Hi Bw. Michuzi a.k.a Misupu

Naomba usinibanie ili uniwekee swali la kizushi kwenye BLOG YA JAMII ! Mimi ni mwanachama wa YANGA mwenye kadi nambari 000491 niliyeko mkoani Mbeya. Na kadi hii niliipata 2008 Machi 26 kwa kupewa na Katibu wa Tawi, Mkoani Mbeya Bw. M. G. Msigwa.

Na niliilipia hiyo kadi kwa mwaka huohuo wa 2008. Sasa swali langu ni kuwa, je na sisi wa mikoani tunahitaji kuwa na kadi mpya dhidi ya hizi tulizonazo ? Kwani tulisikia wakati wa UCHAGUZI MKUU uliofanyika majuzi hapo DSM, ulitakiwa uonyeshe kadi mpya ambazo zilishalipiwa na MANJI ndio uingie kupiga kura !!!! Mimi sijalipa tokea mwaka 2008, je ninadaiwa kiasi gani mpaka sasa ili nijulikane ni mwanachama hai ??

Na je nikitakiwa kulipia hiyo kadi mpya niende wapi ili nikalipie ili nipate kuwa mwanachama hai ???? Naomba hayo maswali yangu yapatiwe UFUMBUZI ili niweze kulipia na kuwa mwanachama HAI. Kwani inaniuma ninapojihisi kuwa siko HAI kichama. YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO !!!!!

Mdua Mkereketwa
Namba 000491

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. yanga bila manji inawezekanaJuly 22, 2010

    bana kadi yako mimi bado tambua kama mimi bado lipia veve sio halali bana mimi manji nalipa yote kadi yanga uliza madega mimi patia pesa yeye yanga bila maji ina wezekana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2010

    sion umuhimu wa mtu wa mbeya kushabikia yanga,tuewe km wenzetu jamani,shabikia timu ya mkoa wako,bila timu ya mkoa wako unadhan hata hyo yangu itakuja huko mbeya??,ni muda wa watz kuamka bwana,changia timu ya mkoa wako,tazama mechi zao na hyo ndo inadumisha soka n upinzani wa kweli,mtu wa iringa anashabikia simba sasa wapi na wapi jaman??,sa matokeo yake lipuli imekufa na hao simba mbona hawaji hapo iringa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2010

    Mkereketwa kwanza nakupongeza kwa kupenda kuchangia timu yako. Wanachama wote wa vilabu wangekuwa kama wewe, matatizo mengi yaliyopo yangetatuliwa. Kuhusu ada, wakati wa mkutano wa kupitisha katiba uliofanyika June 2010, Manji aliwalipia kwa miaka miwili wanachama wote waliopo ktk leja ya klabu kwa hiyo ni vyema kuhakikisha kama jina na kadi yako vipo ktk leja maana vilabu vyetu hivi vikubwa ujanja ujanja ni mwingi sana. Ukiwasiliana na tawi lako hapo Mbeya watakusaidia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2010

    hauna kazi wewe, mwenye kazi awezi kuangaika na jambo la kipuuzi kama hilo !!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2010

    huyu jamaa ni mdua au mdau?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2010

    Yaani Mwanafyale kutokuwa hai kichama kwani Yanga ni chama cha siasa? Pole sana Mwanafyale yaani kutokuwa hai "kichama" kwa mapenzi ya Yanga nasikia umegoma kula maana unajiona kama utaliwa na Mnyama!

    ReplyDelete
  7. HAMAD ADENJuly 22, 2010

    KWANI WEWE NI LAZIMA UWE YANGA? AMIA TIMU NYINGINE YANGA SI UNAJUWA WANA MATATIZO? WAO VIONGOZI WAMECHAGULIWA JUZI TU LEO HAWAWATAKI JE WATAZITAKA KADI ZILIZOTOLEWA MWAKA 2008? FUNGUA MACHO NDUNGU YANGU WATU WANABADILI DINI ITAKUWA TIMU?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2010

    kwako mdau
    hongera sana kwa moyo wako wa kutaka kuwa mwanachama hai! kuna maoni tofauti lakini kila mtu na starehe yake kaka wala usijali wewe weka pamba masikioni njoo tuijenge dar yanga africans. lipia miaka miwili 2009/2010 na 2010/2011 ili uwe mwanachama hai katika akaunti ya crdb ya yanga africans akaunti namba 01J095095801 then peleka kwa katibu wa tawi lako utapewa risiti ya uanachama na kuwa hai. wako martin chacha- mwanayanga

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2010

    Annoy at 12:43 unamwambia mwenzako ashabikie timu za Mbeya mbona wewe ndio mshabiki mkubwa wa Manchester United?? Au Man U wanatoka Dar? Au hao Liverpool watakuja Tanzania bila ya wewe kushabikia Yanga au Simba?? Mutaamuka!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2010

    Unanyejiita mkreketwa wa yanga hakuna lolote!! Uzushi mtupu?? Huna kazi ya kufanya huko Mbeya mpaka ukae kila wakati unawaza mambo ya Yanga?? Yanakuhusu nini hayo? Mambo ya watu wa DSM? Huko mikoani si na kwenyewe kuna timu?? Kuna Mbeya star, Prison, n.k. Na ya Yanga yanakuhusu nini???
    Mdau!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...