MAREHEMU MRS DAFROSA .T. LING’ANDE

FAMILIA YA MAREHEMU MZEE SELEMANI .A. LING’ANDE WA MWANANYAMALA A, TUNAPENDA KUWASHUKURU WOTE KWA MOYO WENU WA HURUMA NA UPENDO MLIOTUONYESHA KATIKA KIPINDI CHOTE KIGUMU TULICHOPITA CHA KUMPOTEZA GHAFLA MAMA YETU MPENZI MAMA LING’ANDE KILICHOTOKEA TAREHE 19/6/2010 NA KUZIKWA 21/07/ 2010 KATIKA MAKABURI YA KINONDONI, MWENYEZI MUNGU AWABARIKI WOTE.

SHUKRANI ZA PEKEE ZIWAFIKIE PAROKO PAROKIA YA MWANANYAMALA, FATHER MBIKU NA FATHER MAHALU WA PAROKIA YA UDSM KWA HUDUMA ZA KIROHO, UONGOZI NA WAFANYAKAZI WOTE WA KITUO CHA MAELEZO YA AFYA – MUHIMBILI, WANAJUMUIYA WA JUMUIYA YA MT. JOSEPH MFANYAKAZI, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WOTE KWA UJUMLA. MUNGU WABARIKI SANA.

TUNAOMBA MSHIRIKIANE NA SISI TENA KATIKA MKESHA WA AROBAINI SIKU YA IJUMAA TAREHE 30/07/2010 NYUMBANI KWETU MWANANYAMALA A NA ASUBUHI YAKE JUMAMOSI 31/07/2010 TUTAKUWA NA MISA YA KUMUOMBEA MAREHEMU KATIKA KANISA KATOLIKI PAROKIA YA MWANANYAMALA NA BAADA YA HAPO SAA 7 MCHANA TUTAKUWA NA SADAKA YA SHUKRANI .

MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAMA YETU MAHALA PEMA PEPONI AMEN

NYOTE MNAKARIBISHWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2010

    R.I.P Mama

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2010

    R.I.P Mama

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2010

    Ooh MAMA Ling'ande, upumzike kwa AMANI.
    Bwana ametoa Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.
    Amen

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2010

    Nimeliona hili tangazo nikashtuka sana maana mimi ninaishi nje ya Tz kwa miaka karibu kumi sasa. Ila nilipoona picha yake tu nikamkumbuka kuwa ni mama mpole na mwenye hekima tele ambaye alishawahi kunipokea na kunipima damu pale muhimbili na kunipatia ushauri nasaha MIAKA YA TISINI ZA MWISHONI. Pamoja na kuwa majibu yangu yalikuwa mazuri lakini alichukua muda wake na ubusara wake kunipa ushauri nasaha na mara zote mbili nilipoenda na kukutana naye katika miezi mitatu alikuwa mwenye upendo, mnyenyekevu sana na tabasamu halikukosekana usoni mwake. Mama PUMZIKA KWA AMANI MAPAKA KIAMA NA KWA NEEMA ya YESU KRISTU AKAKUFUFUE SIKU YAKE HIYO. AMEN.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2010

    Mama, nitaendelea kukumbuka sana katika maisha yangu kwa jinsi ulivyokuwa na upendo na hekima, kwani ulikuwa mtu wa kufunza na kutoa wosia wa maisha kila nilipokuwa naona na wewe, nitakuombea daima kila nitakaposali katika sala zangu pamoja na familia yangu. Tunachoamini kilichokufa ni mwili kiroho uko nasi, na wewe uwe mwombezi wetu! Kwani naamini uko karibu na Bwana Yesu! Kwani siku ya mwisho ulijikabidhi kwa Mungu Baba kwa sala kama kawaida yako, na muda si mrefu ulipatwa na mauti! Raha ya Milele Umpe Ee Bwana...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...