90 ya Watanzania ni wakulima. Kwa kuwa ni wakulima wadogo wadogo hawana uwezo wa kulima kwa wingi. Kama kuna makampuni au nchi kama Korea Kusini au Saudi Arabia ambao wanakodishwa ardhi ili walete kilimo bora na watu kupewa ajira, kwa nini wakatazwe? Je, ni bora ardhi kukaa bila kutumiwa kuliko kuuzwa kama italeta teknolojia mpya, ajira na pesa serikalini?

    Pili, kama serikali inataka Watanzania wapewe kazi kabla ya mgeni, basi wasingewaruhusu wageni waje kuishi bila ya kibali katika umoja huu. Huwezi kumkaribmgeni mgeni aishi bila ya viza na hapo hapo humruhusu kufanya kazi, atakula wapi?

    Kwa sasa, elimu yetu ipo nyuma na wenzetu Kenya na Uganda. Vyuo vyetu havina elimu ya kisasa na Kiingereza chetu ni kibovu. Kenya wana vyuo vya Marekani na vyao vinavyotoa MBA (Master's in Business Administration). Mimi kama mwajira wa Kitanzania katika biashara yangu, nitampa ajira Mkenya kwa kuwa ala elimu bora, Kiingereza kizuri na anaheshimu kazi yake kuliko Mtanzania ambaye kutwa analalamika akipewa kazi nzito. Tajiri mara nyingi anaonekana kama mnyonya damu, sio mtoa ajira wala mlipaji kodi.

    Huu umoja wa EAC hauwezi kwenda mbele mpaka wananchi wake wote wapewe haki moja: haki ya kufanya kazi katika nchi zote, haki za kununua ardhi, na haki ya kufanya biashara kirahisi kama wanavyofanya Jumuiya ya Ulaya (EU). Hata Uingereza imeona jinsi Wapolish na Waromania walivyoivamia kufanya kazi lakini hawawezi kuwafukuza kwa kuwa wapo katika EU.

    ReplyDelete
  4. MIMI NAKUBALI NA WAZIRI WETU KUHUSU AJIRA YA WAGENI HAPA TANZANIA KWA SABABU SISI WATANZANIA HATUNA ELIMU ZA JUU.LAKINI KWA UPANDE MWINGINE INA KUWA NI MNYANYASIKO KWA MTANZANIA AMBAE ANA HAKI ZAIDI KWA NCHI YAKE NA MTEGEMEZI WA NCHI YAKE,NA KWA MAONI YANGU MIMI NAONA KWAMBA KAMPUNI YOYOTE IKIWA INA ENDELEZWA AU AKIWA MENEJA MUAJIRIWA MGENI, HATA WAFANYAKAZI WA ELIMU YA CHINI WANALETEWA KUTOKA NJE NA MISHAHARA YA JUU,NA KAMA SISI WATANZANIA TUKIPEWA MSHAHARA WA AINA HIYO TUNAWEZA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KWA NGUVU ZOTE.NA HISI KWAMBA ELIMU YA KIASI HICHO HATA WATANZANIA TUNAYO.WATANZANIA AMKENI LASIVYO TUTABAKI NA UMASKINI WETU HIYO MAISHA NZIMA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2010

    Kwa hiyo wanaweza kukodisha ama? naona hilo swali halikumaliziwa..

    Kuna wazungu wanaown shamba kubwa sana kule Moshi na walikuja tu vuuuuup ina maana kuna sheria ya kutowauzia raia wa nje ardhi...wale watu wanahilo shamba kama heka sijui ngapi vile...sasa sijui wao walinunuaje? Walitokea sijui zimbabwe au south africa...Hizo sheria hazikuwakuta au waliouza walikua hawajui \

    na akisema ardhi ni ya watu wanje wanaokuja kuwekezaji na hao wakenya si wanakuja kuwekeza pia? mtu akija kununua shamba na kuanzisha kilimo si amewekeza sijui sheria ya kuwekeza ina maana gani na itatofautishwaje hapo naona kama tunajifunga vile...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...